Posts

KAA LA MOTO ANYOOSHA MKONO KUSAIDIA JAMII YA SPRINGS OF HOPE CENTER.

Kuimba tu na kuburudisha hakutoshi ndio usemi mpya wa sanaa ya pwani.Huku Fisherman akimaliza kuwakaribisha wenzake kwa 'TWAAYF KIDS BACK TO SKUL DONATIONS' rapper Kaa la Moto amenakili kwenye ukurasa wake wa Facebook mambo mema aliyokuwa akiwafanyia watoto wa mitaani na wasiojiweza wa Springs Of Hope Watamu.Rapper Kaa La Moto alikuwa na mradi wa HAKUNA CHOKORAA,NI BINADAMU PIA.Tukimnukuu kwenye kurasa zake za facebook Kaa La Moto aliandika haya "As an mcee we do many projects mbali na mziki ...Inafika muda una nyosha mkono kwa Jamii....Msanii ni kioo cha jamii sio kioo cha Jaguar...Asante Mama Nyota Ndogo Kwa yote na harakati tunazofanya...Nikiwa WATAMU the whole week with Street kids at Springs of Hope....Big up kwa the Commitee am wit....Asante Mungu...Project Hakuna Chokoraa ni Binadamu pia ...." Vilevile kutakuwa na mradi wa TWAAYF KIDS BACK TO SKUL DONATIONS jumapili hii tarehe nne kuanzia saa sita Likoni.Nyote mwakaribishwa kusaidia kutoa chochote...

DDI HEMEDI SINGER AZUNGUMZIA KUHUSU VIDEO YAKE MPYA 'USIJALI'.

Image
 Kwa mtindo wake mpya swarnb mkali wa mafleva ya rnb anayeflow kwa lugha ya kiswahili Iddi amekuja wazi kuongelea kuhusu video yake mpya USIJALI.Iddi aliyesajiliwa chini ya Sandstone Studios ya Ted Josiah amefanya vyema kwa ubunifu wake wa hali ya juu na kweli ameteka nyoyo za mashabiki wengi.Tuliwasiliana naye ili aweze kutueleze zaidi kuhusu video yake mpya na alikuwa na haya ya kunena...... "Usijali..is a swarnb song..its all about this insecure "girlfriend" of mine who thinks that i cheat or go out with other women just because am an artist.So the song tell her not to worry about a thing, she's the only one i have..and it's on behalf of my fellow artists who have the kind of problem in life..and anyone else out there who feels like that..to wrap it up 'insecurity' is the theme"   Huku akiisifu video yake, Hustla Jay ambaye pia amesajiliwa kwa studio za Sandstone studios alimpa support mwenzake huku akimsheherekea kama msanii bor...

WASANII WA KIKE WA PWANI WAZUNGUMZIA KUHUSU SHERIA MPYA YA NDOA NA KUOA.

Image
Ni Juzi tu Rais Uhuru alitia sahihi mswada wa kuoa bibi zaidi ya mmoja na leo wasanii wa kike wa pwani wamevunja mbarika na kuzungumzia jambo hilo. NYOTA NDOGO alikuwa na haya ya kunena..."sasa wanawake ndio watakao tafuta mpango wa kando kwa bidii.mume moja wake wanne?ukija kwangu umechoka kama nini hujiwezi.mume anaitaji mapumziko.haya akiwa na hawa wanne watapumzikaje?ndio kuridhisha wengine wengine kupata makombo yasio watosha.mpango wa kando." Naye SIS P hakusita kuöngeza chumvi na kunena hivi...."hehe ati polygamy is now legal in kenya.. mimi bwanangu akiongeza bibi mimi pia naongeza bwana na we be equal".Je wewe maoni yako ni yapi?

GROOVE AWARDS, NANI ALIYEPATA NOMINATIONS?

Image
PWANI SONG OF THE YEAR • Ahadi Za Bwana - Pst. Anthony Musembi • Bwana Wa Mabwana -Princess Farida • Milele - Marion Shako • Mwaminifu - Kristine Ndela Ft. Rozina • Nisamehe - Mercy D Lai • Tam Tam - Masha Mapenzi vile vile, Msanii Mecry D Lai aliweza kupata Nominations mbili kwenye Female Artiste of the Year na pia kwenye Album of The year, (Nisamehe)

WILBERFORCE WA HEARTBEAT ASHEREHEKEA BIRTHDAY YA MPENZIWE KWA NJIA SPECIAL!!!

Image
Promoter gwiji na muandalizi tamasha mashuhuri pwani, Wilberforce Mwikya wa Heartbeart entertainment leo hii ana furaha ya kukata na shoka pale anaposheherekea birthday ya bibi yake. Wilberforce aliweka picha ya binti huyu mzuri kwenye ukurasa wake wa facebook na kutangazia ulimwengu uzito wa penzi lake kwake.Wilberforce Jeff Mwikya Dah! .Binti huyo kwa jina Juliet Mkube hufanya kazi Coast Bus Mombasa office na yupo na miaka 23. Party ya sherehe hiyo ya birthday itafanyika Southcoast, Diani pale Jacaranda hotel. Vilevile promoter huyu amevunja ukimya wake na kutufahamisha kuwa amefungua pub kadhaa katika maeneo ya Majengo mapya Likoni, na punde atarudi kwenye ulingo wa uandalizi wa tamasha za burudani.

SHAMANIZ CONTRACT SAGA: PRODUZA KHALID ASEMA MAISHA YAKE YAPO HATARINI.

Image
 Tukinukuu kutoka kwa ukurasa wake wa facebook "NAHISI MAISHA YANGU YAPO HATARINI. Jana asubuhi kama nilivyosema, nilienda kwa lawyer nikafungua file kuhusu mzozo uliopo baina ya Shamaniz na A Million Records. kisha lawyer akaandika barua mbili, moja kwa shamaniz kumkumbusha kuwa ana mkataba na hafai kuuvunja kiholela, pili ikawa ya producer Totti kumjulisha kuwa kuna mzozo unao endelea kwa hivyo hapaswi kuachilia huo wimbo waliorekodi shamaniz na chikuzee mpaka waniandikie barua rasmi na kunijulisha ni asilimia ngapi Shamaniz na mimi tutapata endapo nyimbo hiyo itachezwa kwa radio na tv na hata pia downloads. Leo mwendo wa saa saba na dakika 25,nilipata simu kutoka kwa Musa Babaz. Nikimnukuu haya ndiyo aliyosema.kadri akiongea langu lilikuwa kumwambia "endelea nakuskiza" wala sijajibishana naye. Alisema hivi..........."Wacha nikueleze kitu kimoja,i le process unaendelea nayo, endelea tu na hiyo process tuone nani atafikisha mwengine kwa ukuta. Fany...

FISHERMAN : TUSAIDIE JAMII NA NAWAKARIBISHA JUMAPILI KWA EVENT YA TWAAYF CHILDREN CENTER .

Image
Mkali wa dancehall na ragga pwani na Afrika Mashariki kwa jumla, Fisherman amekuja wazi na kujitolea kutoa msaada wa BACK TO SCHOOL kwa watoto ya Twaayf orphanage. Fisherman aliyesajiliwa kwenye studio za Grandpa recordz ametueleza kuwa atakuwepo siku ya Jumapili ya tarehe nne ili aweze jumuika na watoto wanapojitayarisha kurudi shule.Vilevile msanii huyu anayevuma kwa kibao chizika akimshirikisha JO-1 amewakaribisha washika dau wa sanaa ya pwani na yeyote yule aliye na uwezo ajitokeze TWAAYF CHILDREN CENTER LIKONI ili aweze toa mchango wake wa BACK TO SCHOOL.