UIMBAJI NA UCHORAJI NDICHO KIPENZI CHA MSANII J'S.


UIMBAJI NA UCHORAJI NDICHO KIPENZI CHA MSANII J'S.

Ama kweli Mungu hutujalia kwa vipawa tofauti tofauti ila kwa Joseph Ngila,Mungu amemjalia vipaji viwili ambayo vyote anavitumia kujifunufaisha na kuelimisha jamii.

Joseph Ngila Ngonzi almaarufu J'S ni mzawa wa papa hapa Mombasa eneo la Changamwe Soweto kisumu ndogo. Uchoraji wake na uimbaji ulianzia shule ya msingi ya Mwijabu.
Kwa umri mdogo sana,J'S aliwashangaza wengi kwa kuchora picha zenye mvuto zilizompelekea yeye kuwa kipenzi cha walimu,akiwasaidia kuchora chati na mabango ya shule.

Tukija kwa kipaji chake cha uimbaji,J'S alikuwa na haya ya kueleza.......
"Nilianza kuimba nikiwa na miaka kumi na mbili ila utunzi wa nyimbo nilianza mwaka wa 2000.Niliupenda muziki jambo lililopelekea mimi kuunda kundi Langu la muziki lililojulikana kamaJ.E aka Joseric."
Kwa sasa msanii J'S yupo na ujio mpya kabisa chini ya Bullet music na ataiwachilia nyimbo hiyo hibi karibuni. Nyimbo yenyewe inajulikana kama TIA BIDII.

CHEKI BAADHI YA MICHORO YA J'S.


Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA