MOMBASA HOTTEST RAPPERS. TO WATCH OUT FOR


 1.KAA LA MOTO KIUMBE aka Mohamed Ali
 MTINDO:Hardcore Rap 
SKILL:Ana freestyle na Punchlines kali. Alianza katika mashindano ya Dont Break the Beat freestyle competition na akafuzu kufika Nairobi. Ni mmoja ya wakali wa Mombasa hip-hop. He is known to call himself the King of freestyle and hosted the hip-hop Thursday on pwani fm alongside Gates Mgenge. Amekua na tetesi za kuibukia bongo na kuwa Mkenya anayeiga flow ya rapper Stamina. Mwaka uliopita alituzwa kwenye Coast Music Awards. Kaa anayetoka mitaa ya Bersheba aliidai kwenye redio kua ana mzungu na alihamia mtwapa anakoishi naye. 
He currently has a song with singer Luv Mamz that is doing good on radio and a video for his song mia kwa mia alongside Jaystar. 

2.ODINAREH BINGWA aka Mr Controversial 
MTINDO:Commercial/­Revolutionary Rapper 
SKILL: Mtunzi Hodari na anafoka mchanganyo wa kizungu,Sheng na Kiswahili. Hubadili mtiririko wake sana kwenye beat. Msanii huyu wa Kelele Records anaye manejiwa na Bee Entertainment ya Producer mkali wa hiphop Teknixx, alianza mziki mwaka uliopita pia kwenye Nokia Dont Break the Beat Freestyle Competition na akawa kati ya kuwakilisha Pwani Nairobi. Huu ukiwa mwaka wake wa pili ulingoni Odinareh amekua msanii wa kutajika na kukubalika na wengi kutokana na mziki wake na pia misimamo yake kwenye showbiz industry ya Mombasa. 
Msanii huyu aliingia ulingoni na ngoma ya Ghetto dreaming iliyofanyiwa video na Cream Vision Nairobi na kuachiwa rasmi kwenye kipindi cha Straight up KTN, baadaye alibwaga Money Lover iliyofanya vyema pwani, kisha baadaye akarudi na collabo kubwa akiwa amemshirikisha Ohms Law Montana kwa jina MAKE A NAME, traki hii ilikua hiphop ya kwanza kushikilia nambari moja kwenye chati na Video yake kufwatia. Odinareh hufunguka bila uoga na usemi wake wa kizushi umekuwa wa kuskika na kuheshimika na wengi kwani atakumbukwa kwa kusababisha saba saba Mombasa kwenye mitandao na maredio alipozungumzia kuhusu ma dj wa redio kucheza miziki ya nje sana kuliko ya pwani. Kwa sasa anatamba na tracki ya PAPER ambayo iko nambari 5 kwenye chati za pwani. 

3.OHMS LAW MONTANA aka Alcapoem 
MTINDO:Hardcore Rapper 
SKILL: Mshairi anajua kucheza na maneno na punchline. He has been in the game since last year where he performed at the Campus Tour ambapo alitambua kipaji chake na kurekodi single yake ya kwanza streetstar. Ohms ambaye ni mwanafunzi wa Mombasa Poly baadaye aliachia Gavaa Yangu pamoja na Drulix MTP ngoma iliyokua yenye kukashifu serikali. 
Montana ambaye alihudhuria Show ya Hiphop Thursday Pwani Fm na kukuza kipaji chake kupitia mitindo huru alirudi baada ya kimya kwenye mziki na collabo ya MAKE A NAME iliyorekodiwa Kelele Records aliyoshirikishwa na mwenzake Odinareh Bingwa. Kwa sasa anatamba kwa ujio wake mpya 'Poleni' uliofanywa na Teknix. Ujio ambao umepokelewa vyema na ako katika mpango wa kuandaa video baada ya mwezi mtukufu wa ramadhan. Ohms Law ambaye ako kwa mazungumzo ya mkataba wa kusainiwa na Studio ya StantMastaz Entertainment amedai kua ana mengi mazuri mwaka huu. 

4.HUSTLAJAY 
MTINDO:Revolutionary­/Hardcore Rapper 
SKILL:Anaelewa siasa na hufoka hiphop siasa. Msanii huyu aliyevuma kwa video ya Continental scars iliyofanywa na Sand Stone Studios ako chini ya Tedd Josiah na kwa sasa anapanga kuachia video nyingine. Hustla ni msanii ambaye amekua kwenye ulingo tangu enzi za ufuoni records hadi kwa sasa ako kwenye Tedd Josiah. Msanii huyo ambaye ana traki kadhaa kama uhuru afrika amekita sana kwenye hardcore hip-hop.

5. DIZASTA 
 MTINDO:Hardcore Rap 
SKILL:Punchline na Wordplay Ni msanii aliyebwaga mixtape yake ya BLACK CITY mwaka huu kutoka studio ya Stantmastaz iliyo washirikisha ma rapper kama Montana, Frankwest na Drulixx. Amekua akitokea kwenye show ya Gates Mgenge freestyle Thursday pwani fm na alitamba na wimbo wake wa Ile mbaya.  

6.RISTO BSB 
MTINDO:Street Hiphop 
SKILL:Ana uwezo wa kushikilia pumzi mda akitema vina. Ni msanii anayeibukia magongo na anayefanikisha kipindi cha HipHop Thursday katika pwani fm.Ni mfwasi wa kundi la BoomSalaBar lillilo na wana hiphop kadhaa. 

7.FRANKWEST MSHAMBA 
MTINDO:Hardcore Rapper 
SKILL:Mashairi mazito. Ni mmoja ya wasanii walioanzia kwenye Nokia Dont Break the Beat freestyle battle,Frank ni member wa kundi la Washamba Wenza linalo husisha Smallz Lethal,Ananda na Kev Mamba mshamba. Akiwa mshirika wa kipekee kutoka Mombasa wenzake wakiwa Nairobi. Alikua katika mixtape ya Dizasta na kwa sasa anafanya mixtape yake itakayotoka mwezi wa nane. 

8.Vedette 
MTINDO:Urban Rap 
SKILL:Anafoka kifaransa na kiingereza. Ni msanii anayejulikana kwa kuskuma harakati za hip-hop kwenye vilabu na kufanya mashow kupitia lebo yake ya Ultimate Hiphop.Expe­rience. Kwa sasa anatamba na ujio wake mpya hip-hop city unaoongelea mji wa Mombasa. 

9.Bancho Bwoy 
MTINDO:Bounce Rap
 SKILL:Mkali wa freestyle anaibukia maeneo ya ukunda na ni msanii aliye na mizizi ya bongo ambaye amekimya sana baada ya traki yake unaringa kufanya vyema na video kuachiwa.Ni msanii aliyewahi kumchafua Kaa la moto kwenye freestyle za hiphop thursday.
Amekimya mno siku hizi. 

10. ACHICHO DIMPALI 
MTINDO:Fast Flow Rap
SKILL:Anaflow fasta. Huyu ndio mc wa kipekee wa kike na anakuja kwa kasi mno. Amewaridhisha wengi kwenye show ya Gates Mgenge anavyofoka mistari. Duru za kuaminika zasema kua ako katika mazungumzo na stantmastaz kusaini mkataba. 

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA