HIVI MSANII DOGO RICHIE ANAWATONGOZA MASHABIKI ZAKE....????
Hivi majuzi meza yetu ya habari kupitia ujumbe wa facebook ilipewa habari kabambe kutoka kwa mwanadada kwa jina REE THE BOSSET kuwa Msanii DOGO RICHY anamtongoza kimapenzi. Mwanadada huyo alitutumia jumbe za simu zenye maongezi yake na Dogo Richy. Jumbe hizo ambazo zina maneno mazito mazito tumeshindwa kuziweka hapa kwa sababu ya adabu na heshima ya Dogo Richy na Ree The Bosset. Dogo naye kwa sasa anavuma kwa video yake mpya ya Hayana mjuzi.Jitihada zetu za kuwasiliana na Dogo Richy hazikufua dafu ila swali ni je ni kweli. Dogo Richy anawanyemelea mashabiki zake wa kike?
Comments
Post a Comment