Posts

Showing posts from November, 2015

HIVI JE KUNA GHOST MUSICIANS WANAOLIPWA NA MCSK KISIRISIRI.YAMEMWAGIKAAAAA!!!!!!!!!SOMA HAPA!!!!

Image
 Wasanii kadhaa wa Nairobu na wengine wa hapa pwani wameamua kuleta vurumai na mwamko mpya. Jamaa hao walioamua kutolala njaa wamesema kuwa kunao wasanii ghost yaani wasiojulikana wanaoliopwa kisirisiri na MCSK.  Kundi flani la wanamuziki hapa Pwani wameshikana na wenzao wa Nairobi na kusema wataandamana kwa ajili ya "Ghost Musicians" wanaodaiwa kulipwa huku wengine wakililia patupu. Vilevile wasanii wa Pwani wanachukua miaka na mikaka kupata nambari ya membership. Regional Director wa MCSK hapa pwani bwana Sango naye amekuwa kimya licha ya kutoa ahadi tele kwa wasanii.

DIAMOND ASEMA HASHIKI SIMU YA ZARI KWA SABABU HATAKI KUUMIA MOYO.

Image
Daah hii sasa balaa tupu,ingawa wana mtoto masuperstar hawa wawili bado wana matatizo ya uaminifu. Diamond president wa Wasafi amemwaga mtama kwenye kuku wengi na kudokeza hadharani kuwa hawezi kamwe kushika simu ya mkewe Zari kwa sababu hataki kuumia moyo. Swali ni je wewe waweza shika simu ya mumeo ama mkeo? “Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa,” alijibu Diamond alipoulizwa na Millard Ayo kama huwa anashika simu ya Zari. Diamond aliendelea kutoa sababu za kutoshika simu yake, “sidiriki kwasababu namjua ni binadamu , unajua sometimes ukizingatia na yeye (Zari) ni mtu maarufu so sometimes watu wengine wanakuwa wanamsumbua, anaweza kukutwa na vishawishi sometimes anaweza akamjibu mtu akaitikia tu poa, kwangu mimi kikanikwaza kwasababu nampenda kwahiyo ikaniumiza, kwahiyo sitaki kabisa kushika simu yake.” Pamoja na kwamba yeye hashiki simu ya mpenzi wake, vipi kuhusu Zari kushika simu yake? “ Simu yangu mi haina password naiachaga tu lakini nafi...

RICH MAVOKO ATUMIA MKOROGO KUWA MWEUPE??? .DAAAH CHEKI PICHA HAPA!!!!

Image
Afrika Mashariki inajivunia kipaji cha Rich Mavoko ambaye kwa sasa ameachia kibao kipya kwa jina NAAMINI. La kushangaza ni kuwa jamaa huyo amezidi kuwa mweupe kila uchao. Sijui anataka kujifanya Michael Jackson au vipi ila kulingana na blog ya Bongo Swaggz picha hizi zake za zamani na za sasa zitasema yote. Kabla

TAZAMA BEHIND THE SCENES YA VIDEO YA "BILA WEWE" YA DULA THE AFRICAN SONGBIRD.

Image
Anaitwa Triple A au ukipenda Dula the African Songbird na chini ya A million videos ya Khalid produza ameandaa video ya wimbo wake BILA WEWE.Video hii atakayo iwachia 3rd December itasumbua sana.Cheki behind the scenes hapa.

"INTERCONTINENTAL SCAR" YA HUSTLA JAY YAPATA TEULIWA KWA TUZO ZA KIMATAIFA ZA FRANCE.

Image
Tulimsikia kwa Mara ya kwanza kwa kibao MINYORORO YA HAKI iliyoshika chati sana na kufanya mapinduzi kwenye sanaa ya Afrika Mashariki. Hustla aliye na hulka ya kuifundisha jamii kwa kupigania haki kupitia muziki wake ameteuliwa kuwania tuzo fulani ambapo video yake imechaguliwa katika kipengele kimoja kwenye tuzo hizo.  Kumpigia kura Send the number " 2 " on email finale@lereveafricain.com / 1 email address = 1 vote

FYATENI NDIMI ZENU WANAHIPHOP WA PWANI WANAOJISHASHA FACEBOOK. TAZAMENI RAPPER MKALI WA FASTCASHMUSIC GROUP ANAVYOMWAGA MICHUZI!!!!

Image
 Huwa wafokaji wa pwani hupenda kupiga kelele mitandaoni jinsi walivyo wakali na muziki wao unvyotamba.Kumbe zote huwa kelele tu ila hakuna kazi yoyote inayofanyika. Ndiposa wakati mwingine inapaswa turudi chini na kunyenyekea na kuwa wakweli. Sio kujisifu na kukashifu presenters kuwa hawachezi miziki na nyimbo zenu mpya ilhali bado mnatapatapa na kuandaa vitu borohoa. Hivyo basi, tazameni mwanahiphop kwa jina KRG ceo wa FASTCASHMUSICGROUP anayetokea Nairobi anavyovuja mkwanja.  Jamaa huyo alimnunulia demu wake bonge la gari baada ya kumrushia Party.  Cha msingi ni STAY HUMBLE ALWAYS.

MAHABUBA ISHAPIKWA IKAPAKULIWA! TAZAMA VIDEO YOTE HAPA!!

Image
Imekuwa midomoni mwa watu na imetrend mitandaoni kwa sana tu. Ila Leo lazima kieleweke...Tunazungumzia video ya Mswazzi Masauti "Mahabuba." Produza Tedd Josiah amewatoa wasanii wengi tu na hapa hajacheza karata zake vibaya. Mahabuba, video iliyochukua siku sita ikiandaliwa sehemu tofauti huku pwani lazima itasumbua sana sio kwa runinga, radio, mitandaoni hadi mitaani. Mswazzi Masauti amejaribu kuweka fleva za kimwambao kwenye mdundo tulivu wa rnb uliokolea nyuzi za gita na sauti tamu za vinanda. Video maridhawa yenye mvuto mzuri na rangi za kupendeza zilizooana vyema na ujumbe unaopitishwa imeleta dhana nzuri kwa mada ya mahaba inayozungumziwa. Tusitumie mate ilhali wino upo.......video yenyewe hii hapa.Tazama kisha utoe maoni--------

HIVI HUYU "KUNGURU MWEUSI" NI NANI?????

Image
Chikuku Abdhalla almaarufu Chikuzee aliyesikika kwa Mara ya kwanza ndani ya Thundersounds records chini ya producer Morbiz aka Sherif ameamua kuwachia kibao kipya kuongelea mtu fulani.Chikuzee kweñye wimbo wake mpya KUNGURU MWEUSI ameongea kimafumbo kumsuta mtu fulani.Hivi swali ni huyu kunguru mweusi chikuzee anayemuimba ni nani?

LOO!!! MSANII KUTOKA KAUNTI YA KWALE AMUUZA MKEWE KWA SHILINGI 500KSH.

Image
MSANII TOKEA PAPA HAPA PWANI MAENEO YA KWALE ALIMUUZA MKEWE KWA SHILINGI 500 PEKEE.TUKIO HILI LA KUTAMAUSHA LILIWASHANGAZA WENGI KWANI WAWILI HAO WALIKUA WAMEOANA KWA MIAKA MINNE.MSANII HUYO KWA JINA MWACHAMBULI SARIA ALIMPIGA BEI MKEWE ANAYEJULIKANA KAMA ADA KASSIM KWA RAFIKIYE BAADA YA NDOA YAO KUINGIA DOA. ZAITWA KUKURU KAKARA ZA SANAA YA PWANI. Picha kwa Hisani ya #TaifaLeo 

CHANGEZ NDZAI AIKABILI SANAA YA PWANI VILIVYO.

Image
Msanii Changez Ndzai, ambaye kwa wengi wanamfahamu kwa uandishi wake wa mashairi na pia hivi majuzi aliachia kibao chake cha kwanza kwa jina ''Msaada'', ameamua kuchukua hatua madhubuti ilikuona anapanda katika ngazi za juu kwenye sanaa. Changez amekua akitembea kutafuta Shows Malindi hapa Mombasa na Kilifi. Akielezea meza yetu ya habari kwanini amekua akipeana shows kipao mbele kuliko radio airplay, Changez amehoji mashabiki wa kweli wako kwenye hizi show. Alisistiza kuwa shows mbali nakuumpa msanii kipato zinampa msanii twaswira kamili kama kweli anafaa ama hafai, kwake yeye anasema ameshangazwa sana na mashabiki vile wanavyo mshobokea kazi zake tokea spokenword hata nyimbo.

BAADA YA MIAKA MITANO PRODUZA AMMZ AWACHA KAZI SQ RECORDS LEO HII.

Image
Baada ya kufanya kazi miaka mitano ndani ya SQ records, producer Ammz ukipenda Wa Leo au tone la maji Leo hii amebwaga chini vyombo vya kazi. Ammz ambaye ameproduce hits kibao tu chini ya Sq records alitudokezea haya hapo Jana na akasema ametoka studio ya SQ Records kwa nia njema na anawashukuru sana aliofanya kazi nao. Ammz amefanya kazi SQ kwa miaka mitano ambapo ni kuanzia 24th November 2010 hadi 24th Novembe r 2015. List ya maproduza wa SQ in order ni kama ifuatavyo: 1.V sita, 2.Shirko 3 K-kroniqs, 4.Tk2 5.Amz. Vile vile Ammz amedokeza kuwa mwaka ujao atafungua studio yake binafsi kwa jina TEMPOZ RECORDING STUDIO.

BROWN MAUZO -SIPENDI UKILIA

Image
Baàda ya kundi lake la Wawili Pekee kusambaratika, Brown Mauzo ameamua kutoangalia nyuma kamwe. Aliingia Mainswitch studios na kusababisha ngoma Kali zilizoshika chati vilivyo. Kwa sasa Brown yupo chini ya Ogopa DJs na ameachia kibao kwa jina SIPENDI UKILIA na video imefanywa na mkongwe wa hizi kazi Tedd Josiah.

HIVI JE HILI NI DHIHIRISHO KUWA WASANII WA MALINDI WAMESUSIA NZUMARI AWARDS?

Image
Baada ya Nzumari Awards kutoa list yao ya nominees na mashabiki kulalamikia baadhi ya vipengele vya nominees,wasanii wa hip hop wa Malindi wametoa listi yao ambayo bado hatujabaii Kuwa in ya awards ama nini. Listi hiyo iliyolenga wasanii wa hip hop pekee vilevile ina voting platform na ukiichunguza sana inaikashifu listing ya Nzumari hip hop artist of the year MOMBASA. List yenyewe ni hii THE BEST HIP HOP ARTIST MALINDI 2015 MCS KIWANJA K- MODE MC NDOMBI YOUNG NJITA KATOI WA TABAKA MITAA YA KISAUNI BOZEN YTE MONSTA WARA WARA HIVI JE MNADHANI NZUMARI AWARDS ILIWADHALILISHA WASANII NJE YA MOMBASA.....MANAKE MAENEO KAMA KWALE, VOI, KILIFI, MALINDI ETC WASANII WAO HAWAKUWEKWA KWENYE ORODHA YA NOMINEES INGALI WAO NI WA PWANI.

DAAAAAAAAAAH KWELI BILA SHAKA HII NI DISS SONG YA MWAKA-KASSAMONEY NA ODINAREH BINGWA WAWACHARAZA BAADHI YA WASHIKA DAU WA SANAA YA PWANI!!!!!!

Image
Bila shaka hii ni nyimbo ya kufunga mwaka na marapper Kassamoney na Odinareh Bingwa wameamua kumalizia mwaka kwa kuwacharaza vikoto vikàli watu fulani.Nyimbo hii kwa jina TO WHOM IT MAY CONCERN imetaja baadhi ya vitu vinavyoikandamiza sanaa ya pwani.Waliotajwa ni presenters,DJs,baadhi ya wasanii na waandalizi awards. Vilevile aliyedissiwa sana ni Kaa la Moto akiambiwa bado hajafika kimistari na apunguze maringo ya kike.Nyimbo hii yapatikana mdundo.......JISKIZIE MWENYEWE HAPA

NAFANYA MODELING PIA- DULLY MELODY AFUATA MKONDO MWINGINE.

Image
Baada ya kutoa kibao HONGERA na kuonja utamu wa sanaa, Dully Melody ameamua kuchukua hatua nyingine. Msanii huyu aliye chini ya Noor Mwamba alidokeza kuwa mabinti wengi wanamfuatilia sana na anaamini Kuwa mvuto wake wa kimwili, sura na sauti ndiyo kielekezo kikuu cha yeye kutaka kufanya modeling. Vilevile Dully yupo na ujio mpya atakao uwachilia hivi karibuni.

BAADA YA KUFURUSHWA KTN MWANAISHA CHIDZUGA APATA KAZI K24 TV.

Image
Alifungishwa virago na runinga ya KTN alipokuwa mwanahabari. Tunamzungumzia Mwanadada mwanahabari aliye na mizizi ya hapa pwani; Mwanaisha Chidzuga. Dada huyu kwa sasa ana wingi wa raha kwani kampuni ya Mediamax inayomiliki runinga ya K24 imempa ajira na tayari ashaanza kupeperusha matangazo. Kwa hiyo wapenzi wa Mwanaisha Chidzuga rudini makochini dada kesha rudi ulingoni.

MIMI HUSAIDIA NINAPOWEZA-NYOTA NDOGO AONGEA BAADA YA CHIPUKO LA CONJESTINA.

Image
Baada ya kuachia video YouTube ya kuhusiana na wasia wake kwa bondia wa kike Conjestina Achieng, mama mlezi wa sanaa ya pwani Nyota Ndogo amekuja wazi na kuongea kuhusu misaada yake. Japo kidogo Nyota alisema kuwa yeye hutumia ufanisi wake kimuziki kusaidia yatima........ "WATU WALIOULIZA YEYE NYOTA KAFANYA NINI KWAO MOMBASA NDIO AMTETE CONJE? Wengi wanafikiria kusaidia nikutoa mamilioni ya hela kutoka mfukoni mwako. Sina uwezo huo but kile kidogo uwa ninacho mimi ushea. NATUMAI MPO SALAMA. kwanza kabisa kwetu Mombasa nimejiusisha na mambo mangi na kujituma. Sijui kama unajua huwa nashughulikiwa watoto yatima kutoka nyumba tafauti mombasa hadi voi. Utoa nguo zangu mwenyewe ama za watoto wangu ama naomba watu fb kuchangia kutuma nguo ili zipewe watoto hao. Nafikiria kwa watu wamombasa wanaonifatilia vizuri wanajua. Nimetoka kwa maisha ya shida nikiwa mdogo hivyo unikumbusha mbali napoona watu wakipata tabu. kila skuku ya idd mimi ula na mayatima nitaitisha mchang...

UNAZUNGUMZIA MAHABA YA KIPWANI???? HIZI HAPA NYIMBO KUMI KALI ZAIDI ZILISHAWAHI TOLEWA NA WASANII WA PWANI!!!!

Image
TOP TEN BEST EVER COASTAL KENYA LOVE SONGS. 10.NAKUSUBIRI- ALKENIA LUV Iliandaliwa chini ya studio za MK2,Produza P-Lion. 9.AMINI MIMI-SUDIBOY ft SIMPLE BOY Produza Emmy Dee -JungleMasters 8.NATAFUTA-NYOTA NDOGO Nyimbo hii japo hatukumbuki iliandaliwa na Produza yupi ilijulikana kama PENZI LA UONGO pia. 7.CHRISTINAH- WAWINDAJI Ndugu hawa wawili walio na vipaji si haba walitayarisha kibao chao Christina ndani ya Blaque records ya producer Badagah. 6.SO NICE-CLD,CHIKUZEE,OHZY,RAZ MICHA & FLIM-C Kikosi hiki kiliandaa wimbo huu ndani ya Thunerdsound records. 5.KICHAPO CHA MAPENZI-KIGOTO Japo haikuvuma Sana,nyimbo hii yenye mahaba makali iliandaliwa na producer TK2. 4.ANANIPENDA- DADDY SELLLE & FAT S Kama vile ngonjera nyimbo hii ya wawili hawa iliwavutia mashabiki sana. 3.ANISA-KINGSTING & BEDBUG Uandalizi wake Produza Bablee wa Tabasamu records. 2.MAPENZI- JAY KINI & ALKENIA LUV Chini ya Mk2 studios, Rapper Jay Kini alimshi...

KHALFAN JULO MENEJA WA MJ ASEMA MENGI YANAPASWA KUFANYWA KWA BURUDANI LA PWANI.

