Posts

Showing posts from December, 2015

USHAIRI JASIRI: KUTANA NA GWIJI WA MASHAIRI MAMBOLEO.

Image
Mamboleo ni Swahili poet ama mshairi anayetumia lugha ya kiswahili.  Mshairi Mamboleo anafanya sanaa yake hapa nchini Kenya na amekuwa akifanya kazi na Mrisho Mpoto wa Bongo. Jamaa huyu kwa sasa ameachilia kazi mpya kwa jina Kumekucha .  Hii ni project ya kuhamasisha jamii kutokana na ubaya wa ukeketaji (Anti-Fgm). Kazi hii yake mpya inaelimisha sana jamii hasa wanafunzi na pia media. Ni njia mojawapo ya vile sanaa hutumika kufunza jamii za Kiafrika. Ni project amefanya na shirika la The guardian kutoka Uingereza. Unaweza kuitazama Video Yenyewe hapa ===> https://www.youtube.com/watch?v=rGcCm0lh6wU&feature=youtu.be  

MAGAZETI HAYAKUWACHWA NYUMA KWA TUKIO LA MSUMARI AWARDS!!!! ‪#‎PEOPLEDAILY‬

Image
It is the season of awards and artistes are excited about them as we are at Spice. However, over the weekend Mombasa based event organiser Eve Adhiambo popularly known as Queen Eve, held Nzumari Awards ceremony which ended on a sour note. According to popular Coast blog Pwani Usanii, Eve had invited TZ showbiz personality Wema Sepetu, but could not foot the bill for her guest (s) which ended up with one of the organisers being arrested and allegedly spending as a guest of the state. The event also witnessed a low turn out with majority of artistes snubbing the event claiming poor organisation and receiving bad treatment from the organisers. It took the aid on a popular Coast politician who came to the rescue and settling some of the bills. Courtesy of #PeopleDaily #ManuelNtoyai

BAADA YA MIAKA TISA AKOTHEE AAMUA KUIHAMA MOMBASA.

Image
Msanii wa kike mwenye hela zaidi Kenya ameamua kuaga maisha ya Uswazi.Akothee ambaye ameishi mjini Mombasa kwa miaka tisa amehamia jijini Nairobi. Msanii huyu aliye na vibao motomoto kama vile Shangerera alipachika ujumbe huu kwenye mtandao............ "“MOMBASA WAS REAL, 9 YEARS OF FUN MPAKA NIKATOKA NA VIKOMBE , A REAL EXAMPLE OF A NOMADIC WOMAN SEARCHING FOR A GREENER PASTURE!YAANI PASTORALIST. SEE YOU SOMEDAY ‪#‎ MOMBASA‬ I MISS YOU ALREADY ,I WILL CLIMB MOUNTAINS FOR MY CUBS ‪#‎ TEAMPOSITIVITY‬ #" Kwaheri Akothee.

WAAAAAHHHHH CHEKI HAPA!!!! MWAMAMITINDO REE THE BOSSETE AONYESHA MAZAGAZAGA YAKE!!!!!

Image
 Tazameni mwanadada Ree the Bossete ambaye vilevile ni model akionyesha mwili wake ulivyo mzuri......Huko mbele jaza wewe.

JOVIAL ATAMBULISHA VIDEO YAKE "CHANDA CHEMA" NDANI YA KISS TV.

Image
Baada ya mashabiki kusubiri sana kwa video yake ya CHANDA CHEMA, Juliet Jovial aliachia video yake kwa kishindo na cheki alivyovurumisha ndani ya kiss TV.

CELEBRITY PHOTO OF THE DAY

Image
Photocredit: #JBPhotography

KUTANA NA SAYARI ZEDDY AKITAMBULISHA NYIMBO MPYA.

