Posts

Showing posts from January, 2016

NATUMIA HELA YANGU MWENYEWE. DAZLAH AKANA KUMTEGEMEA LIZZ JAHSOLJA!!!!

Image
Huku ufanisi wake kimuziki ukizidi kufana, kidekide master almaarufu Dazlah Kiduche amejitokeza kupiga duster mambo flani. Dazlah aliye chini ya promoter na mfanyibiashara Lizz Jahsolja kupitia gazeti la People Daily , amekana madai ya kuwa uhusiano wake na Lizz ni wa kufadiana kihela.  Msanii huyu aliongeza kuwa japo kuna mahaba kati yao, uhusiano wao ni wa kimuziki na biashara zinazooana na muziki. Kando na hayo Dazlah ameonekana sehemu kibao na Dada huyu wakivuja hela kuwa starehe za kigharama ajabu.

AKOTHEE AKAMILISHA KAZI YAKE MPYA NA DIAMOND. Tazama Trailer yake hapa

Image
Ni binti aliyejaa hamu ya muziki na aliamua kutumia juhudi zake zote ili kutamba kimuziki. Si mwingine bali Akothee . Alianza kwa Produza Totti na kuzidi kupanda kwenye chati za muziki hasa za hapa Pwani. Bila kutazama nyuma, alizidi kutamba na kwa sasa ameandaa video moja kali akimshirikisha Diamond Platnumz . Video hiyo iliandaliwa na Godfather production. Tazama kionjo hapa  ===>

KIPINDI CHA TOP MASHARIKI-KBC CHAZIDI KUFANYIWA LAUNCHING KALI!!!!!

Image
Kikijivunia kuwa mizizi ya muziki wa kizazi kipya cha Afrika Mashariki, Top Mashariki kipindi kinachoendeshwa na Mwinyi Mtetezi Kazungu akisaidiana na Caroline Mramba kimezidi nawiri. Sio kwa radio pekee bali hadi kwenye runinga zote, wasanii wa Afrika Mashariki wamepewa kipao mbele kwa jukwaa maridhawa la kukuza vipaji vyao na kuelimisha jamii. Top Mashariki inafanya uzinduzi mdogo wa 2016 utakaowaleta wasanii gwiji pamoja na wanaochipuka pamoja. Uzinduzi huu utafanyika Jumapili tarehe 17 mwezi huu ndani ya 1 Club Kimathi street. Kuelewa zaidi kuhusu uzinduzi, Mwaka jana kulikuwa na uzinduzi wa kipindi cha radio ambapo mambo yalikuwa bomba sana. Wasanii walikuwa kibao sana tena wanaosifika Afrika Mashariki. Uzinduzi huu wa kipindi cha runinga unaleta pamoja wasanii kwote nchini ikizingatiwa Top Mashariki ndio show inayocheza kila msani katika pembe ya Kenya. Mwinyi Kazungu alikuwa na haya ya kunena....... ."Ningependa kuwajulisha watazamaji wa KBC  Channel ...

COLONEL MUSTAFA AKIONA VIDEO HII ATAJUA KUWA WASANII WA MALINDI NI VICHWA VIBOV!!!!

Image
Waaaaahhh basi mwaka huu Malindi imeamua kutolala. Chini ya Malindi Records msanii Kiwanja akimshirikisha K-Mode wametoa video moja chafu sana na kali zaidi ya video zote zilizowahi tolewa Kenya hii. Video hii ikionyesha watu waliotupu tupu wenyewe wanasema imejaribu kuleta dhana ya kisanii. Ikiwa imetayarishwa na Producer Sango video ya HATARI niya kipekee; kwa rangi za black and white wasanii hawa wametoa ujumbe fiche na ukitazama kwa macho ya kisanii basi bila shaka utajua jamaa hawa wa Malindi records walikua na ujumbe fiche wanapitisha. Itazame hapa------->  Warning: the video contains scenes not appropriate for persons under the age of 18. THIS VIDEO CONTAINS PARTIAL FEMALE NUDITY IN AN ARTISTIC CONTEXT >>>>>> http://youtu.be/Fb2ghpTBDzw  

NATAKA MWAKA HUU UWE KAMA 2015-SUSUMILA ASEMA.

Image
Ndio mwaka umen'goa nanga na Susumila ashatoa neno lake tayari. Jamaa huyu aliyetoa zaidi ya hit songs tano mwaka uliopita aliongea na jarida la mwanaspoti na kudai kuwa scandals za 2015 zilimpa motisha sana na kumfanya afanye kazi zaidi. Kwa hiyo Susumila alipendezwa sana na scandals hizo kwani ndizo zilizomfanya kutoa vibao vikali zaidi kimoja baada ya kingine.

"KAZI YAKO NI KUIMBA QASWIDA. OTILE BROWN HUMWEZI MASAUTI!" - RAPPER KASSAMONEY APASUA MBARIKA.

Image
Tushamzoea rapper Kassamoney kuwa mbishi na mkosoaji kwa kila linalomkera. Hapa basi ameuanza mwaka kwa fujo tele kwani baada ya kumgoa msanii Lil Felly ameamua kuchukua upande wake kwenye kukuru kakara za Otile-Mswazi. Kassamoney aliyeachia video yake ya TUKO TARA hivi majuzi alikuwa mwingi wa maneno akimkosoa Otile Brown akimwambia kuwa hajui kuimba lolote isipokua QASWIDA. Rapper hu yu mbishi alikuwa na haya ya kupitisha.......... "Let me set Things Right Do not believe in Hype ‪#‎ Otile_Brown‬ Unafanya ‪#‎ Qaswida‬ of whch ndo uko Best at... Hyo Dejavu ni qaswida type of music if im nt wrong.. So dnt brag a bout it Its Only in Kenya Where Media na fans wanakuwa foold na Vitu ndogo ndogo kama izo... Walio kusigne Walibabaika, ‪#‎ Ghafla_Kenya‬ nao vile Vile Wakababaika A bout it.. ‪#‎ radios‬ and ‪#‎ Tvs‬ Wanababaika a bout it You Can nevr be better than ‪#‎ Masauti‬ better than ‪#‎ Brown_Mauzo‬ Better than ‪#‎ IDDY_SINGER‬ Yall do diff styles Kenyan...

LAMINI 3 NDIO WASANII CHIPUKIZI WA KWANZA KUTOKA MOMBASA KUFANYA COLLABO NA NEY WA MITEGO!!!!!

Image
Baada ya kupiga bonge moja la collabo na Barnaba ndani ya C91 Studios,kundi la Lamini 3 likiongozwa na msanii Chris Micky limeamua kutorudi nyuma.Lamini 3 linalotokea pwani ya Kenya,Mombasa lilifunga safari kuelekea bongo kufanya kazi na msanii Ney wa Mitego.Hii ndiyo Mara ya kwanza msanii Ney Wa Mitego kufanya kazi na wasanii wa Mombasa.Meza yetu ya habari iliwasiliana na kiongozi wa kundi hilo Chris na alikuwa na haya ya kunena, "Tunaukubali sana mtindo wa muziki anaoufanya Ney ndiposa tukazama bongo kufanya naye kazi.Ney ni msanii mzuri na kufanya naue kazi ilikua chance moja ambayo hatuyawahi isahau.Nyimbo yetu bado ipo jikoni inaandaliwa na hivi karibuni tutaiachia hewani." Vilevile wasanii hawa wana nyimbo yao kwa jina DANCE itakayo achiliwa hewani wakati wowote.