JAMII YA WAIGIZAJI WA PWANI;COLLYWOOD YAOMBA KUTAMBULIKA KWENYE TUZO
Waigizaji toka mkoa wa pwani wamejitokeza na kuvunja ukimya wao. Kama vile Hollywood, Bollywood,Nollywood,Tollywood Machawood, sasa wapwani nao hawawachwi nyuma. Jamii ya waigizaji ya wapwani almaarufu COLLYWOOD imekuja bayana kutangaza msimamo, maudhui na malalamishi yao. COLLYWOOD inataka kupewa tuzo au kutambulika kwenye tuzo zozote za pwani na Kenya nzima kwa jumla.Vipindi vya kukata na shoka vinavyotambulika kwa sasa ni kama MOMBASATI kwa QTV,SAIDA kwa CITIZEN TV na AROSTO kwa K24 TV. COLLYWOOD walikuwa na haya ya kunena........"Mwaka huu ingekuwa sawa kama nzumari na Coast music awards waanzishe kitengo cha tuzo la actors, actress ,directors na wengine wanahusika na mambo ya filamu......"