FAHAMU MSANII WAKO : MAHOJIANO NA MSANII HARUN DEEY

FAHAMU MSANII WAKO : MAHOJIANO NA MSANII HARUN DEEY


PWANI USANII:HARUN DEEY NI NANI HASWA?

HARUN : Harun Iddy almaarufu Harun Deey alizaliwa 22/02/1997 na nilianza muziki alnikiwa na umri wa miaka kumi na sita.

PWANI USANII:NYIMBO YAKO YA KWANZA ILIKUA GANI?

HARUN: NASUBIRI ndiyo iliyokuwa nyimbo yangu ya kwanza ikifuatiziwa na NYOTA, zote nilizifanya Liwazo records,Mombasa.

PWANI USANII:LABDA ULIANZA KUPATA UFANISI LINI KWENYE TASNIA YA MUZIKI?

HARUN: Nilianza kupata ufanisi kupitia kwa wimbo wangu wa tatu unaojulikana kama BOSS DON ulioniwezesha kupata show kwenye vilabu tofauti vikiwemo HYPNOTICA (VIPAJI NIGHT), Z LOUNGE (XTRAVANGANZA NIGHT) na DANS LOUNGE (CELEBRITY THURSDAYS). Vilevile siwezi upuuzia wimbo wangu unaojulikana kama MAJARIBU manake ndio ulionipatia video yangu ya kwanza.


PWANI USANII:JE VIDEO YA MAJARIBU ILIFANYA VYEMA AMA?

HARUN: Ndio ilifanya vyema,iliweza kuchezwa kwenye Y254'S PWANI SHOW,Y IN THE MORNING,KBC na RAIA TV.

PWANI USANII:NYIMBO ZAKO HUFANYIA STUDIO IPI?

HARUN:Nyimbo zangu zote zimefanywa na King Ian Michapo studio ni Liwazo Records

PWANI USANII:MALENGO YAKO YA KIMUZIKI NI YAPI?

HARUN: Malengo yangu ya mziki ni kua miongoni mwa wasanii hitajika Ulimwenguni.

PWANI USANII:LABDA UNA ADVICE YOYOTE KWA WASANII WENZAKO?

HARUN: Yeah,advice yangu ni,wasanii watie bidii na wawe wakarimu kwa yoyote yule bila kujali umri au hadhi ya mtu.

PWANI USANII: KANDO NA KUFANYA MUZIKI UNAJISHUGHULISHA NA MAMBO GANI MENGINE?

HARUN: Mimi ni mwanabiashara ndogo ndogo apa nchini

PWANI USANII:UNGEPENDA KUFANYA COLLABO NA NANI MBELENI?

HARUN: Ningependa kufanya collabo na wasanii kama Otile Brown na King Kaka hapa Kenya. Nje ya nchi ningependa sana kufanya kazi na kundi zima la WCB wasafi.

Comments

  1. Harun DEEY I love your courage forward ever backward never

    ReplyDelete
  2. Harun DEEY I love your courage forward ever backward never

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA

MSANII KIJANA RANNY WA KADEM KUMBE KAJIUNGA NA KIKOSI CHA POLISI........pata uhondo hapa.