Je msanii Susumila alimwacha mkewe sababu yake Kush Tracey?
Baada ya kukiri kuachana na mkewe,
msanii tajika Susumila almaarufu "Mr President" , anadaiwa
kuwa na ukuruba wa kimapenzi na msanii wa kike kutoka Nairobi, Kush
Tracey msanii anayetamba na ngoma ya Huezi Nidandia. Akihojiwa na
kituo kimoja cha radio mjini Mombasa, Susumila aliweka bayana
kuachana na mkewe ambaye amezaa naye watoto wawili. "Yeah ni
kweli tuliachana na mke wangu" alikiri msanii huyo. Alipoulizwa
kuhusiana na Kush Tracey ambaye tayari ashafanya naye colabo kama ana
uhusiano wa kimapenzi naye alijibu kwa ufupi "No comment".
Naye Kush Tracey alipoulizwa kama yeye ndiye aliyemfanya Susu kuachana na
mkewe ili ampate Susumila pia yeye alijibu,"No comment".
Wawili hao tayari washafanya collabo inayotamba kwa jina Umenitosha, ngoma iliyosukwa na AMZ na Amoh
Lakini maswali yanayo wagonga vichwa
mashabiki na washikadau wa mziki ni je wasanii hawa wawili
wanauhusiano wakimapenzi au ni mziki tu? Mambo ya collabo hayo.
By Nina Kagia
By Nina Kagia
Comments
Post a Comment