Posts

BAADA YA KIMYA KIREFU SHAMANIZ ARUDI TENA NA MPENZI WA KIZUNGU!

Image
Mara ya mwisho kumsikia ni wakati wa nyimbo yake 'Romeo and Juliet'. Binti huyu,Shamaniz Ann mwenye sauti inayovutia ja ninga alipamba redio zetu kwa midundo motomoto. Baada tu ya kukatisha mkataba wake na Produza Khalid wa A million records,msanii huyu alikimya kabisa. Si mitandaoni,redioni hata mitaani. Baada ya kimya, Shamaniz amerudi kwa kishindo na amepachika picha ya 'mzungu wake' ambaye mwenyewe anadai kuwa si kibabu. (PWANI USANII ONLINE RADIO LISTEM HERE) https://www.spreaker.com/user/9366849/vichapo-motomoto_1 Tazama screenshot ya alichonakili kwenye akaunti yake ya fesibuku.

HIVI JAYSTAR KAMPOKONYA SUSUMILA DANCER WAKE?

Image
Jaystar msanii aliye chini ya management ya Vanilla fleva entertainment yaonekana kasepa na dancer mmoja wa Susumila. Dancer huyu aliyekuwa sako kwa bako na msanii Susumila na alikua chini ya Wachawi International ameonekana kwenye show za Jaystar na hata kwenye video ya Jaystar mpya.

PRODUZA BILLY MOYSES ARUDI KIMUZIKI NA KUTAMBULISHA KUNDI LA WATOTO.

Image
Produza aliyevuma kwa kibao mtazamo.Billy Moyses baada ya kimya kingi ameamua kuzivaa njuga na kurudi ulingoni. Produza huyo aliyemiliki studio yaNewdawn records alipotelea masomoni kwa mwaka mmoja. “Nilikuwa naongeza ujuzi zaidi na vilevile kutafuta vyombo vya kisasa vya kuandaa muziki.” Alieleza BillStudio yake kwa jinaBaraka music  imefunguliwa rasmi na Produza huyu yupo tayari kufanya kazi na msanii yeyote.  Vilevile,ili kuregesha shukrani kwa jamii,Billy Moyses amewachukua watoto mayatima nakutengeneza bendi nao.Watoto hao wanaotoka orphanage yaLIKONI AIDS ORPHANAGE watarekodiwa album moja bure na kufanyiwa marketing. Pesa zitakazo patikana kutoka kwa kazi hiyo zote zitaenda katika elimu ya watoto hao. Bendi hiyo ya watoto watano yafahamika kama LAOP MELODIES na tayari washawachia kibao kipya PARADISO.

PATA KUMFAHAMU MSANII PRINCE WA KIKOSI CHA TEAM RIYAL TALENTS.

Image
Kwa majina kamili ni Samir Said na jina la usanii anafahamika kama Prince. Msanii huyu aliye chini ya himaya yake msanii MNS,ndani ya lebo ya Team Riyal Talent alianza usanii kitambo kidogo wakati alipokua shule ya upili. Enzi hizo, Prince alikua gwiji wa tamasha za muziki na michezo ya kuigiza shuleni kwao (Kenya music and drama festivals).Akiandika na kuelekeza mashairi hadi Kiwango cha kitaifa.Mwaka wa 2006,Prince aliibuka mshindi kwenye ulingo wa ushairi katika kitengo cha kitaifa. Msanii huyu anayefanya muziki wa kipwani vilevile hufanya mitindo ya rnb,afro-fusion na trance. Prince ameandaa kibao kipya kabisa akishirikiana na Msanii Mejakali na MNS. Wimbo huo kwa jina 'Sweety' utadondoshwa hivi karibuni. Studio za RECORD ON STUDIOS QATAR na BIGFOOT PRODUCTION ndizo zinazomsaidia Prince kunoa makali yake kimuziki. Producer Lee wa Qatar humpa wakati msanii huyu kupiga tizi na kumhimiza kujikaza kisabuni huku Produza Baindo akimtengezea midundo ya kimwambao. Kinach...

KASSAMONEY, BENSO, ODINAREH,CHIKUZEE KWENYE SHOW YA PWANI USANII RADIO

Image
Kila uchao,Pwani Usanii Entertainment imejaribu kupanua mbawa zake na kupeperuka juu zaidi. Japo kwa stepu ndogo ndogo,moja baada ya nyingine twasonga mbele. Sikiza kipindi hiki kisha utoe maoni.Bonyeza hapa -- >>>> https://www.spreaker.com/user/9366849/kassamoney-benso-odinare-c-nee

MATATU ZA MOMBASANI KUCHORA WASANII WA NYUMBANI!!!

Image
Yaonekana kazi zimeanza kusifika kwa wingi mjini. Hii inadhihirika pale matatu kadha wa kadha zilipoonekana kubandikwa picha za wasanii wa pwani. Mara Sudiboy,mara Susumila,Dazlah na Lavichunare.Cheki hapa-->>

VIPODOZI LAZIMA: NYOTA NDOGO AFUNGUKA!!!!!

Image
VIPODOZI LAZIMA: NYOTA NDOGO AFUNGUKA!!!!! Baada ya kukiri kuwa hatowahi piga make-up na vipodozi tena. Mama wa sanaa ya pwani ameshindwa kuvumilia na ameregelea urembo. Nyota,aliwahi ahidi kuwa atabakia natural kama alivyozaliwa ila yaonekana ahadi ameivunja!