Posts

Showing posts from February, 2017

RE: SAUTI SOL TO HEADLINE NAKURU CHROME MEGA BASH

Image
In order to bring an unforgettable experience to its fans, Kenya Breweries Limited (KBL) through Chrome Vodka Brand will host “The Chrome Mega Bash with Sauti Sol” in Nakuru, which will be headlined by the afro-pop group. This follows the renewal of the partnership between Chrome Vodka and Sauti Sol in December 2016 which followed a successful Street Bash held at Choices Bar along Baricho Road. Details of the event are as follows: What: Chrome Vodka Street Party When: Saturday, 4th March 2017 Where: Grill Park Lounge, Nakuru Time: 6:00 p.m. till late Sauti Sol signed a partnership in February 2016 with Chrome Vodka to help drive the brand’s marketing campaign ‘Dream Big, Be Bigger’ #ShineOn. This was executed through a series of nationwide concerts and on-ground activations. Last year, Sauti Sol held a nationwide tour to popularize their ‘Live and Die in Africa’ album benefitting Chrome Vodka.

TANZANIAN MEDIA PERSONALITY MIMI MARS LAUNCHES MUSIC CAREER WITH "SHUGA"

Image
Mdee Music presents their latest music act Mimi Mars, sister to celebrated Tanzanian pop music queen Vanessa Mdee in her debut single "SHUGA", produced at Hightable Sounds. Shot in Dar es Salaam by the Tanzania director Hanscana, the colorful music video has cameos by Tanzanian superstars like Navy Kenzo, Rosa Ree, Wildad, Quick Rocka just to name a few. "SHUGA" is nothing but sweetness. "SHUGA" will leave you on a suger high, thanks to its dose of funky freshness. Mimi Mars is a media personality who has over the years established herself as a respected YouTube, TV personality and mcee. In her new music venture, the husky-voiced songstress lures you into her world with a sultry tone and her amazing vocals. Thanks to Mdee Music, the creators of mega hits including Niroge, Hawajui, Never Ever, Nobody but me ft South Africa's K.O.  – Mimi Mars is already in great company as she takes on a new career path.

VIDEO NZURI YAJIUZA YENYEWE----SIRI YAVUJA!!!!

Image
VIDEO NZURI YAJIUZA YENYEWE SIRI YAVUJA!!!! Wengi wa mashabiki na wanaofuatilia sanaa ya Pwani watakubaliana na mimi nitakaposema kuwa watu wengi hawazipendi au kuzifagilia video za pwani.....ndio au la? Jibu unalo mwenyewe. Kasumba hii imejengwa kutoka zamani hivyo basi watu washazoea kuwa hakuna video au ni video chache za pwani huwa nzuri. Na kama ni nzuri basi sio kampuni au director wa pwani aliyeandaa video hiyo. Ni hivi juzi tu msanii tajika wa hapa pwani alipotoa video mbovu mno iliyokosa kabisa vigezo vya kuchezwa kwenye 'mainstream media' kama wasemavyo wazungu. Yote tisa,kumi ni kuwa wasanii watatu waliamua kuja pamoja ili kuweza kugeuza dhana na kasumba ya kuwa pwani hawawezi kutoa video nzuri.Benso,Gee Gee na Kigoto waliyatumia mandhari yaya haya ya pwani kutekeleza kazi yao.Matokeo ni kama muonavyo kwenye picha hizi..........

DONDE KUTOKA KWA UTANGAZAJI HADI KWA UTETEZI WA WANANCHI.

Image
Alianza utangazaji zamani na wengi wetu twamfahamu kutoka enzi akiwa Baraka FM. Donde Samora,mtangazaji mcheshi anayependwa na wengi kwa weledi wake wa kuongea na kuweka mambo wazi aliamua kujiunga na siasa na wengi walijiuliza maswali yaso majibu.... Donde,ambaye alitetea sana vipaji vya wasanii hasa wanaoibuka aliamua kuingia siasani sio kwa minajili ya manufaa yake mwenyewe bali kuwahudumia wananchi wa eneo la Junda na kuwapa mkono vijana wa Pwani wazidi kukua kimaisha. Katika mikutano ya siasa,jamaa huyu huwa sio mwingi wa maneno vile ila katika project z kusaidia jamii hapo ndipo utakapo muona mstari wa mbele akisaidia kwa hali na Mali. Ama kweli sio kwa utangazaji pekee ambapo Donde amebarikiwa bali hata kutetea haki na kuhimiza maendeleo ya jamii ndiposa wanaJunda wamempa jina MTETEZI WA WANYONGE!

JE ULIPITWA NA INTERVIEW YA 'KARIBU MOMBASANI' NDANI YA BARAKA FM HAPO? TAZAMA HAPA UPATE UHONDO!

Image
JE ULIPITWA NA INTERVIEW YA 'KARIBU MOMBASANI' NDANI YA BARAKA FM HAPO? TAZAMA HAPA UPATE UHONDO! Hapo jana kulichimbika ndani ya Baraka fm pale Benso na Miss Gee gee walipovamia kipindi cha THE MEGA BREAKFAST mida ya asubuhi. Wasanii hao,wakiwa katika pilka pilka zao za kuipa promo video yao inayokuja ya KARIBU MOMBASANI waliingia kwa mbwembwe nyingi na kuwazawadi watangazaji wote kwa t.shirt za BCMG. Benso alieleza wazi kuhusu fununu za video yao na jinsi watu wanaivyoizungumzia na kuweka ukweli wote wazi pasi kuficha lolote.Cheki picha hapa - >>

PATA KUMFAHAMU MSANII PERMIUS.ONE ON ONE INTERVIEW.

Image
PATA KUMFAHAMU MSANII PERMIUS.ONE ON ONE INTERVIEW. PWANI USANII JE WANAKUITA NANI JINA LA KISANII? PERMIUS: Jina la usanii naitwa Permius. PWANI USANII:MUZIKI ULIANZA LINI? PERMIUS:Muziki nilianza mwaka wa 2015 hapo ndipo nilianza kuenda studio. PWANI USANII:ENHEE TUELEZE ZAIDI: Nilipatana na kijana mwenzangu mwimbaji kwa jina Burning ice ambaye vilevile ni Produza na akaamua kunikuza kimuziki na kunipeleka kwa studio yake kwa jina Trace records iliyopo Malindi. PWANI USANII:LABDA KAZI ZA KIMUZIKI ULIZOFANYA TRACE RECORDS NI KAMA ZIPI? PERMIUS:Kazi nilizofanikiwa kufanya Trace Records ni nyimbo ya kwanza kwa jina- sitaki tena ambayo inapatikana mdundo .Mwaka jana,2016 nikafanya kazi mpya kwa jina -leo na kesho ambayo mashabiki walipenda na kunipa morali. PWANI USANII:KWA SASA LABDA UNA KAZI MPYA YOYOTE? PERMIUS:Yeah,kuna kazi mpya nimefanya nikimshirikisha Burning ice na nimepanga kuwashtua mashabiki.Kazi hiyo nitakua naiwachilia karibuni....

WATALII WA KIGENI WAJAZANA KWENYE VIDEO YA WASANII WA PWANI!!!!

Image
WATALII WA KIGENI WAJAZANA KWENYE VIDEO YA WASANII WA PWANI!!!! Huku mwaka ukizidi kusonga mbele mdogo mdogo,wasanii wanazidi kupambana kimuziki na kutengeza audio na video ili wasipotee kwenye chati za muziki. Benso ,Kigoto na Miss GeeGee kamwe hawajaachwa nyuma kwani watatu hawa wapo katika matayarisho ya video yao ya Karibu Mombasani na watalii walijazana furifuri kuipamba video hiyo. Fununu ni kwamba,mandhari ya video hiyo wakati wa uandalizi wake uliwavutia watalii sana na wakaamua kujiunga kwenye camera kuuza sura!

SAHAU BAIKOKO NA VIDEO ZA SNURA....HII HAPA ITAKUPAGAWISHA!!!!

Image
SAHAU BAIKOKO NA VIDEO ZA SNURA....HII HAPA ITAKUPAGAWISHA!!!! Kuyeyusha viuno na misakato ya tumbo na makalio ndio mvuto wa video nyingi za muziki w kileo wa Zanzibari na visiwa vya pwani mwa Afrika Mashariki. Video ya "karibu Mombasani" ya wasanii Benso, Kigoto na Miss Gee Gee imeamua kuvuka mipaka yake na kuachia zaidi ya mitindo ya baikoko na kusakata viuno chini kwa chini na kuvipelekwa sako kwa bako ? Sababu kuu ni gani? Labda muelekezi wa video hii ambaye ni Peterz hakutaka kuwacha nje kipengele chochote kile cha tamaduni za upwani....tazama picha hapa -- >>

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

Image
MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMANI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!! Huu bila shaka ni moto wa kuotea mbali na wasanii hawa wamejizatiti vilivyo kuwaleta warembo tele kwenye video yao.Sio warembo tu bali warembo wa kuvutia na kuridhisha nafsi. Wimbo wenyewe ni KARIBU MOMBASANI wa Benso,Kigoto na Miss Gee gee uliotoka mwisho wa mwaka Jana.Kamwe hatujui kulitumika mbinu gani kuwatafuta models wa sampuli hii ila tunachojua ni kuwa hawa sio wale wa kuokota mitaani au vichochoroni bali mabinti wanaofanya uanamitindo wa kulipwa. Bado tukiisubiri video yenyewe itakayotoka hivi karibuni,picha hizi dhahiri shahiri zadhihirisha uzuri unaokuja......