OTILE BROWN-APEPERUSHA BENDERA YA MUZIKI WA PWANI JUU ZAIDI
Otile Brown msanii anayetokea papa hapa pwani ila anafanyia muziki wake Nairobi ameamua kufunguka na kueleza mashabiki mambo mazuri. Msanii huyu ambaye kwa mara ya kwanza tulimsikia kwa kibao chake kikali IMAGINARY LOVE alichomshirikisha Khaligraph Jones ametueleza kuwa yupo tayari kuwapa burudani la kukata na shoka na amefurahi sana jinsi wa pwani walivyoupokea wimbo wake mpya kwa jina DE JAVU. Akiwasiliana na mwandishi hodari Godwin Wambua wa Pwani Usanii, Otile alikuwa nwenye furaha kusema kuwa amekubalika nyumbani pwani na Kenya nzima kwa jumla na hivi karibuni Afrika mashariki itamtambua vilevile. Kwa sasa wimbo wake wa DEJA VU unatawala chati za muziki wa Kenya. Otile Brown amesajiliwa kwa studio ya DREAMLAND MUSIC chini ya usimamizi wake Dr.Eddie
Comments
Post a Comment