Kutana na Shephard wa Shemakinz.
TUELEZE JINSI ULIVYOJIUNGA NA MUZIKI.
Mimi nilianza muziki nikiwa na mwenzangu akiwa ni Jay makini tulipo jitahidi sana nakuunda kikundi kinachoitwa Shemakinz.
KUNDI LENU LA SHEMAKINZ LILIFANYA VIPI KIMUZIKI?
Baada ya miaka kadhaa tulijulikana sana na kutia fora pwani nzima.Naweza sema tulifanya vizuri kimuziki.
TUTAJIE BAADHI YA VIBAO VYENU VILIVYOVUMA:
Vibao vilivyo tutambulisha ni 1.Madam jessica 2. Mahabuba na vinginevyo.
JE KUNDI LENU LIPO HADI SASA?
Hapana lilisambaratika na kugawanyika na nikabaki peke yangu.
KISHA MUZIKI WAKO BINAFSI UKACHUKUA MKONDO UPI?
Baada ya kunyamaza mwaka mzima nilirudi tena mwaka jana nikiwa na hasira sana kwenye huu ulingo wa muziki nilifika mwamba recordz nakushirikiana na Noor mwamba kufanya kazi. MWAMBA RECORDZ MKAFANYA MRADI UPI WA MUZIKI?
Tulianza na kutoa vibao viwili vikali sana .Vikiwa ni mtoto mzuka nikiwa na Ken s na pia mdogo mdogo.
JE UNA LIPI LA KUWAAMBIA MASHABIKI WA MUZIKI,HASA WA PWANI?
Nashukuru sana kwa mashabiki kwa kunipokea tena namshkuru Mungu kwa kunifikisha hapa.
Comments
Post a Comment