Image
Ukisikia flavour za pwani basi hutokosa kumtaja Sayari Zeddy. Msanii huyu anayetamba kwa nyimbo yake DEDE ni mwenye kipaji na kuleta utamaduni wa pwani kwa fleva zake zilizokolea maudhui na sifa za pwani.Tuliwasiliana naye kupitia njia ya simu kuhusiana na wimbo wake mpya na Zeddy alikua na haya ya kutuambia....... "Hi ni ngoma yangu ya tisa. Nilifanya ngoma yangu ya kwanza Bigfoot Production ambayo yaitwa (Moyoni) Kisha nikafanya, Hayana siri, Nakutafuta, Heshima na 'Laiti ungejua' niliyoshirikishwa na dogo anaitwa GWIJI R. Zote hizo ni Tee Hits Production. Kisha nikarudi Bigfoot nikafanya 'Niko naye'. Ngoma ya saba ni 'Tosheka' ambayo niliifanyia Jungle masters Production. Kisha nikafanya 'Dede' ndani ya Green house kabla ya hii mpya sasa inayoitwa 'Kusudi'." Nyimbo kusudi aliyoifanyia Greenhouse production ndio anayoitambulisha kama kazu yake ya msimu huu wa sikukuu.

ANTONIO APIGA SAHIHI MTINDO MPYA WA MUZIKI "SWAHILI SOCA."

Image
Kila msanii kwa sasa yuko mbioni kufanya wimbo wake wa kufunga mwaka na hakuna anayetaka kuwachwa nyuma.Hivyo basi studio ya Newdawn records ikimtmbulisha msanii wake Antonio ; imeamua kufanya mapinduZi makali kimuziki.Billy Moyses,mmiliki na producer wa Newdawn records alidokeza ya kuwa msanii wake Antonio amekuja na mtindo mpya wa muziki kwa jina SWAHILI SOCA."Mtindo huu unachanganya fleva za muziki wa Trinidad na C aribean islands na fleva za hapa nyumbani pwani.Niliamua kufanya kazi na Antonio kwani ujuzi wake ni mkali wa kusonga na mdundo wa aina yoyote."Alieleza producer Billy.Nyimbo ya Antonio ni ya kupigiwa mfano mzuri kwani ipo style ya kipekee na ni ya kuchangamsha mashabiki.LEO NI LEO ni jina la wimbo na bila shaka wasanii lazima mtatoa kijasho chembamba kwa pigo hili la kufunga mwaka.

HIVI UTENGANO UPO KATI YA KIGOTO NA PRODUZA TK2??????

Image
Baada ya kutoa nyimbo NIKO NAWE akiwa kwenye kikosi cha muziki cha NUMBER ONE ACADEMIA,msanii aliyetamba kwa kibao AIRE ameonekana kumkwepa kwepa meneja wake TK2 ambaye vilevile ni Produza wa studio ya NUMBER ONE RECORDS. Fununu zinazojiri in kuwa Kigoto amepata mfadhili na meneja mpya jijini Nairobi. Kigoto amepachika picha tofauti tofauti mitandaoni akiwa studio kadha wa kadha hali iliyozua maswali kibao kwa mashabiki. Katika pitapita zetu mitandaoni tulipatana na picha ya Kigoto akiwa na Produza Jilly, producer Jilly ndiye aliyeandaa wimbo NAONA BADO wa SUDIBOY na AMILEENA.Vilevile producer huyu huwa studio inayojulikana kama Higher levels.

LIL SHAKES AWATOA KIJASHO WASANII WA JIJI KWENYE CHART YA MUZIKI.

Image
Amewachilia kibao kipya DOING IT cha hiphop hivi majuzi na akaamua kutolegeza kamba.Lil Shakes kutoka kikosi cha Coastside Militia amepanda kwenye charti za muziki wa Nairobi kwa kuwapa kivumbi wasanii wakubwa. Chart iliyokali zaidi Kenya ndani ya Tribe43 gazeti la PEOPLE DAILY inawakilisha wasanii Kenya nzima wanaofanya vyema.  Hongera kwake.

