MSANII YAGAYAGA ANAYEISHI BAHARINI MAMANGINA.
Msanii huyu kutoka hapa mkoani pwani kwa
majina Yaga Yaga ni jamaa ambaye anaishi
maisha ya kubahatisha ila yee hushukuru
mwenyezi Mungu kila kuchao kwa kumpa uhai.
Yaga Yaga hana makao maalumu na yeye hulala
kando ya baharini kule mama Ngina manake huko
ndio nyumbani aanakojua. Kando na hayo yote
msanii huyu hujibidiisha kwa kufanya vibarua
vidogo vidogo hapa mjini na kuchanga hela za
kurekodi studio. Ameweza kwa sasa kurekodi
nyimbo mbili Kule SQ Records na akafanya video
moja. Yeye husema hawezi kufa moyo kwasababu
ya maisha yake ya upweke manake anaamini ipo
siku atakuja faulu kupitia kwa kipaji chake cha
usanii...
$hukrani kwa #backstreet entertainment.Yagayaga twakutakia kila la kheri.
Comments
Post a Comment