Promoter wa Wasiojali Band Athman baba akizungumza na mmoja wa wadaku wetu amesema Chapatizo ambaye alikuwa ameimba nyimbo hiyo pamoja na Susumila, nakuihama green house aliacha wimbo huo bila kuifanyia mastering na hata kutishia kuifuta baada ya Susumila kuifanya tena na wasojali band. Promoter huyo amedai msanii tajika Susumila aliataka vijana hao kurudia stanza kadhaa, hali ambayo ilichochea kufanywa upya kwa nyimbo hio ambayo kwa sasa imetoka na iko kwenye radio mbali mbali, lakini hilo linamuuma sana Chapatizo ambaye aliagiza ngoma ifutwe akidai aligharamika kwa kuitengeneza ngoma . Ngoma hiyo inayo julikana kama Jirani iliachiliwa wiki iliyo pita na kwa sasa inafanya vizuri baada ya Susumila kupush kuachiliwa kwa pini hilo. Kundi la wasojali linawajumuisha Ability,Hamso , Jaybro na Kamalu. By Nina Kagia.