KIPINDI CHA TOP MASHARIKI-KBC CHAZIDI KUFANYIWA LAUNCHING KALI!!!!!
Kikijivunia kuwa mizizi ya muziki wa kizazi kipya cha Afrika Mashariki, Top Mashariki kipindi kinachoendeshwa na Mwinyi Mtetezi Kazungu akisaidiana na Caroline Mramba kimezidi nawiri. Sio kwa radio pekee bali hadi kwenye runinga zote, wasanii wa Afrika Mashariki wamepewa kipao mbele kwa jukwaa maridhawa la kukuza vipaji vyao na kuelimisha jamii. Top Mashariki inafanya uzinduzi mdogo wa 2016 utakaowaleta wasanii gwiji pamoja na wanaochipuka pamoja. Uzinduzi huu utafanyika Jumapili tarehe 17 mwezi huu ndani ya 1 Club Kimathi street. Kuelewa zaidi kuhusu uzinduzi, Mwaka jana kulikuwa na uzinduzi wa kipindi cha radio ambapo mambo yalikuwa bomba sana. Wasanii walikuwa kibao sana tena wanaosifika Afrika Mashariki. Uzinduzi huu wa kipindi cha runinga unaleta pamoja wasanii kwote nchini ikizingatiwa Top Mashariki ndio show inayocheza kila msani katika pembe ya Kenya. Mwinyi Kazungu alikuwa na haya ya kunena........"Ningependa kuwajulisha watazamaji wa KBC Channel One huu ni uzinduzi mdogo lakini mkubwa upo njiani hivi karibuni. Mengi yapo njiani. Kwenye uzinduzi huu nimejitolea kuwapatia wataojitokeza kusheherekea kwa kula mbuzi, vyakula na vinywaji."
Comments
Post a Comment