WANAHABARI MAGWIJI WA BARAKA FM WATEULIWA TENA....HII SASA KALI!!!


Watangazaji na wanahabari 5 kutoka Baraka FM kwa mara nyingine wameteuliwa kugombea tuzo za baraza la vyombo vya habari nchini –MCK, mwaka huu wa 2015.
Wanahabari hao wameteuliwa miongoni mwa wale bora zaidi nchini kutokana na uandishi na utangazaji wa habari, katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Wanahitajika kusafiri Nairobi May tarehe 3 ili kuhudhuria hafla ya kuwatuza, ikiandaliwa na Media Council of Kenya.
Baraza hilo limeandaa tuza hiyo kama njia ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari, mnamo May 4.
Kila mwaka Baraka FM imefaulu kuwa na kati ya wanahabari 3 na 5 katika tuzo mbali mbali za kitaifa na hata za kimataifa na hata kushinda nyingi, inapoadhimisha miaka 15 ya utangazaji bora.
Picha tuliyoweka hapo juu ya ukurasa huu inaonesha wanahabari wa Baraka FM wanaofanya kazi katika ofisi ya Mombasa.
Kuna wale walio katika ofisi ya Nairobi na wengine katika kaunti mbali mbali wanaotoa mchango mkubwa wa kufanikisha kazi na ushindi huo.
Je, wadhani kwa majina unaweza kuwataja wanahabari wa Baraka FM walioshinda tuzo kadhaa?
Tunakupa fursa hiyo ya kuwataja na pia unaweza kubashiri walioteuliwa mwaka huu kugombea tuzo za MCK mjini Nairobi.
‪#‎kwahisani_ya_barakaFM‬

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA