Posts

HIVI JE KUNA GHOST MUSICIANS WANAOLIPWA NA MCSK KISIRISIRI.YAMEMWAGIKAAAAA!!!!!!!!!SOMA HAPA!!!!

Image
 Wasanii kadhaa wa Nairobu na wengine wa hapa pwani wameamua kuleta vurumai na mwamko mpya. Jamaa hao walioamua kutolala njaa wamesema kuwa kunao wasanii ghost yaani wasiojulikana wanaoliopwa kisirisiri na MCSK.  Kundi flani la wanamuziki hapa Pwani wameshikana na wenzao wa Nairobi na kusema wataandamana kwa ajili ya "Ghost Musicians" wanaodaiwa kulipwa huku wengine wakililia patupu. Vilevile wasanii wa Pwani wanachukua miaka na mikaka kupata nambari ya membership. Regional Director wa MCSK hapa pwani bwana Sango naye amekuwa kimya licha ya kutoa ahadi tele kwa wasanii.

DIAMOND ASEMA HASHIKI SIMU YA ZARI KWA SABABU HATAKI KUUMIA MOYO.

Image
Daah hii sasa balaa tupu,ingawa wana mtoto masuperstar hawa wawili bado wana matatizo ya uaminifu. Diamond president wa Wasafi amemwaga mtama kwenye kuku wengi na kudokeza hadharani kuwa hawezi kamwe kushika simu ya mkewe Zari kwa sababu hataki kuumia moyo. Swali ni je wewe waweza shika simu ya mumeo ama mkeo? “Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa,” alijibu Diamond alipoulizwa na Millard Ayo kama huwa anashika simu ya Zari. Diamond aliendelea kutoa sababu za kutoshika simu yake, “sidiriki kwasababu namjua ni binadamu , unajua sometimes ukizingatia na yeye (Zari) ni mtu maarufu so sometimes watu wengine wanakuwa wanamsumbua, anaweza kukutwa na vishawishi sometimes anaweza akamjibu mtu akaitikia tu poa, kwangu mimi kikanikwaza kwasababu nampenda kwahiyo ikaniumiza, kwahiyo sitaki kabisa kushika simu yake.” Pamoja na kwamba yeye hashiki simu ya mpenzi wake, vipi kuhusu Zari kushika simu yake? “ Simu yangu mi haina password naiachaga tu lakini nafi...

RICH MAVOKO ATUMIA MKOROGO KUWA MWEUPE??? .DAAAH CHEKI PICHA HAPA!!!!

Image
Afrika Mashariki inajivunia kipaji cha Rich Mavoko ambaye kwa sasa ameachia kibao kipya kwa jina NAAMINI. La kushangaza ni kuwa jamaa huyo amezidi kuwa mweupe kila uchao. Sijui anataka kujifanya Michael Jackson au vipi ila kulingana na blog ya Bongo Swaggz picha hizi zake za zamani na za sasa zitasema yote. Kabla

TAZAMA BEHIND THE SCENES YA VIDEO YA "BILA WEWE" YA DULA THE AFRICAN SONGBIRD.

Image
Anaitwa Triple A au ukipenda Dula the African Songbird na chini ya A million videos ya Khalid produza ameandaa video ya wimbo wake BILA WEWE.Video hii atakayo iwachia 3rd December itasumbua sana.Cheki behind the scenes hapa.

"INTERCONTINENTAL SCAR" YA HUSTLA JAY YAPATA TEULIWA KWA TUZO ZA KIMATAIFA ZA FRANCE.

Image
Tulimsikia kwa Mara ya kwanza kwa kibao MINYORORO YA HAKI iliyoshika chati sana na kufanya mapinduzi kwenye sanaa ya Afrika Mashariki. Hustla aliye na hulka ya kuifundisha jamii kwa kupigania haki kupitia muziki wake ameteuliwa kuwania tuzo fulani ambapo video yake imechaguliwa katika kipengele kimoja kwenye tuzo hizo.  Kumpigia kura Send the number " 2 " on email finale@lereveafricain.com / 1 email address = 1 vote

FYATENI NDIMI ZENU WANAHIPHOP WA PWANI WANAOJISHASHA FACEBOOK. TAZAMENI RAPPER MKALI WA FASTCASHMUSIC GROUP ANAVYOMWAGA MICHUZI!!!!

Image
 Huwa wafokaji wa pwani hupenda kupiga kelele mitandaoni jinsi walivyo wakali na muziki wao unvyotamba.Kumbe zote huwa kelele tu ila hakuna kazi yoyote inayofanyika. Ndiposa wakati mwingine inapaswa turudi chini na kunyenyekea na kuwa wakweli. Sio kujisifu na kukashifu presenters kuwa hawachezi miziki na nyimbo zenu mpya ilhali bado mnatapatapa na kuandaa vitu borohoa. Hivyo basi, tazameni mwanahiphop kwa jina KRG ceo wa FASTCASHMUSICGROUP anayetokea Nairobi anavyovuja mkwanja.  Jamaa huyo alimnunulia demu wake bonge la gari baada ya kumrushia Party.  Cha msingi ni STAY HUMBLE ALWAYS.

MAHABUBA ISHAPIKWA IKAPAKULIWA! TAZAMA VIDEO YOTE HAPA!!

Image
Imekuwa midomoni mwa watu na imetrend mitandaoni kwa sana tu. Ila Leo lazima kieleweke...Tunazungumzia video ya Mswazzi Masauti "Mahabuba." Produza Tedd Josiah amewatoa wasanii wengi tu na hapa hajacheza karata zake vibaya. Mahabuba, video iliyochukua siku sita ikiandaliwa sehemu tofauti huku pwani lazima itasumbua sana sio kwa runinga, radio, mitandaoni hadi mitaani. Mswazzi Masauti amejaribu kuweka fleva za kimwambao kwenye mdundo tulivu wa rnb uliokolea nyuzi za gita na sauti tamu za vinanda. Video maridhawa yenye mvuto mzuri na rangi za kupendeza zilizooana vyema na ujumbe unaopitishwa imeleta dhana nzuri kwa mada ya mahaba inayozungumziwa. Tusitumie mate ilhali wino upo.......video yenyewe hii hapa.Tazama kisha utoe maoni--------