KUTANA NA THE REAL MAPETE BABUDEE.

Image
Ukizungumzia masonara na mapete kibao. Hapa basi mmefika, jamaa huyu ana mapete zaidi ya mnavyofikiria. Babu Dee Mapete ni msanii wa hapa pwani ambapo mama yake ni mtaita kutoka voi na babake ni mtanzania. Mapete ashawahi Fanya bonge la colabo na Ali kiba "kilio cha moyo" na vilevile akatoa kibao "gazeti la taifa' na kwa sasa ameachia ngoma yake mpya inayoitwa "Nairobi baridi." Video hiyo kwa sasa pwani tv iko number 1 kwa chat ya kumi kali.

MLISEMA SUSUMILA HAWEZI KUTOA KIBAO KIKALI PEKE YAKE......BASI ANA KITU KIPYA JINA "OYOO"

Image
Ndani ya studio mpya kabisa za Tempoz records chini ya producer Ammz; Susumila ameamua kufanya jambo ambalo mashabiki wengi hatukutarajia.Baada ya collabo mbili na Chikuzee,mara Kigoto,akaja Dazlah,Ikawa Busy-K,Ikaja King Kaka,Vivonce na Kaa la Moto,vilevile Bwenyenye....Mdosi wa Mishemishe music empire ameamua kudondosha kitu kipya peke yake.Wimbo wake mpya ni OYOO na Ameimba peke yake.Nashangaa waliomfunza kuimba watasemaje sasa.......OYOOO

LISTI YA WASANII CHIPUKIZI WAKALI WATAKAO TETEMESHA ZAIDI MWAKA UJAO.

5.YUNG-C 4.MAKINI 99 3.DULLY MELODY 2.DICE GANG 1.ZIKY WA ZIKY

Dowg Guerrilas album is officially out

Image
Tracklisting 1 Point of no return Ft Holy G prod by Ransom notes ( U.K ) mix & mastered by Sango ( Kenya ) 2 Pain & betrayal Ft Holy G prod by Sango 3 In my hood Ft Friskey Yr prod Q the beatboy ( U.S.A ) mix & mastered by Sango ( Kenya ) 4 Rules of engangment Ft Holy G prod by Jimus heamstead ( U.K ) mix & mastered by Sango ( Kenya ) 5 Rock with me Ft kocktail of Y.T.E & Tessy prod by Q the beatboy ( U.S.A ) mix & mastered by Sango ( Kenya ) 6 Blaze us the trail Ft Holy G prod by Sango 7 Sunshine Ft Chyna & Tonny Reezy prod by Stanslav ( Bulgaria ) mix cuts & mastered by Sango ( Kenya ) 8 First time Ft Holy G prod by Sango 9 Special Delivery Ft Chyna & Rued Eye prod by Vlad versus ( Romania ) mix & mastered by Sango ( Kenya )

KENYA YAPATA NOMINATION NNE KWENYE KORA MUSIC AWARDS.

Image
 Wanamuziki wa Nigeria wakiongoza kwenye list ya nomination za Kora awards mwaka huu. Kenya imejikwachulia nafasi nne. Victoria Kimani - Best Female Artist – East Africa  Sauti Sol - Best African Group Gloria Muliro - Best Female Artist – Spiritual Music 24 Elders- Best Group – Spiritual Music   Most Promising Male Artiste of Africa Reekado Banks (Nigeria) Chem Edine Boudra (Algeria) Numerica (Cameroon) Odyai (Madagascar) J Rio (Gabon) Yamoto Band (Tanzania) Most Promising Female Artiste of Africa Bading M – Stop Pretending (Gabon) Yemi Alade – Kissing ft. Marvin (Nigeria) Nelida Karr – Congosa (Equatorial Guinea) Daphe – Rastafari (Cameroon) Namina Kay – (South Africa) Kaaki (Ghana) Best Male Artist – West Africa Flavour (Nigeria) Serge Beynaud (Cote d’Ivoire) Bisa Kdei (Ghana) Nelson Freitas (Cape Verde) Atumpan (Ghana) Davido (Nigeria) Best Female Artist -West Africa Tiwa Savage (Nigeria) Adiouza (Senegal) Efya...

