Posts

Showing posts from December, 2016

PWANI USANII ONLINE RADIO. LISTEN HERE!!!

Image
PWANI USANII ONLINE RADIO FEATURING NASSIZU MURUME,IDDI SINGER,NEPTUNE RECORDS, WYNAS,BABLUE AKA ANTONIO LISTEN HERE - >> https://www.spreaker.com/user/9366849/pwani-usanii-online-radio-featuring-nass SEND US YOUR MUSIC THROUGH pwanimusiknewsgodwinpwani@gmail.com or contact us through 0723 936960 for at enquiries. We also do adverts.

UIMBAJI NA UCHORAJI NDICHO KIPENZI CHA MSANII J'S.

Image
UIMBAJI NA UCHORAJI NDICHO KIPENZI CHA MSANII J'S. Ama kweli Mungu hutujalia kwa vipawa tofauti tofauti ila kwa Joseph Ngila,Mungu amemjalia vipaji viwili ambayo vyote anavitumia kujifunufaisha na kuelimisha jamii. Joseph Ngila Ngonzi almaarufu J'S ni mzawa wa papa hapa Mombasa eneo la Changamwe Soweto kisumu ndogo. Uchoraji wake na uimbaji ulianzia shule ya msingi ya Mwijabu. Kwa umri mdogo sana,J'S aliwashangaza wengi kwa kuchora picha zenye mvuto zilizompelekea yeye kuwa kipenzi cha walimu,akiwasaidia kuchora chati na mabango ya shule. Tukija kwa kipaji chake cha uimbaji,J'S alikuwa na haya ya kueleza....... "Nilianza kuimba nikiwa na miaka kumi na mbili ila utunzi wa nyimbo nilianza mwaka wa 2000.Niliupenda muziki jambo lililopelekea mimi kuunda kundi Langu la muziki lililojulikana kamaJ.E aka Joseric." Kwa sasa msanii J'S yupo na ujio mpya kabisa chini ya Bullet music na ataiwachilia nyimbo hiyo hibi karibuni. Nyimbo yenyewe inajulikana k...

DULLY MELODY AMPONGEZA DIRECTOR WA VIDEO YAKE YA KIVUMBI.

Image
Video Director:Thomas. DULLY MELODY AMPONGEZA DIRECTOR WA VIDEO YAKE YA KIVUMBI. Supasta anayechipukia kwa kasi, Dully Melody amekuja wazi na kumpongeza mwandalizi wa video ya wimbo wake 'KIVUMBI' Dully, alimpongeza sana director Thomas Tomsy anayetokea Nakuru na akasema kuwa jamaa huyo ni mwenye moyo mzuri wa kusaidia na kukuza vipaji. "Sio kwamba eti pwani hakuna waandalizi wazuri wa video,wapo wengi sana ila nilipendelea kufanya kazi na director Thomas kwa kuwa Thomas alianza kunifuatilia mimi kama msanii pindi tu aliposikia nyimbo yangu ya kwanza hongera.Japo yupo Nakuru,amekua akinipa motisha na hata kusambaza muziki wangu sana ndiposa nikaona nifanye kazi naye na vilevile kwa sababu Thomas yupo Nakuru na mimi nipo Pwani basi ni kama tutakuwa tukeshika Kenya nzima kwa ushirikiano wetu kutoka magatuzi tofauti."Alitusimulia Dully. Video ya Kivumbi ambapo Dully amemshirikisha rapper wa kike CML tayari ishakamilishwa uandalizi na hivi karibuni basi itawach...

NASSIZU MURUME AWACHILIA MAWAZO

Image
Baada ya kuwa signed na label ya Watanashati Classics, msanii Nassizu Murume ameachilia kibao kingine kwa jina Mawazo. Nassizu ambaye tayari ameachilia nyimbo kadhaa ikiwemo Sindi, amekuwa aking'ara hasa baada ya kazi zake kupokelewa vyema  na media. Watanashati Classics ndio kampuni iliyoandaa show ya Diamond Platnumz miezi kadhaa iliyopita, huko Meru. Tazama video yenyewe hapa

CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WASANII WA LAMU.

Image
Wengi Wetu tunausikia mji wa Lamu kwa utajiri wake wa kitalii na tamaduni za kiswazi ila hatujui kwamba wapo wasanii wa kizazi kipya wanaofanya muziki kwa bidii. Tulijaribu kuwasiliana na baadhi ya wasanii wanaotokea Lamu na walikua na mengi ya kutueleza kuhusu kufanya muziki Lamu. Kikosi cha IslandLove records kikiongozwa na meneja wao kwa jina Enoch,walituwekea mambo bayana. Man Azzer na producer Doni ambaye vilevile ni msanii walipasua mbarika na kusema kuwa wasanii wa Lamu hawadhaminiwi na kuheshimiwa kama wenzao wa Mombasa. "Kaunti yetu ya Lamu haithamini kazi za wasanii wa kizazi kipya. Katika tamasha za viongozi wa serikali au wanasiasa hatuitwi wala kupata hata mualiko wa kutuimbuiza na kuonyesha vipaji vyetu." Alieleza Man Azzer. Vilevile Produza Doni aliongezea kuwa vituo vya redio vya pwani vimewatenga sana wasanii wa Lamu. Doni alikua na haya ya kusema kuhusiana na swala la redio......" Stesheni za pwani zimewakandamiza sana wasanii wa Lamu na La...

LA TUKUL KUACHIA KIBAO KIPYA: ZUNGUSHA

Image
Msanii anayechipukia kwa sanaa,La Tukul ameamua kuwaonjesha mashabiki wa muziki utamu wake kabla mwaka uishe. Msanii huyu ameamua liwe liwalo hadi raundi hii apige bao kisanaa. Kibao chake "zungusha" tayari kishaiva toka studio za Thundersound chini ya Produza Morbiz. Pindi tu mambo yakiwa tayari basi,wimbo zungusha mtaupata kwenye akaunti za mdundo,YouTube na nyinginezo.

ALIKIBA SIO KAKANGU ! MSANII AFUNGUKA.

Image
ALIKIBA SIO KAKANGU ! MSANII AFUNGUKA. Baada ya kutambulika kwenye road show ya Meru iliyoongozwa na comedian Churchill,msanii Nassizu Murume aliyesajiliwa na lebo ya Watanashati classic entertainment amekuja wazi na kukana madai yanayosambaa mitandaoni kuwa yeye ni kakaye msanii wa Bongo,Alikiba. Habari hizi zilipamba moto hasa pale video ya wimbo wake 'mawazo' ilipodondoshwa na wengi walidhani ni nduguye Alikiba.Unapotazama video mawazo ya msanii huyu basi bila shaka utamfananisha na Alikiba kwani kisura na sauti wameona vilivyo.Tulipata kuwasiliana na meneja wa lebo ya Watanashati classic entertainment kuhusiana na swala zima la msanii wake kuitwa nduguye Alikiba.Alikuwa na haya ya kunena........ "Wengi wamekuwa wakimfananisha na Alikiba na walidhani ni kakake ila msanii wetu Nassizu anapinga na kusema hana uhusiano wowote na Kiba ila urafiki wa karibu tu. Kwa sasa kazi zake zinafanywa chini ya Watanashati classic." PATA KUITAZAMA VIDEO YAKE YA "MAW...