Posts

JUMA SHIBE ASHINDA TUZO ZA PWANI CELEBRITY NA KUAHIDI MASHABIKI KITU!!!

Image
Juma Shibe almaarufu MJ, muigizaji anayetamba kwa kasi baada ya kushinda tuzo za Pwani Celebrity Awards kupitia meneja wake Mjomba Khalfan wa Ukweli aliahidi kuwa kutakuwa na party itakayo andaliwa kusheherekea tuzo ya MJ.Tukinukuu maneno ya meneja wake Khalfan,"Tuna furaha sana kumsheherekea muigizaji wetu hodari Juma Shibe kwa tuzo aliyoipata.Na mengi zaidi yanakuja kwani tayari vipindi na filamu kabambe zimetayarishwa.Vilevile tutawaalika mashabiki nyote kwa party ya ushindi wa Juma Shibe."

DULA AFRICAN SONGBIRD AKUKARIBISHA KIOTANI MWAKE.

Image
Dula ambaye kwa sasa wimbo wake wa TIARA umeshika wimbi la muziki wa pwani ameamua kupanua mbawa zake zaidi.Msanii huyu yupo matayarishoni ya video yake ya muziki ya kwanza kabisa na anatafuta band ya muziki na mabinti 20 ili kuweza kuifanikisha video yenyewe. "Dula is looking for a Band & 20 Ladies to feature in His first Music Video ever... Dula will be shooting His new Song "Bila wewe" Wiki ijayo. For More info: Call +254727649494" Huu ndio ujumbe alioutoa mitandaoni.Kwa hio kama una band ya muziki wasiliana kwa nambari uliyopewa.Bila kusahau mabinti 20 vilevile wanahitajika.

JE WAJUA MSANII WA KIKE MUMMY-D ALIPOTELEA WAPI??? PATA MAJIBU HAPA!!!

Image
Huku wasanii wa kike wakizidi kutokomea hapa pwani. Meza yetu ya habari iliingia chini ya carpet na kutupa habari kuwa Msanii Mummy-D aliyevuma kitambo kidogo aliolewa na msanii French-C Makaps. Msanii French ambaye kwa sasa anatamba kwa kibao chake BADILIKA kilichotayarishwa ndani ya studio za Tee Hits aliwasiliana nasi na kutujulisha kuwa yeye ni mume wake Mummy-D name hivi karibuni wanatarajia mtoto.Vilevile French aliongeza kuwa anayo nyimbo mpya kutoka jikoni studio na ataiwachia hivi karibuni.

PICHA ZA BINTI ALIYEACHIA MKANDA WA NGONO NA DJ CREME ZAVUJA.TAZAMA HAPA!!!

Image
Huku ikiwa bado trending mitandaoni, mkanda wa ngono wa Dj Creme amezua gumzo. Picha hii ni ya mwanadada kwa jina Halima Nassir aliyegwaragazana na Dj Creme.

NILIWAPA NAFASI MKAPUUZA,SASA WACHENI NIFANYE KAZI MUONE MATOKEO-KAULI YA PRODUZA KHALID KWA A MILLION STAR SEARCH.

Image
A Million records chini ya Produza Khalid ukipenda Eric Bizzo ilianzisha tamasha la kutafuta wasanii na baadhi ya watu hasa washika dau wa sanaa hapa pwani walilipinga tamasha vikali.(Nadhani kwa sababu ya wivu). Leo Khalid ameamua kupasua mbarika kuhusu mipango yake ya A MILLION STAR SEARCH............ "Khalid Produza Ati A Million Star Search ilienda wapi? Nilipokuja na idea ya A Million Star Search watu wengi kutoka hapa Mombasa walidharau na kukejeli kama kawaida yao. Kitu hawakujua ni kuwa nilikuwa nimetenga one million shillings za hiyo Star Search. 250k mshindi, 150k wa pili na 100k mshindi wa Tatu. Advert ya radio nililipa 150k ndio ikuwe mentioned everyday, judges walitoka Nairobi na host, wasanii waliokuwa wakiperform kama Dazlah, Sudi, Susumila wote walilipwa. Advert za banners, posters and other logistics zili cost sana. Chenye nilitaka ilikuwa real talent coz I know how to turn talent into money. Wengi mukaanza kejeli mbona nisim sign Sis P Kwanza...

"SIJAWACHA MUZIKI!" EDDYTICHA WA KUNDI LA WATASH APASUA MBARIKA BAADA YA KIMYA KIREFU.

Image
Alivuma miaka michache iliyopita na kupotelea mitini.Akiwa kwa kikosi kilichokuwa na wafuasi wengi,Watash. Eddyticha alifanya collabo na wasanii kama Chikuzee, Captain Lui na Lady Zippi. Chini ya studios za Thundersound kwa producer mkongwe Morbiz, Eddyticha amefanya album kwa jina "Vunja". Kwa sasa ngoma mpya alioachia kwa inafahamika kama "Mapigo ya moyo."

CHANZO CHA KIFO CHA MWANANGU NI MKE WANGU-MSANII ROMEO ADONDOKWA CHOZI.

Image
Ni msanii mwenye utulivu na adiye na tetesi nyingi; Romeo Rnb. Msanii huyu aliyetamba kwa vibao kama 'Nimechoka' alifunga harusi miaka michache iliyopita na ilikuwa mbwembwe, furaha na vifijo mitaa ya Likoni. Baada ya kimya kirefu tetesi zilitamba mitaani kuwa Romeo ana ugomvi wa kinyumbani na mkewe. Migogoro ilifanya ndoa hiyo kuvunjika na Romeo akaarifu wanahabari wetu kuwa mke wake ndiye aliyekuwa chanzo kikuu cha mwanawe kufariki na anasikitika sana kwa kupitia hali ngumu. Romeo aliongeza kuwa watu wasikimbilie kuoa tu kiholela, mambo ya ndoa yataka uvumilivu.