Mwanamuziki tokea pwani ya Kenya,P-day ametoa kauli yake kuhusiana na matukio ya mauaji ya wazee wanaoshukiwa kuwa wachawi pande za Kilifi. Msanii huyo aliyetamba kwa kibao tarumbeta,Nylon guitar,Visingizo,Niringe naye na vinginevyo amedokeza haya kupitia ukurasa wake wa facebook akikashifu vikali vitendo hivyo. P-day alisema ya kwamba usemi wake anaopenda kuusema kwa nyimbo zake....."MZEE HATEMEWI MATE" unapaswa kuwa kauli mbiu itakayochukuliwa na kuwekwa kama mtajo utakaowaokao wazee kutoka kwenye janga hili. Tukinukuu kutoka alichonakili kwenye akaunti yake ya facebook..... "Social cohesion department to buy the mzee hatemewi mate lebol ( uzee si uchawi ) nliamka tu nkatunga hii lebol din't know itafika huku ........Sasa vijana kilifi county walianza kuua wazee kwa kua niwachawi BT sio Kila mwenye mvi ni mchawi ..let's respect the old" JE MAONI YAKO NI YAPI KUHUSIANA NA PENDEKEZO LA P-DAY KUHUSIANA NA WAZEE KUUAWA?
Mwanadada kutoa Tanzania Ray C, Ametoa picha zake wakati alipokuwa anatumia mihadharati, picha ambazo zimezua hisia kali katika mitandao ya Jamii. Ray C ambaye alichukuliwa na Rais wa TZ Jakaya Kikwete na kupelekwa kwenye rehab kwa sasa yuko katika hali nzuri ya afya na ameanza kazi zake za mziki huku single yake ikitarajiwa kutokea hivi karibuni.
Ni msanii aliyekubalika na wengi na aliyevuma kwa vibao motomoto kama; mtoto wa shule,umaskini si kilema,kadem,toka nenda,kadem kameparara na nyinginezo. Msanii huyu aliyemaliza shule ya upili mwaka uliopita alifuzu na kuchaguliwa kwenye kikosi cha askari polisi kitengo cha AP. Ranny aliyekuwa studio ya Homeworks na kuhamia studio ya Mwamba records kwa sasa yupo kwenye kambi mafunzoni na aliahidi kuwa kamwe hatowacha muziki,atashughulika na muziki pamoja na kazi yake mpya ya kulinda usalama.
Comments
Post a Comment