Produza msanii Lameck Boy wa Neptune records alifunguka mengi kuhusiana na sanaa ya Pwani hapo jana,25th. 7.2017. Lameck Boy aliongea haya baada ya kuona msukosuko flani ndani ya dau hili la muziki wa Pwani. Tukinukuu.... " Sanaa ya Pwani kikweli iko na muziki mzuri,ambao mtu anaweza penda kuusikiliza nakuushabikia,wasanii wako wenye bidii,maproducer wazuri pia,watangazaji pia wazuri wanaosapot muziki.Wako wasanii tajika kama Susumila,Ally B,Nyota Ndogo,Chikuzee,Sudi Boy,Dogo Richie,Fat S,Fisherman,Escobah,Simon Simz na wengine,wako maproducer tajika,nikiwemo,akiwa pia P Baindo,Amz,Emmy Dee,Toti,Noor Mwamba,Tk2,J Crack,Lai,P Lion,Mobiz na wengi ambao tunafanya kazi nzuri. 2;Vitu ambavyo vinaweza au vinarudisha nyuma sanaa ya Pwani ni vitu vitano.... " 1. Wasanii kutopendana,kutofanya kazi pamoja,wasanii kujiona bora kumliko mwengine. 2. Maprodusa pia kukosa kuja pamoja nakushirikiana,wengine kujiona wao ndio wakali kuliko wengine,produsa kujifanya anajua kila kitu,k...