KUTOKA MOMBASA HADI DUNIA NZIMA. MSANII JEY AWAKILISHA BENDERA YA KENYA!

KUTOKA MOMBASA HADI DUNIA NZIMA. MSANII JEY AWAKILISHA BENDERA YA KENYA!

Juma Seif alianza muziki mwaka wa 2005 town moja yaitwa Blackpool. Wimbo wake wa kwanza ulikua unaitwa "Cool charlie" na aliurekodi yeye pamoja na kikosi chake kwa jina G-lADS.

"Producer hapo alikua ni Hassan wa tabasam records ila siku hiyo alikua university Manchester tukaenda hapo kwa room shuleni akaturecod.Tukaendelea na kikosi chetu kikawa kikubwa paka Nchi jirani ya Tanzania tukaungana na vijana kutoka Temeke na mimi na machizi wangu wa Bombolulu." Alidokeza JEY.

Baada ya miaka kama miwili hivi kundi lake la muziki lilisambaratika.Jey hakufa moyo bali aliendelea kulisukuma gurudumu la sanaa hadi alipopata chance na kupiga collabo na Susumila."Tukafanya mikakati na Susumila, hivyo basi nikaja Kenya manake wakati huo nilikua nimesafiri ng'ambo kwa minajili ya kazi."
Baada ya Kufanya kazi na Susumila ambayo ilitoka vyema kabisa,Jey aliachia kibao motomoto kwa jina "busy".
Mambo ya muziki yalinigandama sana hata nikaamua kujifunza kuwa producer .Nilianza kutengeza beat mwenyewe,Wimbo wangu "busy" nikafanya remix jamaa wa bongo anaitwa Snake ambao kila kitu nilitayarisha mwenyewe.' Alieleza JEY.

Jey alilirudisha kundi lake la G-IADS na kufanya nao nyimbo kadha wa kadha.
Baada ya hapo,JEY alirudi na kwanza kufanya solo projects hasa kuhusu mambo ya madawa ya kulevya.Msanii huyu alifululiza na kolabo kadhaa wa kadhaa na wasanii ka Dogo Richie,Wazobaba,Dazlah na wengineo.
Wimbo wake na Dazlah kwa jina UTANIPENDA umetayarishwa ndani ya Tee hits Records na hivi karibuni atauwachia hewani.

https://youtu.be/QWbg4ZD-gS0

Comments

Popular posts from this blog

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.

MKISEMA WAREMBO HAWAJAZAWA....TAZAMENI PICHA ZA VIDEO HII INAYOKUJA!!!