Posts

Showing posts from August, 2016

KUTANA NA ACTRESS MASHUHURI CARO KUTOKA MALINDI.

Image
Caro ni actress sifika m mjini malindi na pwani kwa jumla. Mwanadada huyu hutumia kipaji chake kujimudu na uigazi ndio humpa mkaye wake wa kila siku. Caro ameigiza kwenye filamu kama vile Uzito Wa hisia,The meeting na nyingine nyingi.

SAUTI MPYA MJINI; PATA KUMFAHAMU MSANII LA TWKUL

Image
Alianza muziki mwaka huu na kamwe ameamua kutorudi nyuma.Msanii La Twkul amejitosa kwenye maji ya kina kirefu na ana imani kuwa nyota yake itan'gaa. La Twkul aliandaa nyimbo yake ya kwanza 'chekecha' akiwa katika kundi la Wapole Band. Baada ya kundi lake la Wapole Band kusambaratika,LaTwkul aliamua kuanza kufanya muziki kivyake kama solo artist. Kwa sasa kibao chake kipya kinatoka tarehe nne mwezi huu. Kibao chenyewe 'niokote' kimeandaliwa Asali records chini ya produza B.i. La Twkul alituelezea kuwa lengo lake kuu kwenye muziki ni kuwa Msanii wa kipekee atakaye kuwa kielelezo kwa jamii na kuigwa vizazi vijavyo.

MLIPUKO WA MABINTI!!! HII ITAKUWA KALI SANA!

Image
Produza Amz Jadidi almaarufu tone la maji alifunganya virago kutoka kambi ya SQ records na kuanzisha himaya yake kwa jina TEMPOZ.Kwa kipindi kifupi,Tempoz imefanya juhudi kuu na imeonekana kutoa hits nyingi zinazotikisa pwani na Kenya kiujumla. Kwa sasa Produza Amz amewaleta pamoja wasanii wa kike ili kufanya kazi pamoja. Wasanii hao wakiwemo Mamalao,CML,Pendo,Tatu,Jovial na Vivonve wamejitwika vazi la Tempoz na tayari ujio mpya upo njiani. Kwenye kumbukumbu zetu,pwani imekua na mlegezo Fulani kuenua mabinti kwenye sanaa. Wasanii wa kike ni wa kuhesabu tu ba hivyo basi,Amz amejaribu kuliziba pengo hili na kutaka kutuonyesha kuwa wasanii wa kike wapo na wanaweza.

MWANADADA MNIGERIA ATAKAYESISIMUA VIDEO YA FRANKIE DEE!!!!

Image
Huku kibao chake kipya cha Madda dem kikizidi kupata makali,staa wa miondoko ya dancehall Frankie Dee yasemekana ana mipango bambam ya video. Frankie Dee ambaye vilevile ni mmoja wa watumbuizaji wa tamasha la Msanii Romain Virgo,kupitia kurasa za Dancehall Msa Family and Friends ilisomeka kuwa jamaa huyu atatoa video na vide vixen mashuhuri anayetokea Nigeria. Video hiyo itakayoandaliwa na video director X-Antonio amepigiwa debe kuwa itakuwa moja ya kipekee na itakayoleta mageuzi kwenye sanaa ya Afrika Mashariki.Japo haikuwekwa wazi wimbo upi utakao fanyiwa video hiyo,tuna imani kuwa Frankie Dee atawasha moto kwenye ulingo wa muziki wa Afrika Mashariki.

DISMAIL LYRICS by KITOLE KENDA

Image
INTRO: Talk YOW, ONDIKO ITS YOUR MAN KITOLE KENDA, GOT SOMETHING FOR YOU. YOU NEVER MISS THE WATER TILL THE WELL RUNS DRY,NOW SHES GONE DISMAIL,OOOOH HEEYp VERSE 1 YOU KNOW LOVE, IS A BEAUTIFUL THING, A HAPPY FEELING LOVING SOMEONE COULD BE, LOVE IS A BEAUTIFUL THING, A HAPPY FEELING LOVING SOMEONE COULD BE, BUT WHEN TEMPTATION,TAKES OVER YOUR MIIND , NOW SHE GOT IT ALL IN THE VIDEOO SHE DOESNT WANNA SEE ME NO MORE, BE WITH ME NO,BE MA SENORITA LOVING ME SLOW SEE ME NO MORE, BE WITH ME NO,BE MA MAMACITA SHE WANNA GOO GOO GOOOO, SHE WANNA GO GO, SHE WANNA GO GO AWAY SHE WANNA GO GO, SHE WANNA GO GO AWAY CHORUS SO SHE SEND A.. DISMAIL DISAMAIL DISMAIL, SHE DOESNT WANNA SEE ME LATER, SO SHE SENDING ME A REGRET LETTER, AAAAH SO SHE SEND A, DISMAIL DISAMAIL DISMAIL, SHE DOESNT WANNA LOOSE CONTROL, SO SHE DOESNT WANNA SEE ME NO MORE, she doesnt wanna na na, VERSE 2 DAKIKA MOJA NAWE, nawe mi nataka TURUDIANE NAWE,we mi nataka YALIYOKUWA YAWE,yawe mi...