Image
Baada ya ushindi wa Juma Shibe almaarufu MJ, meneja wake Khalfan Julo amepasua mbarika kuhusiana na tasnia ya burudani la pwani. Khalfan,ambaye vilevile ni muigizaji mkali na assistant director wa Coast Films alidokeza haya huku akimtayarisha Mj kwa ziara ya kuzuru Tanzania. Julo alidokeza kuwa pwani ina vipaji vingi na wakati umefika vipaji viweze kupepea. "Sio uimbaji au uigizaji,pwani imejaa vipaji tele na viongozi wa serikali wanapaswa kutilia mkazo kwenye ukuzaji talanta. Hii itasaidia sana vijana kujiajiri na kupigana na madawa ya kulevya."Alisema Julo.

"MAHABUBA" MSWAZZY MASAUTI TAYARI KUACHIA WIMBO MPYA KWA MTINDO MPYA!!!!

Image
Meli ya pwani imekita nanga na ya mgambo ikilia bila shaka kuna jambo. Alitamba kwa vibao kama uko mbali, Siwezi, Niko nawe na vinginevyo na ndiposa gwiji wa ukuzaji talanta Ted Josiah akamchukua kumtambulisha kwenye sauti mpya SWARNB. Masauti tayari ashatayarisha kibao kipya kwa jina Mahabuba kilichokolea wingi wa tanakali za uswazi na mvuto wa ndimi za asili ya kipwani. Huku tarehe ikiwa imepangwa 27 mwezi huu, kikosi cha SWARNB records kikiongozwa na Ted Josiah kwa Mara ya kwanza kitatambulisha kazi mpya ya Mswazi Masauti na Mashabiki lazima watakubali matokeo kwani palipo na wazee bila shaka hapakoseki jambo. Kwa hiyo, kaeni mkao wa kula Masauti anawaandalia Mahabuba.

FULL LIST YA WASHINDI WA TUZO ZA AFRIMMA.

Image
BEST MALE ARTIST IN WEST AFRICA Winner – Olamide BEST FEMALE ARTISTE IN WEST AFRICA Winner – Yemi Alade BEST FEMALE ARTISTE IN NORTH AFRICA Winner- Manal BEST MALE ARTISTE IN NORTH AFRICA Winner-Ahmed Soultan BEST EAST AFRICAN MALE ARTIST Winner – Diamond Platnumz BEST EAST AFRICAN FEMALE ARTIST Winner – Tsedenia Gebremarkos BEST MALE ARTISTE IN CENTRAL AFRICA Winner – Stanley Enow BEST FEMALE ARTISTE IN CENTRAL AFRICA Winner – Charlotte Dipanda BEST MALE ARTISTE IN SOUTHERN AFRICA Winner – Cassper Nyovest BEST FEMALE ARTISTE IN SOUTHERN AFRICA Winner – Busiswa Ngoku LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD Ladysmith Black Mambazo BEST MALE ARTISTE IN AFRICAN INSPIRATIONAL MUSIC Winner – Darey BEST FEMALE ARTIST IN AFRICAN INSPIRATIONAL MUSIC Winner – Betty Akna BEST AFRICAN CONTEMPORARY Winner – Charlotte Dipanda MOST PROMISING ARTISTE IN AFRICA Winner –Kiss Daniel BEST AFRICAN JAZZ Winner – Kunle Ayo BEST AFRICAN POP Winner – Vanessa Mdee BEST AFRICAN ...

SIO JICHO NINALOZUNGUMZIA BALI JICHO LA MOYO-SHINEY ANNE APIGIA MUHURI UJIO WAKE MPYA.

Image
Huku idadi ya wasanii wa kike ikizidi kuyoyoma,Shiney Anne amejaribu kuziparaga kuta za sanaa ya pwani na kutaka kufikia kilele.Binti huyu aliyechini ya studio za Bigfoot ameachia kibao kwa jina Jicho ambacho wengi wa mashabiki wamewachwa mdomo wazi kwani hawajui ni jicho gani linaloongelewa.Ni jicho kama kiungo cha mwili ama ni ujumbe fiche? Kutufafanulia zaidi huu hapa usemi wa Shiney kuhusiana na wimbo wake......."Wimbo jicho nazungumziama jicho la moyoni.Kwa hio hata vipofu macho wako nayo ila wanaona kwa moyo.Nyimbo yangu mpya haijabagui vilema wa macho.Naomba mnipe support kwa ujio wangu mpya."