PATA KUMFAHAMU MSANII PERMIUS.ONE ON ONE INTERVIEW.
PATA KUMFAHAMU MSANII PERMIUS.ONE ON ONE INTERVIEW.
PWANI USANII JE WANAKUITA NANI JINA LA KISANII?
PERMIUS: Jina la usanii naitwa Permius.
PWANI USANII:MUZIKI ULIANZA LINI?
PERMIUS:Muziki nilianza mwaka wa 2015 hapo ndipo nilianza kuenda studio.
PWANI USANII:ENHEE TUELEZE ZAIDI: Nilipatana na kijana mwenzangu mwimbaji kwa jina Burning ice ambaye vilevile ni Produza na akaamua kunikuza kimuziki na kunipeleka kwa studio yake kwa jina Trace records iliyopo Malindi.
PWANI USANII:LABDA KAZI ZA KIMUZIKI ULIZOFANYA TRACE RECORDS NI KAMA ZIPI?
PERMIUS:Kazi nilizofanikiwa kufanya Trace Records ni nyimbo ya kwanza kwa jina- sitaki tena ambayo inapatikana mdundo .Mwaka jana,2016 nikafanya kazi mpya kwa jina -leo na kesho ambayo mashabiki walipenda na kunipa morali.
PWANI USANII:KWA SASA LABDA UNA KAZI MPYA YOYOTE?
PERMIUS:Yeah,kuna kazi mpya nimefanya nikimshirikisha Burning ice na nimepanga kuwashtua mashabiki.Kazi hiyo nitakua naiwachilia karibuni....
Comments
Post a Comment