MSANII AKOTHEE AZIRAI BAADA YA HABARI KUHUSIANA UJA UZITO WAKE!!!

Image
MSANII AKOTHEE AZIRAI BAADA YA HABARI KUHUSIANA UJA UZITO WAKE!!! Msanii mashuhuri wa hapa Kenya,Akothee alianguka na kuzirai kwenye kituo cha reli Geneva, nchini Kenyan singer Akothee Switzerland,Jumanne Agosti 30,ambayo ni Leo. Akothee alikimbizwa hospitalini haraka iwezekanavyo kama alivyoeleza ,Nelson,meneja wake. Kulingana na habari alizozitoa Nelson ni kuwa Akothee alitarajia kupata mapacha na madaktari walisema kuwa hali ya pacha mmoja haipo sawaa. "Akothee was expecting twins, but doctors at a Geneva hospital say they can’t feel the second unborn baby’s heartbeat." Kwa sasa msanii huyo wa GIVE IT TO ME yupo hospitali na anaendelea na matibabu. Team pwani usanii,Twamtakia hali njema na apone haraka.

MSANII WA PWANI DULA THE AFRICAN SONGBIRD KUTUMBUIZA JUKWAA MOJA NA ROMAIN VIRGO.

Image
Tarehe 24 mwezi wa September (weka alama kwenye kalenda) kutaporomoshwa bonge moja la show ya kukata na shoka.Yard Beat entertainment waandalizi wa tamasha litakalowaleta wasanii kadha wa kadha wa hapa pwani,wakiwemo Dula the African Songbird, Frankie Dee,Fidempa na wengineo wamelileta tamasha hizo kwenye jumba la kimataifa la KICC. Hivi majuzi,ufanisi kwenye anga za muziki wa reggae na dancehall pwani umeanza kuonekana na wasanii wamejizatiti kuenuka vilivyo. Dula,ambaye Vilevile ni Produza shupavu ameachia vibao kadha wa kadha vya kusisimua kama vile singing the same songs,Loose control na Tiara.

BREAKING NEWS!!PRODUZA MORBIZ APIGWA RISASI.

Image
Produza mashuhuri wa pwani Morbiz wa studio ya Thundersound iliyopo Maeneo ya Likoni alimiminwa risasi ya kichwa na kufariki papo hapo. Tukio hili la kuigiza kwenye video ya Jaffarizoh lilifanyika kuonyesha mifano huru ya jinsi utu unavyokosekana kwa ajili ya pesa. Morbiz alikua anaigiza kama mnunuzi wa shamba pale alipomiminwa risasi ya kichwa. Jaffarizoh,msanii mwenye video hiyo iliyoandaliwa na Bullet wa Stunner Pictures ameonekana akifanya msukumo wa kila aina ili kuipa msukumo video hiyo ya Pesa. Pata kuitazama video yenyewe kwenye mtandao wa youtube jinsi Produza Morbiz alivyoigiza -- >>>>>  http://www.youtube.com/watch?v=CuzLCyRWDAchttps://youtu.be/CuzLCyRWDAc

USISHINDANE NA MTU,NYOTA NDOGO ATOA MAWAIDHA.

Image
Je ushaitazama video ya Nyota Ndogo,Subira yangu? Hivi je Nyota alikuwa na ujumbe gani kwa mashabiki zake...? Pata kuitazama hapa - >>>>>https://youtu.be/nTwae7mxezA

SiS P AGADHABISHWA!!!!! KISA NINI???......SOMA HAPA!!!

Image
Mwanadada wa bonge la bwana,Sis-P ameguswa pasipostahili. Binti huyu aliyechini ya A Million records ni mwenye uchungu na wanahabari wa Kenya. Sis-P kupitia account yake ya Facebook alizisuta media house za Kenya kwa kutoonyesha uzalendo. Haya yamejiri pale,mwanamuziki Diambond Platinums kulakiwa bega kwa bega na wanahabari furifuri kwenye uwanja wa ndege ilhali wanariadha wa Kenya hawakupokelewa na yeyote. Sis-P anayevuma kwa video yake ya uchoyo aliyomshirikisha Dazlah alikua mwingi wa maneno na kushtumu Wakenya kutokuwa wazalendo.Cheki screenshot ya akaunti yake ya Facebook.

PRODUZA KHALID:"Nitajie msanii yoyote aliye hit nikwambie presenter gani anamu manage na kina nani wamembeba..."

Image
Tukinukuu moja kwa moja kutoka kwa account ya Khalid Produza wa A Million records akizungumzia kuhusiana na branding...... #Branding Neno 'Branding' limekuwa likitumika vibaya na watu wengi sana, sanasana watu wa media. Neno hili linatumika kudhalilisha, kunyanyasa, kudhulumu wasanii bila kujua. Wanaotumia neno hili huwa Wana nia fiche ya kukuweka kapuni bila ya wewe kulalama ili uwape nafasi wawabebe wanaotaka kuwabeba.Ukweli ni kuwa in Africa hakuna msanii aliyeweza kutoka au ku hit kisa na maana ameji 'brand'. 90% ya wasanii walio hit wamebebwa na media au watu fulani maarufu. Na huu ndio ukweli wa mambo. Nipe majina ya wasanii watano unaodhani walijibrand ndio wakahit nami nikwambie ni nani amewabeba bila ya wewe kujua ndio Waka hit. Ukweli ni kuwa presenters wengi ni managers wa wasanii japo hili huwa linafanyika chini ya maji. Kinachofuata ni nyimbo kuchezwa kila siku na shows kupewa hao ili wapate commission. Kuna tofauti ya msanii kuwa na pesa na kufany...

GAVANA HASSAN JOHO........SISEMI KITU

Image
Huko akiendeleza miradi bumbum na kukuza uchumi,Gavana wetu shupavu alijitosa uwanjani hivi majuzi kusakata kabumbu. Mheshimiwa Ali Hasan Joho alikua kwenye uwanja wa Mlaleo 7-aside akipiga chenga mbili tatu. Uwanja huo uliotengenezwa kwenye safu za kimataifa utakua mstari mbele kukuza uchezaji soka miongoni mwa vijana wa pwani. Akiwa pamoja na Mheshiwa Bedzimba,Joho alionyesha weledi wake wa kutikisa nyavu na kuzituliza Vilevile.Tazama picha....

NAMELESS AINGIA WASAFI CLASSIC NA KUACHIKIA KIBAO HIKI AKIMSHIRIKISHA BEN POL (SKIZA HAPA)

Image
Nameless sio jina geni kwa wengi wetu baada ya kuwa kwenye tasnia ya mziki zaidi ya miaka kumi na tano. Baada ya kuachilia collabo na rapper Nyashinski, Nameless amepiga mbizi na kuingia studio ya Wasafi Classics na kufanya collabo na mkali wa Bongo Fleva, Ben Pol, YAMENIKUTA  Ngoma yenyewe pia imepitia mikono ya producer Sappy.

JAGUAR AMUONDOLEA GENERAL DEFAO AIBU (PICHA)

Image
Msanii wa mziki wa Lingala General Defao alijipata matatani baada ya kushindwa kulipia gharama za chakula za malazi, lakini akaokolewa na msanii wa Kenya na Director wa NACADA Jaguar. Muimbaji huyo mwenye umri wa miaka 57 alikuwa ameshikiliwa kwenye hoteli ya Rickseaside Villas huko Nyali. “Kutokana na tukio hilo la bahati mbaya la General Defao, aliyeshindwa kulipa bili kwenye hoteli ya Mombasa, nimejitolea kulipa kiasi hicho cha fedha kwakuwa mimi ni msanii kama yeye na hiyo inaweza kutokea kwa yeyote,” alisema Jaguar. Muimbaji huyo alikuwa anadaiwa Ksh 20,000

NEW VIDEO ALERT: WEWE - SUSUMILA ft AVRIL

Image
Baada ya kufanya collabo na King Kaka wa Kaka Empire, mkali wa Ziki la Nazi Susumila ameingia kwenye studio na kuangusha collabo nyingine na Avril, aliyes chini ya Kaka Empire. WEWE ni ngoma iliyoandaliwa na Produza Totti na Video kufanywa na Ricky Bekko. Icheki hapa --->