WIMBO KIDEKIDE WA DAZLAH NA SUSUMILA WAZIDI KUKOSELEWA ZAIDI.
Huku mori ukipanda na youtube views zikizidi kwa wimbo KIDEKIDE wa Dazlah na Susumila,watu zaidi wanazidi kuubandika majina tofauti na kudai kuwa jamaa hao wawili walicopy.Mara ya kwanza waliambiwa wameigiza NAJUTA ya Yamoto band na kwa sasa mshika dau wa sanaa Manuel Ntoyai wa jarida la Tribe 43 na Spice Magazine za People Daily ametoanisha wimbo huo na kudai kuwa unafanana sana na wimbo wa Caro wa Wizkid. Japokuwa wimbo huo umekumbwa natetesi za kila aina,video yake iliyoandaliwa na Hamza Omar inazidi kupeta sana
Tazama video yenyewe hapa ujionee mwenyewe
Comments
Post a Comment