Posts

Showing posts from May, 2015

MWENDA TEZI NA OMO MAREJEO NI.......????

Image
Baada ya kutengana na produza Tk2 kutokana na tofauti zilizozuka kati ya msanii Susumila na studio ya Number records.Chikuzee aliwachwa mataani asijue la kufanya.Kimya hiki kilizua maswali mengi na matokeo yalimfanya msanii Chikuzee kuingia mitini kisanaa asijue la kufanya.Jana produza Tk2 wa Number one records alivunja ukimya na kusema due to public demand ameamua kumchukua ChikuZee tena ili kufanya kazi naye.Tayari produza na msanii huyu wametayarisha kibao kipya kwa jina Simuachi.Ama kweli mwenda tezi na omo marejeo.......ni ngamani.

VITA ULIANZIA WAPI KATI YA MADINI KENYA CLASSIC NA KAA LA MOTO KIUMBE?

Image
 Msanii mwenye miondoko wenye flava za kibongo au mwana mlezi wa mapenzi anaejulikana kwa jina Madini Kenya Classic amponda msanii wa pwani mwenye mtindo wa kufoka anaetajika kwa jina la Kaa La Moto Kiumbe kwamba hana mashairi mazito za kuvutia na kuleta maana kwenye jamii kama ilivyo ada msanii kio cha jamii ila anaungaunga kwa kutaja watu majina kama vile wasanii wenzake na wanasiasa jambo ambalo kama msanii kidogo inakera ila Madini anazidi kusema hata hivyo ana ujanja ya kufanya mashabiki zake wapagawe anasema Kaa La Moto anaiga msanii wa Tanzania maarufu kama ‪#‎ FidQ‬ ila bado hajagundua mtindo wake kama mchanaji ...akielezea wasanii ambao anawakubali amewataja kwenye mchezo wa hiphop anamtaja... ‪#‎ Kaligraph‬ ‪#‎ CrazyK‬ ‪#‎ Rabbit‬ na cha ajabu akagusia msanii chipkizi anae julikana kama ‪#‎ Noblemirror92‬ na kusema anamkubali sana kwani huyu msanii amewahi mvitia kwa mistari wenye ukomavu....Hata hivyo alimalizia kusema kwamba amewahi fanya kazi na Kaa ...

MASSIGER-BANANGE VIDEO KALI SANA!!!!!

Image
Huku wanamuziki wa Kenya wakizidi kuparamia kwenye tasnia ya muziki wa Afrika mashariki.Msanii mpya kabisa kwenye ulingo wa hii sanaa ameamua kuingia ndani ya studio kubwa nchini Kenya Ogopa djs na kufanya video itakayo wazuzua wengi.Msanii Massiger ameachia video yake kwa jina BANANGE na bila shaka video hiii ni ya kipekee kwani imeandaliwa kwa hali juu.Pata kuitazama

MTAZAME MSANII WA HIPHOP AKIMPA KICHAPO MSANII WA GOSPE(VIDEO).......WAAAAH HUTAAMINI

Image

DAAAAAAHHHHHHHH..........HII NI SHIDAAAAA!!!!!!!!! LABDA HAYA NI MANENO YA PRESENTA GATES MGENGE BAADA YA SHOW YA MAMANGINA??

Image
 Baada ya baadhi ya wasanii kulalimika baada ya show ya juzi ya Mamangina. Presenta Eric Gates wa Mashavmashav aliyekuwa mc hiyo siku, jamaa huyo aliamua kupachika maneno fulani ambayo hatuwezi sema ni ya mistari ya nyimbo fulani au fikira zake kwa wanaomzungumzia mabaya....... Gates aliandika haya(TUKINUU)..... . Eric Mmu Bonga mbaya mi na cheka .....kama Ni ganji nitaokota.Natesa Yesterday at 15:18 · Public Hayo ni tisa,kumi ni kuwa wasiwasi wako ndilo jibu lako!!!

DJ IVORY(PEMBE ZA NDOVU) VS DJ BUNDUKI (MARISASI) WAKIKWARIZANA NANI MKALI ZAIDI KWA MIXX?

Image
Pwani imezidi kupanuka na kukua kubwa zaidi kwa showbiz. Hivyo basi vipaji vipya vimeenuka na vijana wengi wanasema wazee wanapaswa kufunga mizigo waende retire. Sasa dj Ivory amewasili na dj Bunduki alikuwapo ila wamkubali nani zaidi?  

NATAKA KUM****** SOCILITE HUDDAH MONROE -ODINAREH BINGWA APASUA MBARIKA!!!!

Image
Odinareh yule ambaye wengi wetu humuita bingwa amezuka tena. Jamaa huyo ambaye huwa na maneno mazito na hulka za kutajikatajika kila mara ameamua kutoa dukuduku lake la moyo. Odibareh alikuja bayana na kudai kuwa anamzimia sana sociliate Huddah monroe na anatamani kum***** sana!!! "Namtafuta kwa udi na uvumba na tayari mikakati nishaweka kwa hivyo nipo safarini kuelekea Nairobi",alisema Bingwa. Huku hayo yakizidi kujiri, rapper huyu kwa sasa anapepea angani kwa kibao chake kipya ALL NIGHT LONG ambacho kinatikisa spika kwa redio stesheni zote nchini Kwa sasa kibao hicho kipo nambari tatu kwenye radio show ya capital fm hits not homework. Je Huddah upo tayari...manake una rambo naye bingwa ana mua!!

"WACHENI KUBANIA WASANII DANCEHALL HAPA NCHINI" PROMOTER SELECTA KRAS ASEMA!!

Image
Huku kivumbi kikizidi tifuka kwenye ulingo wa sanaa ya Kenya,yaonekana kuna kundi flani la wasanii limesaulika.Kusaulika kwao kumeleta gumzo la kiuhakika ndiposa promoter wa muziki Selector Kras akapasua mbarika.Selekta Kras ambaye ni CEO wa Reunion entertainment alizua malalamishi kuwa wasanii wa dancehall na ragga wametengwa sana hapa Kenya.Kras aliongeza msumari moto kwenye kidonda pale aliposema kuwa wasanii wanaothaminiwa wa dancehall ni Wyre na Redsan pekee. Kwanini tutumie mate ilhali wino upo, soma alivyosema hapa........ .... " ‪#‎ SADDEST‬ ‪#‎ TRUTH‬ Most radio listeners cant list beyond two Kenyan reggae / dancehall artists they'll start with ‪#‎ Redsan‬ and stop at ‪#‎ Wyre‬ who has since moved to lingala ... " Hayo Ni maoni yake tu.Je yako Ni yapi?????