DOGO RICHIE KUSAJILIWA UGANDA NA KUFANYA COLLABO NA DAVIDO NA NAMELESS:
Huku akiwa bado anasheherekea kuvuma kwa video yake Sijasahau, msanii Dogo Richie leo hii amepasua mbarika. Dogo aliyekuwa anahojiwa kwenye kipindi cha Homegrown KBC alitangaza hadharani kuwa amesajiliwa na studio nchini Uganda ambayo pia ipo USA.
Vilevile,msanii huyo alisema kuwa video yake itakayofuata itaandaliwa Afrika kusini kwa kiwango cha shilingi zaidi ya milioni moja. Kando na hayo, Richy ri aliongezea kuwa yupo katika matayarisho ya kufanya collabo na Nameless kabla hajarudi pwani na baadaye amshirikishe msanii Davido wa Nigeria kwa wimbo utakao tawala chati za muziki wa Afrika.
Comments
Post a Comment