Posts

MSANII WA INJILI AELEZA KUHUSU SHIDA ALIZOPITIA NDIPOSA KUTOA WIMBO MTETEZI.

Image
MSANII WA INJILI AELEZA KUHUSU SHIDA ALIZOPITIA NDIPOSA KUTOA WIMBO MTETEZI. Mula Sanz ni msanii anayefanya muziki wa injili na ameamua kivyovyote vile lazima aeneze neno la Mungu kupitia kipaji chake. Wimbo 'mtetezi' ndio unaopiga muhuri album yake ndogo ya nyimbo tano. Albamu hii ambayo ni yake ya kwanza inaitwa YULEYULE na Mula Sanz ameirekodi kwa studio yake mwenyewe. Msanii huyu alitueleza kuhusiana na wimbo wake mtetezi na alikuwa na haya ya kunena..... "Mtetezi is a gospel song describing how jesus is faithful to us.We always pass through difficult situations na binadamu wanaweza kututema msimu wa shida.Unaweza tafuta msaada kwa watu ila wote wanaweza kukutema.Only God helps us in times of need.Mtetezi is an inspirational song to all who believe in God." Vilevile msanii huyu atawachia wimbo wake wa mwisho kwenye albumu hiyo mwezi ujao. http://mdundo.com/a/27490

VIDEO YA NYIMBO YETU 'KAA RADA' TUTAIFANYA NCHINI IRELAND-JEY KITOLE AFUNGUKA.

Image
Mwanasarakasi ambaye Vilevile ni msanii aliyekita mizizi kwa miondoko ya ufokaji na hiphop,Jey Kitole amefunguka na kumwaga mtama kwenye kuku wengi. Msanii huyu alishirikiana na wasanii wenza wa hiphop na kuachia dongo kali kwa jina KAA RADA. Wimbo huu,kama alivyotueleza Jey Kitole utakuwa mmoja wa kipekee kwani video yake itaandaliwa jijini Dublin nchini Ireland. "Tutatumia pesa za kisawasawa kuandaa video hii na bila shaka itakuwa ya kimataifa." Jey alieleza. Kando na kuandaa video hiyo,Jey yupo katika pilkapilka za kuachia rasmi wimbo wake UKINIPENDA aliomshirikisha Dazlah.

MEET JACKTONAIR AND KASH-FAR REPRESENTING THE HIPHOP CREW MASELA FULANI.

Image
Masela Fulani is a hiphop crew started by two individuals Jacktonair and Kash-far. This hiphop clique has members all over Coastal streets; from Mishomoroni,Kisauni to Kaloleni. Singing,rapping,composing and educating the youth,Music has been their passion since high school.The two rappers started doing serious music early this year keenly following the footsteps of Ukoo Flani and Makeke Family. We asked Jacktonair and Kash-far some questions and here they are ------ >>> PWANI USANII: WHY DO YOU DO THIS KIND OF MUSIC. JACKTONAIR:Most of the youths nowdays listen to hiphop music so our aim is to inspire youths,motivate and encourage them to deviate from committing crimes, indulging into drugs,and loosing focus. KASH-FAR:To us Hiphop is life, you create it,commit to it with hopes of performing it and achieve it.So we educate our fellow youths through our music to gain for better hopes. PWANI USANII:TELL US ABOUT THE MUSIC PROJECTS YOU'VE DONE SO FAR. JACKTONAIR...

STUDIO ZA ISLANDLOVE RECORDS KUMSAJILI DULLY MELODY??

Image
STUDIO ZA ISLANDLOVE RECORDS KUMSAJILI DULLY MELODY?? Msanii Dully Melody aliyetamba kwa vibao kama Hongera,Source na Yagayaga yaonekana kawapendeza wengi na kuwavutia mameneja wengi mno. Baada ya kupiga show Lamu akiwa pamoja na Chikuzee,meneja wa ISLANDLOVE records ambayo ni studio kali zaidi Lamu alifurahishwa sana na kazi za msanii huyu na akampa fursa ya kuwa msanii wa studio yake. Hivi majuzi studio hii imepata ufanisi mkubwa na wasanii wake kupata mpenyo kwenye ulingo wa sanaa ya pwani. Wasanii waliosajiliwa kwenye studio hiyo ni Produza msanii Doni na mwenziwe Man Azzer na tayari washatoa vibao motomoto na video ya kukata na shoka. Tulipowasilian na Dully Melody alisema kuwa jambo hili bado lipo "pending" na kuna mambo mengi ya kufikiria na kuongea kabla mkataba wowote.

TEAM RIYAL TALENTS KUACHIA KIBAO CHAO SWEETY!!

Image
Kikosi kinachowakilisa Kenya pande za Uarabuni,Team Riyal Talent kipo tayari kudondosha mzigo dakika yoyote kuanzia saa hii. Wimbo huo kwa jina "sweety" umetayarishwa na studio ya Bigfoot music chini ya Produza Baindo na studio za Record in Studios Qatar. Mwanzilishi wa Team Riyal Talent,MNS alidokeza ya kuwa ni bidii na kuja kufanya kazi pamoja kwa nchi zote mbili,Qatar na Kenya ndiposa kazi hii ikafanyika. Wimbo sweety ni ushirikiano wa wasanii Prince, Mejakali na Mns.

Diamond Platnumz kuzindua marashi ya CHIBU

Image
Mkali wa bongoflava Diamond Platnumz ameingia kwenye biashara ya vipodozi na kupitia Facebook yake, alionyesha sample ya kwanza ya CHIBU Perfume ambayo anatarajia kuzindua hivi usoni. About to make another History @ChibuPerfume #TheScentYouDeserve soon will be in your favorite store!

DULA WETU AZITUPILIA MBALI TUZO ZA PWANI CELEBRITY AWARDS.

Image
Msanii wa dancehall,Dula the African songbird amegadhabishwa sana na tuzo zinazoendelea za pwani celebrity awards. LISTEN TO PWANI USANII ONLINE RADIO HERE >>> https://www.spreaker.com/user/9366849/vichapo-motomoto_1 Dula aliyekuwa mstari wa mbele kujipigia debe kwenye kinyang'anyiro cha tuzo hizo alikuwa Mwingi wa hasira na kushtumu jinsi upigaji kura unavyoeendeshwa. Msanii huyu aliye na vibao kama singing the same songs,Babylon na huzuni alijitoa kwenye tuzo hizi zitakazofanyika Jumamosi hii katika mkahawa wa English Point Marina.