MUNGU HAMTUPI MJA WAKE.....KIGOTO APATA USAIDIZI BAADA YA KUMWAGWA NA SUSUMILA.


Ni tabasamu chungu nzima usoni mwa Kigoto baada ya msanii mwenzake Amoury Beybie kujitolea kumsaidia. Amoury Beybie ambaye anaendelea na uandalizi wake wa video inayozidi takriban milioni mbili amekuja wazi na kumsifu msanii Kigoto Mmbonde na kusema kuwa Kigoto Mmbonde ana kipaji kikubwa ila wasanii wamemtenga.Amourey amejitolea kumlipia na kumsimamia Kigoto video yake ya wimbo NAPENDA VIZURI........
Amourey alinakili haya kwenye mtandao wake wa Facebook....

"Kigoto Mmbonde ni kati ya wasanii ninao wakubali sana kimziki, ni mtunzi hodari, msanii mnyenyekevu..hana kiburi na majivuno.. mwenye bidii, anafanya nyimbo zenye ubunifu wa hali ya juu na ujumbe wa kueleweka, kutokua na sapot kwake kumenitia unyonge sana. Japo baadhi ya wasanii wamemtenga, na ameandika hits nyingi zilizofanya vyema, kwani siko tayari kuona kipaji na mtunzi bora aje akate tamaa baadae, ndio maana mimi binafsi kama ‪#‎ARTIST_001‬ nitamsimamia VIDEO YA nyimbo yake mpya ‪#‎napenda_vizuri‬ iliotengenezwa na PRODUCER NA MANAGER WAKE Tk Mbili .. najua ni sapryz kwako mdogo wangu ila mikakati yote nimetayarisha tayary na DIRECTOR / PRODUCER na MANAGER WANGU Guy G Vid Produza......"

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA