FISHERMAN 'NDOTO' YA GRANDPA KUDIDIMIA.
Miaka miwili iliyopita msanii Fisherman anayetokea Mtongwe na mzaliwa wa papa hapa Pwani alisajiliwa na studio kubwa Nairobi kwa jina Grandpa.Kilichofuata kwa star huyu wa Dancehall ni kufanyishwa collabo mbili ambazo alifanywa kushirikishwa.Fisherman ambaye ndugu yake ni Noir Mwamba anayemiliki studio ya Mwamba records aliacha kurekodi muziki kwa muda huku mashabiki wakisubiria kazi sake kutoka Grandpa records. Cha kushangaza ni kuwa msanii wetu wa hapa Pwani Fisherman hajarekodi wimbo wowote hadi sasa. Kuongezea msumari moto kwenye kidonda Fisherman ametemwa kwenye wimbo wa Grandpa FIMBO YA TATU 'DAWA YA MOTO'.Swali ni je Fisherman alitemwa au Grandpa wamemchoka??? La mwisho kabisa,mashabiki wana hamu ya kumsikia Fisherman tena.Je atawachilia lini kazi mpya????
Comments
Post a Comment