Ni tabasamu chungu nzima usoni mwa Kigoto baada ya msanii mwenzake Amoury Beybie kujitolea kumsaidia. Amoury Beybie ambaye anaendelea na uandalizi wake wa video inayozidi takriban milioni mbili amekuja wazi na kumsifu msanii Kigoto Mmbonde na kusema kuwa Kigoto Mmbonde ana kipaji kikubwa ila wasanii wamemtenga.Amourey amejitolea kumlipia na kumsimamia Kigoto video yake ya wimbo NAPENDA VIZURI..... ... Amourey alinakili haya kwenye mtandao wake wa Facebook.... "Kigoto Mmbonde ni kati ya wasanii ninao wakubali sana kimziki, ni mtunzi hodari, msanii mnyenyekevu..hana kiburi na majivuno.. mwenye bidii, anafanya nyimbo zenye ubunifu wa hali ya juu na ujumbe wa kueleweka, kutokua na sapot kwake kumenitia unyonge sana. Japo baadhi ya wasanii wamemtenga, na ameandika hits nyingi zilizofanya vyema, kwani siko tayari kuona kipaji na mtunzi bora aje akate tamaa baadae, ndio maana mimi binafsi kama # ARTIST_001 nitamsimamia VIDEO YA nyimbo yake mpya # napenda_vizuri ...