BIFU YA DIAMOND NA ALIKIBA, NI SIASA YA TANZANIA. SAUTI SOL YAFUNGUKA
Baada ya kuangusha kibao Unconditional Bae waliyomshirikisha Mkali wa BongoFlava Ali Kiba, Savara Mudigi ambaye ni member wa Sauti Sol, amefunguka na kusema kufanya kazi kwao na Ali Kiba ni hali ya kikazi tu. “Mambo ya Alikiba na Diamond hiyo ni siasa ya Tanzania,” member wa kundi hilo, Savara amekiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka aliyeuliza iwapo kundi hilo linaona kuwa uimbaji wa Alikiba unaendana zaidi na mtindo wao kuliko wa Diamond. “Mimi ni msanii, yule ambaye anakuja wa kwanza na yule ninayefeel vibe yake nitafanya naye muziki, muziki utafanywa kila siku, haijalishwi unafanya na nani, mimi nitafanya hata collabo na Diamond, tutafanya collabo na msanii mwingine yeyote,” amesema.