Posts

TAZAMA BEHIND THE SCENES YA VIDEO YA "BILA WEWE" YA DULA THE AFRICAN SONGBIRD.

Image
Anaitwa Triple A au ukipenda Dula the African Songbird na chini ya A million videos ya Khalid produza ameandaa video ya wimbo wake BILA WEWE.Video hii atakayo iwachia 3rd December itasumbua sana.Cheki behind the scenes hapa.

"INTERCONTINENTAL SCAR" YA HUSTLA JAY YAPATA TEULIWA KWA TUZO ZA KIMATAIFA ZA FRANCE.

Image
Tulimsikia kwa Mara ya kwanza kwa kibao MINYORORO YA HAKI iliyoshika chati sana na kufanya mapinduzi kwenye sanaa ya Afrika Mashariki. Hustla aliye na hulka ya kuifundisha jamii kwa kupigania haki kupitia muziki wake ameteuliwa kuwania tuzo fulani ambapo video yake imechaguliwa katika kipengele kimoja kwenye tuzo hizo.  Kumpigia kura Send the number " 2 " on email finale@lereveafricain.com / 1 email address = 1 vote

FYATENI NDIMI ZENU WANAHIPHOP WA PWANI WANAOJISHASHA FACEBOOK. TAZAMENI RAPPER MKALI WA FASTCASHMUSIC GROUP ANAVYOMWAGA MICHUZI!!!!

Image
 Huwa wafokaji wa pwani hupenda kupiga kelele mitandaoni jinsi walivyo wakali na muziki wao unvyotamba.Kumbe zote huwa kelele tu ila hakuna kazi yoyote inayofanyika. Ndiposa wakati mwingine inapaswa turudi chini na kunyenyekea na kuwa wakweli. Sio kujisifu na kukashifu presenters kuwa hawachezi miziki na nyimbo zenu mpya ilhali bado mnatapatapa na kuandaa vitu borohoa. Hivyo basi, tazameni mwanahiphop kwa jina KRG ceo wa FASTCASHMUSICGROUP anayetokea Nairobi anavyovuja mkwanja.  Jamaa huyo alimnunulia demu wake bonge la gari baada ya kumrushia Party.  Cha msingi ni STAY HUMBLE ALWAYS.

MAHABUBA ISHAPIKWA IKAPAKULIWA! TAZAMA VIDEO YOTE HAPA!!

Image
Imekuwa midomoni mwa watu na imetrend mitandaoni kwa sana tu. Ila Leo lazima kieleweke...Tunazungumzia video ya Mswazzi Masauti "Mahabuba." Produza Tedd Josiah amewatoa wasanii wengi tu na hapa hajacheza karata zake vibaya. Mahabuba, video iliyochukua siku sita ikiandaliwa sehemu tofauti huku pwani lazima itasumbua sana sio kwa runinga, radio, mitandaoni hadi mitaani. Mswazzi Masauti amejaribu kuweka fleva za kimwambao kwenye mdundo tulivu wa rnb uliokolea nyuzi za gita na sauti tamu za vinanda. Video maridhawa yenye mvuto mzuri na rangi za kupendeza zilizooana vyema na ujumbe unaopitishwa imeleta dhana nzuri kwa mada ya mahaba inayozungumziwa. Tusitumie mate ilhali wino upo.......video yenyewe hii hapa.Tazama kisha utoe maoni--------

HIVI HUYU "KUNGURU MWEUSI" NI NANI?????

Image
Chikuku Abdhalla almaarufu Chikuzee aliyesikika kwa Mara ya kwanza ndani ya Thundersounds records chini ya producer Morbiz aka Sherif ameamua kuwachia kibao kipya kuongelea mtu fulani.Chikuzee kweƱye wimbo wake mpya KUNGURU MWEUSI ameongea kimafumbo kumsuta mtu fulani.Hivi swali ni huyu kunguru mweusi chikuzee anayemuimba ni nani?

LOO!!! MSANII KUTOKA KAUNTI YA KWALE AMUUZA MKEWE KWA SHILINGI 500KSH.

Image
MSANII TOKEA PAPA HAPA PWANI MAENEO YA KWALE ALIMUUZA MKEWE KWA SHILINGI 500 PEKEE.TUKIO HILI LA KUTAMAUSHA LILIWASHANGAZA WENGI KWANI WAWILI HAO WALIKUA WAMEOANA KWA MIAKA MINNE.MSANII HUYO KWA JINA MWACHAMBULI SARIA ALIMPIGA BEI MKEWE ANAYEJULIKANA KAMA ADA KASSIM KWA RAFIKIYE BAADA YA NDOA YAO KUINGIA DOA. ZAITWA KUKURU KAKARA ZA SANAA YA PWANI. Picha kwa Hisani ya #TaifaLeo 

CHANGEZ NDZAI AIKABILI SANAA YA PWANI VILIVYO.

Image
Msanii Changez Ndzai, ambaye kwa wengi wanamfahamu kwa uandishi wake wa mashairi na pia hivi majuzi aliachia kibao chake cha kwanza kwa jina ''Msaada'', ameamua kuchukua hatua madhubuti ilikuona anapanda katika ngazi za juu kwenye sanaa. Changez amekua akitembea kutafuta Shows Malindi hapa Mombasa na Kilifi. Akielezea meza yetu ya habari kwanini amekua akipeana shows kipao mbele kuliko radio airplay, Changez amehoji mashabiki wa kweli wako kwenye hizi show. Alisistiza kuwa shows mbali nakuumpa msanii kipato zinampa msanii twaswira kamili kama kweli anafaa ama hafai, kwake yeye anasema ameshangazwa sana na mashabiki vile wanavyo mshobokea kazi zake tokea spokenword hata nyimbo.