RAPDEM AWACHA MUZIKI NA KUJIUNGA NA COMEDY!!!
Huku nyanja za muziki wa pwani ya Kenya zikizidi kupamba moto, wengi wa wasanii wanaonekana kufuata mkondo na kujaribu bahati yao mahali kwingine. C'zars alikuja akapotea, Bablee wa Tabasamu recordz akakimbia, Sketcher wa Rude boys akajiuzulu kimuziki, Shamaniz na Shiney wakataka kuwacha muziki ila wakarudi kwa kishindo. Raundi hii, dada mkali wa maflavour ya kufoka, Rapdem alitangaza rasmi azimio lake la kujiunga na tasnia ya comedy.
Rapdem aliyevuma kwa kibao Jitambulishe alinakili kwenye ukurasa wake wa facebook kuwa angependa sana kujiunga na ucheshi na kuupiga teke muziki. Msanii huyu alisema hivi, tukinukuu kutoka kwenye ukurasa wake wa fb
"I'm official Minusing myself from Music industry and adding fully in Comedy ...after doubting myself too, had to do my own investigation 1001 people say am little funny but if i decide to grow, then am a big thing, now i wanna grow. Leave alone my classmates, people who leave around me, my family they serve as major witness, anyway i don't need to prove this, i wanna wish my fellow artistes al the best , and thanks to everybody who was behind me since 2011 when i started my music career....." Twamtakia kila la kheri Rapdem.
Comments
Post a Comment