Posts

BARUA WAZI KWA RAPPER KAA LA MOTO!!!

Image
Baada ya mitandao kuzua kwamba rapper gwiji wa hapa pwani Kaa La Moto Kiumbe ameenda breki kimuziki; Anita Santuri ambaye ni CEO wa tuzo za Pwani Celebrity Awards ameamua kumuandikia barua rapper huyo. Anita ambaye vilevile ni mtangazaji saidia wa Mseto EastAfrika alikua mwingi wa maneno huku akimueleza Kaa La Moto vile anavyomthamini kimuziki.

WASANII WOTE WA PWANI MNAPASWA KWENDA NGUMBARU ISIPOKUWA CASH ERA!!! SOMA HAPA UPATE UHONDO!!!!

Image
Chambilecho wahenga,palipo na ukweli uongo hujitenga.Hivyo basi tukipasua mbarika na kuumwaga mtama penye kuku wengi; kinachojiri ni kuwa wasanii wa pwani wanapaswa kwenda ngumbaru wote isipokua msanii Cashera.Choko choko hii ya kumchokoa pweza ni chapisho la mtandao wa blogi moja kwa jina THE EVENING POST. Blogi hiyo ilichapisha nyaraka zake za mitandao na kuwadhalilisha wasanii wa pwani kuwa sio wasomi kabisa na wanapaswa kwenda ngumbaru. Ila msanii aliyewachwa kwa listi ni Cashera ambaye ni msomi kama walivyodai waandishi hao. Cashera ambaye yupo na ujio mpya kwa jina CHIJEGO alisifiwa sana kwa shahada mbali mbali alizopata kutoka kwa vyuo tajika nchini. CHEKI SNAPSHOT ZA EVENING POST.......USIJE UKASEMA 'TWAWAONEA!!!'

ONE ON ONE WITH THE NEW SOUND IN TOWN:ANTONIO KARANI!!!!

Image
Pwani Usanii:Whats your  real name and what name do use on stage? Antonio: My real name is Antonio Karani and Antonio is my stage name. PU: What genre of music do you do? Antonio: I do afrofusion and rnb,sometimes dancehall. PU:How and when did you start music? Antonio:I have always been interested in music but the real thing and ambition started in highskul as a song writer and singer. PU:Nice,and when did you start recording your music? Antonio: I started recording immediately after highskul in 2014,where in college I met a music oriented guy and a producer called Sharpy who had set up a recording equipment in the hostel.He introduced me to recording and commercial music.Since then I've taken serious interest in music as a passion. PU:Which music producers have you worked with so far? Antonio: I've been working hard trying to find my sound by working with different producers starting with my home studio Crack sounds in kilifonia with J Crack. Then to Cha...

VICHAPO KUMI VYA PWANI: TOP TEN MUSIC

Image
1.Ting go - Frankie Dee 2.Nitalia-Dazlah 2.Niende-Kigoto & Iddi Singer 4.Alivyonipenda-Otile Brown ft King Kaka 5.Source- Dully Melody 6.Naringa naye-Chikuzee ft Cassim Mganga 7.Niambie-Gaspery & Kaa la Moto 8.Goodmorning-Babudee Mapete 9.Yakatobina-Jaffarizoh 10.Wako wapi- Jaykah ft Kimbo

SASA HAWA NDIO WALIOTEULIWA KAMA BEST DRESSED CELEBRITIES PWANI!!!!

Image
Wakati umefikia wa Pwani Fashion Awards ambayo baadhi ya walioteuliwa kuwania BEST DRESSED CELEBRITY hapa pwani ukiwa hivi: BEST DRESSED CELEBRITY 1. DJ LENIUM-PFWA22 2. DAZLAH KIDUCHE-PFWA23 3. JAMAL GADDAFI-PFWA24 4. VIVONCE-PFWA25 5. ANITA SANTURI-PFWA26

HAWA NI WASANII NINAOWAFAGILIA ZAIDI PWANI!!! ALI MANZU WA KTN ASEMA NA PWANI USANII!!!

Image
Ni mwanahabari sifika na tajika Kenya nzima,muite Ali Manzu.Manzu anayefanya kazi ya uanahabari kwenye runinga ya KTN ya shirika la standard alipiga gumzo na mwandishi wetu hodari,Godwin Wambua na alipasua mbarika kuhusiana na wasanii anaowapenda zaidi hapa pwani. GODWIN WA PWANI USANII: Ali Manzu wewe ni wa asili ya kipwani na umelelewa kuku huku pwani.Leo nataka utuambie,ni msanii au wasanii wapi unaowafagilia sana hapa pwani? ALI MANZU:Shwari kabisa.Wasanii ninaowakubali pwani ni hawa Iddi Singer namkubali sana Kaa la Moto kisha Ukoo flani bado ni miti kwangu. IDDI SINGER KAA LA MOTO UKOO FLANI

NAPENDA NGONO SANA KAENI MKIJUA HIVYO!!!! MSANII TAJIKA PWANI AFUNGUKA!!!

Image
Msanii Kigoto Mmbonde,ameamua kuyaweka wazi.Baada ya kufuatwa na mashangingi na mabinti kadha wa kadha kwenye mitandao hasa ya fesibuku na whatssap,msanii huyu ameamua kuwaambia ukweli wake.Kigoto anayevuma kwa kibao chake kipya NIENDE alichoshirikiana na Iddi Singer aliyasema haya ili kuwakaribisha wanawake wote wanaompenda. "Kama kuna msichana yeyote anayevutiwa na Mimi basi akae akijua akija kwangu ngono lazima na kumuonja lazima.Wajua watu siku hizi wanajidai sana eti kufichaficha siri zao ilhali wanapenda mambo hayo.Afadhali tuambiane ukweli ndiposa Mimi nimesema napenda ngono na sioni lolote la ajabu wala aibu." Alieleza Kigoto. Baada ya kutoa video ya Hello Hello iliyoshika kwa sana tu,jamaa huyu ameachia kichapo kingine kwa Produza wake TK2 na kibao hiki NIENDE sio tu kikali bali ujumbe unaowasiloshwa pia ni mzito ajabu!!!