DULLY MELODY AMPONGEZA DIRECTOR WA VIDEO YAKE YA KIVUMBI.


Video Director:Thomas.
DULLY MELODY AMPONGEZA DIRECTOR WA VIDEO YAKE YA KIVUMBI.


Supasta anayechipukia kwa kasi, Dully Melody amekuja wazi na kumpongeza mwandalizi wa video ya wimbo wake 'KIVUMBI'
Dully, alimpongeza sana director Thomas Tomsy anayetokea Nakuru na akasema kuwa jamaa huyo ni mwenye moyo mzuri wa kusaidia na kukuza vipaji.

"Sio kwamba eti pwani hakuna waandalizi wazuri wa video,wapo wengi sana ila nilipendelea kufanya kazi na director Thomas kwa kuwa Thomas alianza kunifuatilia mimi kama msanii pindi tu aliposikia nyimbo yangu ya kwanza hongera.Japo yupo Nakuru,amekua akinipa motisha na hata kusambaza muziki wangu sana ndiposa nikaona nifanye kazi naye na vilevile kwa sababu Thomas yupo Nakuru na mimi nipo Pwani basi ni kama tutakuwa tukeshika Kenya nzima kwa ushirikiano wetu kutoka magatuzi tofauti."Alitusimulia Dully.

Video ya Kivumbi ambapo Dully amemshirikisha rapper wa kike CML tayari ishakamilishwa uandalizi na hivi karibuni basi itawachiliwa rasmi.
Kwa sasa single ya wimbo hiyo tayari ishapeta maredioni.

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA