DONDE KUTOKA KWA UTANGAZAJI HADI KWA UTETEZI WA WANANCHI.
Alianza utangazaji zamani na wengi wetu twamfahamu kutoka enzi akiwa Baraka FM. Donde Samora,mtangazaji mcheshi anayependwa na wengi kwa weledi wake wa kuongea na kuweka mambo wazi aliamua kujiunga na siasa na wengi walijiuliza maswali yaso majibu....
Donde,ambaye alitetea sana vipaji vya wasanii hasa wanaoibuka aliamua kuingia siasani sio kwa minajili ya manufaa yake mwenyewe bali kuwahudumia wananchi wa eneo la Junda na kuwapa mkono vijana wa Pwani wazidi kukua kimaisha.
Katika mikutano ya siasa,jamaa huyu huwa sio mwingi wa maneno vile ila katika project z kusaidia jamii hapo ndipo utakapo muona mstari wa mbele akisaidia kwa hali na Mali.
Ama kweli sio kwa utangazaji pekee ambapo Donde amebarikiwa bali hata kutetea haki na kuhimiza maendeleo ya jamii ndiposa wanaJunda wamempa jina MTETEZI WA WANYONGE!
Comments
Post a Comment