REDSAN AFANYA VIDEO SAFI NA SESAN.

Image
 Ana mazoea ya kukaa kimya kimuziki ila pindi awachiliapo muziki basi hutetemesha industry yote. Sio mwingine bali superstar ambaye wengine hudai mizizi yake imeanzia hapa pwani; Swabir Mohamed almaarufu Redsan. Jamaa huyo amefanya kazi safi kwa jina shoulder back na video imeandaliwa na Sedan. Sedan, ni videographer mkali zaidi Afrika na amefanya kazi na wasanii tajika. Redsan Sesan wameamua kuutambulisha mtindo wa dance mpya shoulder back kwa video ya kukata na shoka na bila shaka hawakulenga kando. Video yenyewe ilifanyiwa nchini Africa Kusini. 

WASANII WA HIPHOP WAKIMBILIA MSAADA KWA MZEE MWENYE BUSARA NA MAARIFA.

Image
 Baada ya Odinareh Bingwa kuonyesha picha yake akiwa na gwiji wa Bango Mzee Ngala mwenyewe,yaliyofuata ni Kuwa kuna collabo kati ya Odinareh na Mzee Ngala. Baada ya hapo, vilevile rapper Kaa la Moto aliachia picha yake na kudai kuwa pia yeye yupo katika pilkapilka za kuangusha kibao kipya akimshirikisha mzee Ngala. Yaonekana jamaa hawa wamekimbia kwa mzee kupata busara na maarifa.

NEW VIDEO ALERT: BILA WEWE BY DULA

Image

NEW VIDEO ALERT: CHANDA BY JOVIAL

Image

SWAHIB WA MASSELE -"POLE"

Image
Swahib wa Massele ni msanii tokea maeneo ya Kilifi. Msanii huyu ambaye vilevile ni produza wa Baseline records ameachia kibao chake kipya kwa jina “Pole”. Tuliwasiliana naye na alikuwa na haya ya kunena....... "Nilifaa kuachiliwa nyimbo yangu tarehe 30, mwezi wa November Mwaka huu. Lakini kwa sababu ya kutoelewana baina yangu na management, nyimbo ikachelewa kutoka. Hivyo basi, kwa kuwa nimekuwa msanii wa kujitegemea mwenyewe ninawachilia nyimbo hii tarehe 8/12/2015, ambayo itakuwa jumanne." Nyimbo hii imekomesha kimya chake kilichokuwa cha Zaidi ya nusu mwaka, na sahii Swahib amerudi na nguvu mpya."

LIL SHAKES AACHIA KIBAO CHAKE CHA PILI "I'M DOING IT"

Image
Aliamua kuja kimtindo tofauti wa hiphop na Lil Shakes halazi damu kamwe.Akiwa kwenye kundi la hiphop la Coastside Militia, Shakes ameachia kibao kipya toka studio za Kelele records kwa jina IM DOING IT. Akizungumzia bidii maradufu anayoweka kwenye muziki,msanii huyu amejibiidiisha kuweka sahihi yake kwenye map ya muziki wa pwani. Tusiseme pwani tu bali Kenya nzima kwa jumla. Download Lil Shake's new truck "DOING IT" on mdundo for free" http://mdundo.com/a/5897 "

HONGERA KWA WASANII FRENC MAKAPELA NA MUMMY-D KWA KUJALIWA KUPATA MTOTO.

Image
Waambiwa mapenzi matamu kwa wale wanaoyajua.Twachukua fursa hii kuwapa hongera wasanii French Makapela na Mummy-D kwa kujaliwa kupata mtoto wa kike kwa jina Natalia.Mwenyezi awajalie mama na baba Natalia.