WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA
Mwanamuziki tokea pwani ya Kenya,P-day ametoa kauli yake kuhusiana na matukio ya mauaji ya wazee wanaoshukiwa kuwa wachawi pande za Kilifi. Msanii huyo aliyetamba kwa kibao tarumbeta,Nylon guitar,Visingizo,Niringe naye na vinginevyo amedokeza haya kupitia ukurasa wake wa facebook akikashifu vikali vitendo hivyo. P-day alisema ya kwamba usemi wake anaopenda kuusema kwa nyimbo zake....."MZEE HATEMEWI MATE" unapaswa kuwa kauli mbiu itakayochukuliwa na kuwekwa kama mtajo utakaowaokao wazee kutoka kwenye janga hili. Tukinukuu kutoka alichonakili kwenye akaunti yake ya facebook..... "Social cohesion department to buy the mzee hatemewi mate lebol ( uzee si uchawi ) nliamka tu nkatunga hii lebol din't know itafika huku ........Sasa vijana kilifi county walianza kuua wazee kwa kua niwachawi BT sio Kila mwenye mvi ni mchawi ..let's respect the old" JE MAONI YAKO NI YAPI KUHUSIANA NA PENDEKEZO LA P-DAY KUHUSIANA NA WAZEE KUUAWA?