KUTANA NA MWANDISHI HODARI WA SANAA YA PWANI KWA MARA YA KWANZA!!!!

 INTERVIEW HII IMEFANYWA NA MWANDISHI TOFAUTI AKIMHOJI MWANDISHI GWIJI WA PWANI USANII

PWANI USANII:JITAMBULISHE KWA MAJINA YAKO KAMILI.
GODWIN: Jina langu kamili ni Godwin Wambua au kama wengi wanavyonifahamu 'habari za mombasani usanii'.
PU:WATU WENGI WANAKUFAHAMUA KUPITIA MITANDAO ILA HAWAJUI ULIANZA VIPI UANDISHI WA SANAA AU SHOWBIZ WRITING.TAFADHALI TUJUZE.....
GODWIN:Nilianza showbiz writing miaka mitatu iliyopita pale nilipoanzisha HABARI ZA MOMBASANI USANII.Baada ya kuona sanaa ya pwani imetengwa na magazeti,majarida na mitandao ndiposa nikajitwika jukumu la kuangazia Sanaa ya pwani pekee ili kuikuza na kusaidia vijana wenzangu wenye vipaji.Kitu watu hawafahamu ni Kuwa nimesomea blogging na creative writing papa hapa online na hata kupata cheti.
PU:NI NANI MMILIKI WA PWANI USANII?
GODWIN:Mwanzo kabisa Pwani Usanii ni blog inayoangazia Sanaa ya pwani kwa kuandika kuhusu wanamitindo,wanamuziki,waigizaji na washika dau wengine wa sanaa.Blog hii inamilikiwa na jamaa flani ambaye nitambana jina kwa sasa na Mimi mwenyewe ambapo kuna General manager na writer na mimi mwenyewe ni editor.
PU:BLOGGING NA SHOWBIZ WRITING INA MALIPO KWELI?
GODWIN:Blogging na showbiz writing inalipa ila inahitaji uvumilivu sana.Jijini Nairobi na Tanzania kampuni kubwa zinawekeza kwenye blogs na mitandao ya Sanaa tofauti. Blogs zinapata malipo kupitia adverts na promotion tenders wanazopata bila kusahau marketing vilevile.
PU:UNA MIAKA MINGAPI NA MAMBO YAPI UNAYOJIVUNIA KAMA MWANDISHI WA SANAA YA PWANI?
GODWIN:Nina umri wa miaka ishirini na ninachojivunia zaidi ni kushuhudia wasani ninaowaangazia na kuwatambulisha kwa jamii kuweza kufanikiwa.
PU:JE WASANII KAMA NANI UNAJIVUNIA KUWAANGAZIA NA SASA WANAFANYA VYEMA?
GODWIN:Wengi sana ila kuna wale niliotoka nao mwanzo nikianza HABARI ZA MOMBASANI USANII na sasa wamejulikana kama Kigoto, Shembwana Masauti, Shiney, Odinareh Bingwa, Ohms law,Dj Ivory na wengineo.Wengine hata niliwafanya watokee kwa gazeti kwa mara yao ya kwanza.
PU:NI CHANGAMOTO KAMA ZIPI MNAZOPITIA WAANDISHI?
GODWIN:Changamoto ni kibao tu ila kuna kampuni zapenda kutumia watu vibaya.Wawafanyia marketing poa kwa blog Kisha hawakulipi.Vilevile nishawahi pokea vitisho Mara nyingi kutoka kwa wasanii tofauti baada ya kuwaangazia na kutoboa mambo yao.Pia kuna baadhi ya washika dau wasio na shukurani kamwe hata ukawafanyia kazi nzuri kupiga simu wakwambie asante hawawezi.Mi natenda wema tu kwani wema bila shaka hauozi.
PU:UMEPIGA INTERVIEW NYINGI MNO KWENYE BLOG YAKO;LABDA NI INTERVIEW ZIPI ULIZOFURAHIA SANA?
GODWIN:Interview zote mi huzifurahia ila ya mtangazaji Mwinyi Kazungu wa KBC,Donde Samora,msanii Dazlah,Benso,Producer Baindo na muigizaji Juma Shibe ambaye yupo kwa kipindi Sumu cha K24 TV akiigiza kama Musa.
PU:JE NI NANI ANAYEKUMENTOR SANA?
GODWIN :Manuel Ntoyai yule acting editor wa spice magazine na Tribe 43 gazeti la PEOPLE DAILY.Kusema kweli amenisaidia sana.Producer Baindo wa Bigfoot music pia amenimentor sana.
PU:UNA MIPANGO GANI MIAKA IJAYO?
GODWIN:Nina kipawa cha kuongea manake mi ni mwalimu na hivyo basi nikichanganya uandishi na kuongea bila shaka nitakuwa mtangazaji bora sana. Kwa hivyo malengo yangu makuu ni kuwa mtangazaji wa redio ili niweze kuwasaidia wasanii zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA