PATA KUMFAHAMU BINGWA WA UTANGAZAJI ROSELYNE KAKINDA.


Roselyne Mnyazi Kakinda wengi wetu twamfahamu tu kupitia sauti yake nyororo ya kuvutia,uchangamfu wake na mawaidha yake yasiyoisha ila bado hatumjui ni nani haswa!
Ndiposa mwanahabari wetu Godwin Wambua alijitwika jukumu la kuwaletea mtangazaji huyu anayetikisa mawimbi ya redio za pwani,Roselyne Mnyazi Kakinda....

Pwani Usanii:Je unaitwa nani majina kamili na una miaka mingapi?
R KAKINDA:Majina kamili Roselyne Mnyazi Kakinda na nina umri wa miaka 25.

Pwani Usanii: Umeolewa?
R Kakinda:Bado sijaolewa na nipo single.

Pwani Usanii: Tupe historia yake kidogo tukujue zaidi..
R Kakinda:Mimi ni Mtoto wa mwisho kwa familia ya watoto 7,ni mchonyi kutoka eneo bunge la Kilifi Kusini wadi ya Mwarakaya eneo la Silala.

Pwani Usanii: Labda kitu gani watu hawafahamu kukuhusu?
R Kakinda:Kitu watu wengi hawafahamu ni kuwa niko na damu ya kitaita…Mamangu anatokea Sagala Teri.

Pwani Usanii: Umesomea wapi?

R Kakinda:Nimesomea shule ya upili ya Chumani Secondary School katika Kaunti ya Kilifi na Nilimaliza kidato cha nne mwaka wa 2008.Mwaka wa 2011 nilijiunga na taasisi ya Mombasa Aviation na kusomea kuwa mwanahabari.

Pwani Usanii: Na ulianza utangazaji baraka FM Lini?

R Kakinda:Nilijiunga na Baraka Fm mwaka 2013 ambapo nilianza kazi kama ripota wa mahakamani ‘Court Reporter’.
Mwaka wa 2014 bado nikiwa ‘Senior Court Reporter’ nilipata pia fursa ya kuanza kufanya kipindi cha Bango maarufu ‘Mdobwedo Reloaded’ hadi sasa kipindi hicho ni siku ya jumapili kuanzia 4pm-8pm.
Mwaka huu wa 2016 mwezi Mei nilianza kufanya Mid Mrng Show kipindi kinachoitwa Mziki Mzuka 10am-1pm.
Hapa nilipo sasa naeza sema ni kwa neema na uwezo wake Maulana….Ni mbali nimetoka na bado safari ni ndefu…

Pwani Usanii: Je changamoto kama zipi unazokumbana nazo katika kazi yako?

R KAKINDA:Kutafuta content ambayo shabiki wako atafurahia kwa sababu siku hizi kila mtu yupo katika mitandao.
Taaluma hii iko na ushindani mkubwa yaani kila mahali kuna radio station sasa lazima kujituma…
Wakati wowote unafaa uwe tayari kwa jambo lolote.
Changamoto zipo na kila siku mambo yanabadilika na Inafaa kujituma sana tena sana.Ila uzuri wake ni kuwa kila siku unajifunza mambo mapya.Kila siku unakumbana na changamoto zinazokukuza zaidi kikazi.Kila siku unakutana na watu tofauti na unajifunza mambo mengi.

Pwani Usanii: Labda una ushauri gani kwa watangazaji wenzako kuhusiana na kazi hii.

R KAKINDA:Endapo unapata fursa kama hii niliyonayo au fursa ya kuwa mtangazaji hakikisha unaitumia vizuri…Usijione umefika kwa sababu wewe ni mtangazaji la hasha… Unafaa uwe tayari kuskiza mkubwa na mdogo.. Pale utakapo koselewa hakikisha unarekebisha na wala usione wale watangazaji chipukizi kuwa hawafai na wewe ndo ‘STAR’.Kazi hii ni sawa na ule msemo unaosema ‘The beautiful ones are not yet born’…. Yaani kila siku wapo watangazaji chipukizi wanaojitosa katika ulingo huu na wanakuja kwa kasi sana hivyo basi ni kukaza buti na kujituma zaidi kwa sababu ukizubaa utachekea chooni.

Pwani Usanii: Je tatizo lipi kubwa linalowakumba watangazaji hasa wale wanaibuka.
R KAKINDA:Tatizo la baadhi yetu tunakuwa na kiburi.Hii haifaii wala haipendezi.Mie Mnyazi husema siezi onyesha mtu madharau kisa na maana mimi presenter aka? Hakuna ajuae hatma ya maisha yangu ila Maulana tu…Leo nasikika redioni kesho sijui itakuwaje?.. Heshimu Yule msikilizaji wako pamoja na wale marafiki zako ambao umekuwa nao tangu kitambo. Ukiwaona mashabiki wako TABASAMU hata kama umechoka kindly fake it but wasikuone m’baya… Cha msingi tusibadilike kisa na maana tumekuwa ‘MAPRESENTER’.Tunafaa tufahamu kuwa hakuna mtangazaji bora ila kila mtangazaji ana ubora wake.


Pwani Usanii: Nani Alikua motisha au inspiration kwenye tasnia hii ya utangazaji?

R KAKINDA:Mimi siendi mbali jamani…..Na si mwingine bali Nzula Makosi Makite.
Jamani nampenda,tena nampenda tena sana. Mimi nimekuwa shabiki wa Nzula tangu akiwa Radio Kaya… Nilikuwa nitafanya kazi zangu zote nyumbani but ikifika 9am am tuned in.
Nakumbuka kuna siku alikuwa amepost status Fulani, nadhani ni wakati alipokuwa amepata kaziMilele Fm na mie nilikuwa bado college nilimwambia she deserves the best na alifurahi sanaaaa…


Pwani Usanii: Je una Advice gani kwa wale wanaotamani utangazaji kama wewe?

R KAKINDA:Kwa wale ambao wanatamani au pia wanasomea taaluma hii mazee ni kujituma.Usisomee taaluma hii kisa na maana wataka kusikika redioni au wataka kuonekana kwa TV si hivyo,kwa sababu kabla usikike au uonekane kwenye TV unapitia vitu vingi sana.Lazima ukuwe na passion katika taaluma hii la sivyo utashindwa njiani.

Pwani Usanii: Una gani la mwisho wa mashabiki zako?

R KAKINDA:Msikose kunitegea kila siku ya juma kuanzia 10-1pm katika kipindi cha Mziki Mzuka Baraka Fm.
Na kwa wale mashabiki wa bango tukutane kila siku ya jumapili kuanzia 4pm-8pm ndani ya Mdobwedo Reloaded.
Vile vile follow me on twitter @MnyaziKakinda IG@MnyaziKakinda fb@MnyaziKakinda

Comments

  1. I love you...your fan number 1

    ReplyDelete
  2. Beautiful mpenzi,hongera sky is your limit

    ReplyDelete
  3. Beautiful mpenzi,hongera sky is your limit

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli katika watangazaji wa redio, nakukubali sana Mnyazi. Huna maringo wala madharau licha ya ww kuwa mtangazaji bora pwani. Kaza boti na uzidi kutufurahisha mashabiki wako. Mungu azidi kukutangulia katika kazi zako za kila siku.

    ReplyDelete
  5. This one of the Best interviews nimehawai kuskia jikaze utafika kilele your my favorite presenter

    ReplyDelete
  6. This one of the Best interviews nimehawai kuskia jikaze utafika kilele your my favorite presenter

    ReplyDelete
  7. Humble in person and in talking.I appreciate the good work your doing educating and entertaining. Keep the good work going.

    ReplyDelete
  8. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  9. Wachonyi twajivunia wakakinda acha Mungu aitwe Mungu.May God continue to bless the works of your hands. An inspiration to me too ..

    ReplyDelete
  10. ��hongera sana kwa kazi yako
    Mungu akujalie uweze kufikia kikomo cha
    Malengo yako��

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!