Posts

YAKWETU BAND : ISINGEKUWA LIZZ JASOLJAH BASI TUSINGELIJULIKANA!

Image
Band inayopeta kwa sana tu, Yakwetu Band imetoboa siri ya mafanikio yao. Kikundi hiki kilichoanza anza mbwembwe zake mwaka uliopita 2016 kimemtaja Lizz Jasoljah kama msingi wao wa kutoka kimuziki. "Kusema ukweli ule, isingelikua Lizz basi tusingefika tulipofika. Manake tulipojuana naye ndio mambo yetu yalianza kufunguka na yuyu huyu Lizz ndiye aliyetupeleka kwa producer Ammz na tukarekodi ngoma kwa jina Olele. "Walieleza vijana hao. Yakwetu, ilipata umaarufu wa haraka jambo lililopelekea wao kuchaguliwa kama nominees wa Pwani Celebrity Awards. Kwa sasa ngoma yao ya ''sugar" ipo hewani na inafanya vyema Sana.

PRODUCER WA PWANI AFUNGUKA MENGI KUHUSU SANAA YA PWANI. SOMA ZAIDI HAPA!

Image
Produza msanii Lameck Boy wa Neptune records alifunguka mengi kuhusiana na sanaa ya Pwani hapo jana,25th. 7.2017. Lameck Boy aliongea haya baada ya kuona msukosuko flani ndani ya dau hili la muziki wa Pwani. Tukinukuu.... " Sanaa ya Pwani kikweli iko na muziki mzuri,ambao mtu anaweza penda kuusikiliza nakuushabikia,wasanii wako wenye bidii,maproducer wazuri pia,watangazaji pia wazuri wanaosapot muziki.Wako wasanii tajika kama Susumila,Ally B,Nyota Ndogo,Chikuzee,Sudi Boy,Dogo Richie,Fat S,Fisherman,Escobah,Simon Simz na wengine,wako maproducer tajika,nikiwemo,akiwa pia P Baindo,Amz,Emmy Dee,Toti,Noor Mwamba,Tk2,J Crack,Lai,P Lion,Mobiz na wengi ambao tunafanya kazi nzuri. 2;Vitu ambavyo vinaweza au vinarudisha nyuma sanaa ya Pwani ni vitu vitano.... " 1. Wasanii kutopendana,kutofanya kazi pamoja,wasanii kujiona bora kumliko mwengine. 2. Maprodusa pia kukosa kuja pamoja nakushirikiana,wengine kujiona wao ndio wakali kuliko wengine,produsa kujifanya anajua kila kitu,k...

RAPPER KNAMY KREEZY SHARES TEN THINGS YOU DIDN'T KNOW ABOUT HIM

Image
Fast uprising rapper Knamy Kreezy shares some secrets we didn't know about him. The Thika based trapstar was raised in the Coastal parts of Kenya and later shifted to Thika with his family. Read on.... Lights........ Camera...... Action!!!! Here is Knamy Kreezy for you!!! 1) I can do any type of music but people think I only do hiphop. (This is true) 2) I dont have a sports club(specifically football) although I really love sports. (Okay....) 3)The girl I'm dating right now is the first that am being faithful at. (that means he's been a player to all the other chicks.....mmmmmhhh) 4) Ive always thought of doing gospel music in my life but found myself doing secular. (Thats the voice of God calling, don't ignore it, hell fire is waiting!) 5)I got my first tattoo when I was 13 years old.   (OmG!!! Tatto at 13? Most of us would have been disowned by our parents) 6) I cannot sit down and listen to my first song and I dont even have it in phone be...

RAPPER OHMZ LAW MOMBASA AZINDULIWA KWENYE DOCUMENTARY YA HIPHOP SAVES LIVES

Image
Rapper gwiji ambaye vilevile ni mshairi mkali, Ohmz Law Montana ameshirikishwa kwenye documentary ya kimataifa kwa jina Hiphop Saves Lives. Ohms, amekuwa mstari wa mbele katika harakati za kuenua jamii kupitia hiphop. Jamaa huyu vilevile ameandaa video kali chini Ya director Johnson Kyalo.

MIMI SI PETER MSECHU WALA SIHUSIANI NAYE.MSANII WA TAVETA AONGEA.

Image
MIMI SI PETER MSECHU WALA SIHUSIANI NAYE.MSANII WA TAVETA AONGEA. Msanii anayeibukia kwa kasi sana, Nashipai ameamua kuongea kuhusiana na swala lake la kuitwa Peter Msechu. Nashipai, anayetokea Taita Taveta aliyaongea haya baada ya video yake ANGEJUA aliyomshirikisha msanii wa Bongo linex kutoka. "Watu wengi wanasema video ile ni ya Msechu na Linex ndiye aliyepiga kolabo Na Msechu ilhali ni mimi. Kweli twafanana kimpango ila sihusiani naye wala ile nyimbo sio yake. Nyimbo ni yangu nimemshirikisha Linex. "Alitueleza kupitia njia ya Simu. Tazama hapa video yenyewe iliyoandaliwa Na X Benjoes....... https://youtu.be/yO6GAjwdqLc

SABABU KUU YA KIGOTO KUKIMYA KUFICHUKA!!!! SOMA HAPA!!!

Image
SABABU KUU YA KIGOTO KUKIMYA KUFICHUKA!!!! SOMA HAPA!!! Aliwika sana na kujizolea sifa kem kem kutoka kwa mashabiki sio wa Pwani bali Kenya nzima. Tunamzungumzia msanii sifika Kigoto Mbonde. Staa huyu wa Kichapo cha Mapenzi alitoa hit kali kali zilizomfanya kuwa kipenzi cha watu. Kigoto alifanya kazi studio kadhaa ila urafiki wake wa karibu sana ulikuwa kwa studio ya Produza Tk2,hapa tunazungumzia Hornet Records Na baadae Number one records. Baada ya purukushani zisizoeleweka Kigoto alikatiza muziki ghafla na kunyamaza zii. Majuzi alirudi kupiga collabo Na Mswazi Masauti ambaye amenyamaza vilevile, nyimbo ikijulikana kama "Sawa." Cha kushangaza nyimbo hii haikupokelewa vyema Na ikabidi Kigoto kuingia mitini. Meza yetu ya habari ilichukua jukumu la kuwasiliana na Kigoto kuhusiana na ukimya wake na hapo ndipo tulipobaini kuwa jamaa huyu alikua masomoni. "Wajua mimi nilipomaliza shule ya upili, moja kwa moja nikaanza muziki hivyo sikupata nafasi ya kusoma. Sasa ku...

RINGA TALEMO AWACHIA VIDEO MPYA AKIWAHIMIZA WASANII WAFANYE VIDEO ZAO NA WAAANDALIZI WA PWANI

Image
Msanii Ringa Talemo Leo hii ameachia video yake ya Nipe Nipagawe chini Ya uandalizi wake produza Nau. Talemo alirekodi wimbo wake ndani ya Thundersounds kwa produza Morbiz almaarufu Sherrif na akaamua kufanya video papa hapa Pwani. "Nilionelea kazi hii nishughulikie hapa kwetu Pwani kwani waandalizi wa video wamekua wengi na wanajaribu sana kwa kazi zao.Kama wana uwezo kwanini tusikuzane sisi kwa sisi. Haina haja twende hadi Nairobi kufanya video ilhali Pwani kunao walio Na uwezo kama vile Produza Nau aliyedirect video yangu ya Nipe Nipagawe. " Alieleza Ringa Talemo kupitia njia ya simu. Tazama video hapa Na uone kama imeweza ama bado ------ >>> https://youtu.be/xGY5ALg0T8A