SANAA YA PWANI KUPEWA NAFASI YA KWANZA KWENYE GAZETI LA PEOPLE DAILY JUMAPILI.


 Hayawi hayawi yashakuwa. Baada ya wasanii wa pwani kulalamika kwa miaka mingi kuwa sanaa yao haipewi nafasi na vyombo vya habari hasa vya Nairobi,gazeti People Daily lilikuja wazi na kuwapa nafasi ya mbele wasanii wa pwani na sanaa ya pwani kwa jumla. People Daily ambalo huwa na jarida la burudani{entertainment magazine} kwa jina SPICE limeahidi kuangazia sanaa ya pwani kwa undani zaidi na kuwapa kipao mbele wasanii wanaovuma na wanaochipuka kwa jumla. 
People Daily limewapa wasanii wa pwani ukurasa mmoja kila jumapili utakaojazwa habari za sanaa ya pwani pekee. Tulipowasiliana na Acting Editor wa jarida la Spice na mwandishi wa mashuhuri wa burudani,Manuel Ntoyai alitudokezea haya...."Tumeamua kuiangazia sanaa ya pwani kwa undani katika gazeti letu la People Daily ili lipate kujulikana zaidi. Sio wasanii wa muziki pekee tutakao chapisha habari zao bali actors, dj's, promoters yaani sanaa yote kwa jumla. Tayari Jumapili iliyopita tumechapisha habari kwa kuangazia maswala kadha wa kadha yalikuwa yameleta tetesi Pwani." Vilevile kwetu naona ni jambo la busara wanalolifanya People Daily kwa kuipa nafasi sanaa ya pwani kukua Kenya nzima na kujulikana Afrika mashariki.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA