ANTONIO APIGA SAHIHI MTINDO MPYA WA MUZIKI "SWAHILI SOCA."
Kila msanii kwa sasa yuko mbioni kufanya wimbo wake wa kufunga mwaka na hakuna anayetaka kuwachwa nyuma.Hivyo basi studio ya Newdawn records ikimtmbulisha msanii wake Antonio ; imeamua kufanya mapinduZi makali kimuziki.Billy Moyses,mmiliki na producer wa Newdawn records alidokeza ya kuwa msanii wake Antonio amekuja na mtindo mpya wa muziki kwa jina SWAHILI SOCA."Mtindo huu unachanganya fleva za muziki wa Trinidad na Caribean islands na fleva za hapa nyumbani pwani.Niliamua kufanya kazi na Antonio kwani ujuzi wake ni mkali wa kusonga na mdundo wa aina yoyote."Alieleza producer Billy.Nyimbo ya Antonio ni ya kupigiwa mfano mzuri kwani ipo style ya kipekee na ni ya kuchangamsha mashabiki.LEO NI LEO ni jina la wimbo na bila shaka wasanii lazima mtatoa kijasho chembamba kwa pigo hili la kufunga mwaka.
Comments
Post a Comment