Posts

P-DAY MSANII WA AHADI.......

Image
Mwaka uliopita msanii P-Day na Alkenia Luv waliwaahidi dancers wote wa Mtwapa Talent search season one kwamba watapewa nafasi Kuwa kwenye video ya NIRINGE NAYE.Video ilipotoka,kweli P-day aliitimiza ahadi yake.Video ya NIRINGE NAYE iliyoandaliwa na Jeff Santana ilikuwa na dancers wote aliowaahidi.Leo msanii P-Day ameamua kulipia fee mwanafunzi wa Mwatate mix secondary.Kisa na maana kajiita jina lake P-Day. "...HAHAHA NIMEPATA HABARI KUA KUNA DOG O FLANI MWATATE MIX SECONDARY ANAJIITA ( PDAY ) NIMESKIA POA SANA COZ AV ONLY SEEN SOME FEW KENYANS CALLING THEMSELVS 2PAC ATHERS BEYONCE,LYL WIZ BT Alocal artist like me aving afan like him!!!, growin wid my name?irealy appreciate....napanga nifike apo nikuone na ikiwezekana nlipe fee mwaka mzima." Msanii ni kioo cha jamii.

NYOTA NDOGO KUFUNGUA REDIO STESHENI YAKE BINAFSI .

Image
Mama mlezi wa sanaa ya pwani aka Nyota Ndogo yaonekana kila uchao ana mapya mazuri. Msanii huyu ambaye ameingia tu majuzi kutoka ng'ambo amewasili na habari njema ambazo wasanii wa pwani watakua na raha kabambe wakizipata.Nyota yupo katika harakati za kufungua redio stesheni yake. Nyota alikuwa na haya ya kutujuza......... "Moja kati ya mipango yangu ni.niko katika hatakati za kufungua radio yangu.itakayo itwa MAMA NYOTA FM.msicheke maana ni moja ya ndoto ya mda mrefu.cooming soon." Habari ndivyo hii na twamtakia kila la kheri na bila shaka akifanikiwa Pwani usanii,backstreet entertainment, the greatmulley,Solo King,Ommy Dallah na bloggers wote hatutakosa kipindi chetu cha udaku.

MSANII YAGAYAGA ANAYEISHI BAHARINI MAMANGINA.

Image
Msanii huyu kutoka hapa mkoani pwani kwa majina Yaga Yaga ni jamaa ambaye anaishi maisha ya kubahatisha ila yee hushukuru mwenyezi Mungu kila kuchao kwa kumpa uhai. Yaga Yaga hana makao maalumu na yeye hulala kando ya baharini kule mama Ngina manake huko ndio nyumbani aanakojua. Kando na hayo yote msanii huyu hujibidiisha kwa kufanya vibarua vidogo vidogo hapa mjini na kuchanga hela za kurekodi studio. Ameweza kwa sasa kurekodi nyimbo mbili Kule SQ Records na akafanya video moja. Yeye husema hawezi kufa moyo kwasababu ya maisha yake ya upweke manake anaamini ipo siku atakuja faulu kupitia kwa kipaji chake cha usanii... $hukrani kwa ‪#‎ backstreet‬ entertainment.Yagayaga twakutakia kila la kheri.

KIGOTO MMBONDE-NAPENDA VIZURI.JE USHAISIKIZA?KIGOTO ALILENGA KINA NANI?

Image
Chini ya produza Tkmbili,Kigoto Mmbonde amejaribu kuuteka mtindo mpya unaovuma kwa saa hapa Pwani na bongo. Tukianzia kwa kuuchanganua mdundo wenyewe, producer Tk2 amepanga vyombo vya muziki akifuatilia mtindo unaosambaa kwa sasa. Mdundo wenyewe unafuatana au lingana na ule wa YA MOTO band ila Tk2 ameambatanisha vyema vyombo vya muziki na kuupata kama ulivyo. Tukiskiza wimbo wenyewe sasa, Kigoto ameamua kuwaeleza watu fulani kwamba yupo imara na anatosheka kwa kile apatacho. Kama kawaida tunavyofahamu msanii huyu si mchache wa mane no na vijembe, amewapaka jamaa Fulani kwa vidaka vya maneno na tayari tushafahamu ni kina nani. Ukitaka kufahamu zaidi bila shaka wimbo upo mitandaoni na redioni.Napenda vizuri.

HAPPY BIRTHDAY TO HAMISI YUSUF WHO TURNS 2 YEARS

Image
Anapenda mziki kama babake Susumila na leo PWANI USANII family wishes the young lad HAPPY BELATED BIRTHDAY as he turns 2 years

BENSO-"IMEREMENDE" MWAKA HUU NDIO MOTO ZAIDI!!!!!

Image
Huku kila uchao mashindano ya muziki yakizidi kupamba moto kwenye tasnia ya Sanaa ya Pwani na Afrika mashariki kwa jumla.Ambapo baadhi ya washika dau wa sekta ya muziki kudai Kuwa muziki wa Kenya umekufa,msanii Benso ameamua kuweka bidii zaidi ili kuregesha sifa ya muziki wa Kenya.Mwanamuziki huyu aliyetuzwa kama mwanamuZiki bora wa kiume kwenye Coast music awards mwaka Jana chini ya BRAIN CHILD MUSIC GROUP ameandaa video ya kimataifa itakayowazuzua Wengi. Benso ambaye hupenda kugaramikia video sake,raundi hii amedhihirisha wazi kuwa yeye ndiye bingwa wa muziki na video safi Pwani kwa Afrikaa mashariki.PATA KUITAZAMA VIDEO YENYEWE HAPA-- . https://m.youtube.com/watch?feature=youtu.be&v=yE9EfR8BepU

MSANII PAPAH AGADHABISHWA NA KITENDO CHA SHETTAH KUONGELEA VIBAYA WIMBO "DATA"

Image
Papah au ukipenda Agiza Nitakuja lipa msanii imara wa Hornet records amegadhabishwa sana na msanii Shettah wa bongo aliyekuja Mombasa na kufanya collabo na Msanii Kigoto.cGwiji huyu amekashifu vikali maneno ya Shettah na hivi ndivyo alivyonakili....... " Shetta from TZ, he is very stupid and primitive. alipokuja Hornet Records Mtwapa kufanya track na Kigoto, I wanted him to pay but Welo Kagomaz and Shetta himself, w akadai niwaruhusu wafanye kazi na Kigoto ili waka market studio TZ. Saa hii adai ilikuwa ZOEZI akaenda fanya tena na DIAMOND. Alafu ana kashifu kazi zetu?! Sina number zake bt mkimuona mwambie ameambiwa awache UPUMBAVU hakuna studio ya zoezi MOMBASA. Sasa basi Blog n radio station za Coast twawaomba muache kuwapa shavu sana hawa makafiri wa Tz because wanamaudhio sana alafu uko kwao sisi atupewi shavu."