CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WASANII WA LAMU.




Wengi Wetu tunausikia mji wa Lamu kwa utajiri wake wa kitalii na tamaduni za kiswazi ila hatujui kwamba wapo wasanii wa kizazi kipya wanaofanya muziki kwa bidii.
Tulijaribu kuwasiliana na baadhi ya wasanii wanaotokea Lamu na walikua na mengi ya kutueleza kuhusu kufanya muziki Lamu.


Kikosi cha IslandLove records kikiongozwa na meneja wao kwa jina Enoch,walituwekea mambo bayana. Man Azzer na producer Doni ambaye vilevile ni msanii walipasua mbarika na kusema kuwa wasanii wa Lamu hawadhaminiwi na kuheshimiwa kama wenzao wa Mombasa.

"Kaunti yetu ya Lamu haithamini kazi za wasanii wa kizazi kipya. Katika tamasha za viongozi wa serikali au wanasiasa hatuitwi wala kupata hata mualiko wa kutuimbuiza na kuonyesha vipaji vyetu." Alieleza Man Azzer.

Vilevile Produza Doni aliongezea kuwa vituo vya redio vya pwani vimewatenga sana wasanii wa Lamu. Doni alikua na haya

ya kusema kuhusiana na swala la redio......" Stesheni za pwani zimewakandamiza sana wasanii wa Lamu na Lamu bado ni pwani. Sisi ni wasanii kama vile wale wa Mombasa,Malindi na Kwale. Ila hatuchezwi kamwe kwenye stesheni. Hii inapelekea mashabiki kutotutambua."

SWALI NI NANI ATAKAYETATUA SHIDA ZIWAKUMBAZO WASANII WA LAMU????

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA