Posts

Showing posts from 2016

PWANI USANII ONLINE RADIO. LISTEN HERE!!!

Image
PWANI USANII ONLINE RADIO FEATURING NASSIZU MURUME,IDDI SINGER,NEPTUNE RECORDS, WYNAS,BABLUE AKA ANTONIO LISTEN HERE - >> https://www.spreaker.com/user/9366849/pwani-usanii-online-radio-featuring-nass SEND US YOUR MUSIC THROUGH pwanimusiknewsgodwinpwani@gmail.com or contact us through 0723 936960 for at enquiries. We also do adverts.

UIMBAJI NA UCHORAJI NDICHO KIPENZI CHA MSANII J'S.

Image
UIMBAJI NA UCHORAJI NDICHO KIPENZI CHA MSANII J'S. Ama kweli Mungu hutujalia kwa vipawa tofauti tofauti ila kwa Joseph Ngila,Mungu amemjalia vipaji viwili ambayo vyote anavitumia kujifunufaisha na kuelimisha jamii. Joseph Ngila Ngonzi almaarufu J'S ni mzawa wa papa hapa Mombasa eneo la Changamwe Soweto kisumu ndogo. Uchoraji wake na uimbaji ulianzia shule ya msingi ya Mwijabu. Kwa umri mdogo sana,J'S aliwashangaza wengi kwa kuchora picha zenye mvuto zilizompelekea yeye kuwa kipenzi cha walimu,akiwasaidia kuchora chati na mabango ya shule. Tukija kwa kipaji chake cha uimbaji,J'S alikuwa na haya ya kueleza....... "Nilianza kuimba nikiwa na miaka kumi na mbili ila utunzi wa nyimbo nilianza mwaka wa 2000.Niliupenda muziki jambo lililopelekea mimi kuunda kundi Langu la muziki lililojulikana kamaJ.E aka Joseric." Kwa sasa msanii J'S yupo na ujio mpya kabisa chini ya Bullet music na ataiwachilia nyimbo hiyo hibi karibuni. Nyimbo yenyewe inajulikana k

DULLY MELODY AMPONGEZA DIRECTOR WA VIDEO YAKE YA KIVUMBI.

Image
Video Director:Thomas. DULLY MELODY AMPONGEZA DIRECTOR WA VIDEO YAKE YA KIVUMBI. Supasta anayechipukia kwa kasi, Dully Melody amekuja wazi na kumpongeza mwandalizi wa video ya wimbo wake 'KIVUMBI' Dully, alimpongeza sana director Thomas Tomsy anayetokea Nakuru na akasema kuwa jamaa huyo ni mwenye moyo mzuri wa kusaidia na kukuza vipaji. "Sio kwamba eti pwani hakuna waandalizi wazuri wa video,wapo wengi sana ila nilipendelea kufanya kazi na director Thomas kwa kuwa Thomas alianza kunifuatilia mimi kama msanii pindi tu aliposikia nyimbo yangu ya kwanza hongera.Japo yupo Nakuru,amekua akinipa motisha na hata kusambaza muziki wangu sana ndiposa nikaona nifanye kazi naye na vilevile kwa sababu Thomas yupo Nakuru na mimi nipo Pwani basi ni kama tutakuwa tukeshika Kenya nzima kwa ushirikiano wetu kutoka magatuzi tofauti."Alitusimulia Dully. Video ya Kivumbi ambapo Dully amemshirikisha rapper wa kike CML tayari ishakamilishwa uandalizi na hivi karibuni basi itawach

NASSIZU MURUME AWACHILIA MAWAZO

Image
Baada ya kuwa signed na label ya Watanashati Classics, msanii Nassizu Murume ameachilia kibao kingine kwa jina Mawazo. Nassizu ambaye tayari ameachilia nyimbo kadhaa ikiwemo Sindi, amekuwa aking'ara hasa baada ya kazi zake kupokelewa vyema  na media. Watanashati Classics ndio kampuni iliyoandaa show ya Diamond Platnumz miezi kadhaa iliyopita, huko Meru. Tazama video yenyewe hapa

CHANGAMOTO ZINAZOWAKUMBA WASANII WA LAMU.

Image
Wengi Wetu tunausikia mji wa Lamu kwa utajiri wake wa kitalii na tamaduni za kiswazi ila hatujui kwamba wapo wasanii wa kizazi kipya wanaofanya muziki kwa bidii. Tulijaribu kuwasiliana na baadhi ya wasanii wanaotokea Lamu na walikua na mengi ya kutueleza kuhusu kufanya muziki Lamu. Kikosi cha IslandLove records kikiongozwa na meneja wao kwa jina Enoch,walituwekea mambo bayana. Man Azzer na producer Doni ambaye vilevile ni msanii walipasua mbarika na kusema kuwa wasanii wa Lamu hawadhaminiwi na kuheshimiwa kama wenzao wa Mombasa. "Kaunti yetu ya Lamu haithamini kazi za wasanii wa kizazi kipya. Katika tamasha za viongozi wa serikali au wanasiasa hatuitwi wala kupata hata mualiko wa kutuimbuiza na kuonyesha vipaji vyetu." Alieleza Man Azzer. Vilevile Produza Doni aliongezea kuwa vituo vya redio vya pwani vimewatenga sana wasanii wa Lamu. Doni alikua na haya ya kusema kuhusiana na swala la redio......" Stesheni za pwani zimewakandamiza sana wasanii wa Lamu na La

LA TUKUL KUACHIA KIBAO KIPYA: ZUNGUSHA

Image
Msanii anayechipukia kwa sanaa,La Tukul ameamua kuwaonjesha mashabiki wa muziki utamu wake kabla mwaka uishe. Msanii huyu ameamua liwe liwalo hadi raundi hii apige bao kisanaa. Kibao chake "zungusha" tayari kishaiva toka studio za Thundersound chini ya Produza Morbiz. Pindi tu mambo yakiwa tayari basi,wimbo zungusha mtaupata kwenye akaunti za mdundo,YouTube na nyinginezo.

ALIKIBA SIO KAKANGU ! MSANII AFUNGUKA.

Image
ALIKIBA SIO KAKANGU ! MSANII AFUNGUKA. Baada ya kutambulika kwenye road show ya Meru iliyoongozwa na comedian Churchill,msanii Nassizu Murume aliyesajiliwa na lebo ya Watanashati classic entertainment amekuja wazi na kukana madai yanayosambaa mitandaoni kuwa yeye ni kakaye msanii wa Bongo,Alikiba. Habari hizi zilipamba moto hasa pale video ya wimbo wake 'mawazo' ilipodondoshwa na wengi walidhani ni nduguye Alikiba.Unapotazama video mawazo ya msanii huyu basi bila shaka utamfananisha na Alikiba kwani kisura na sauti wameona vilivyo.Tulipata kuwasiliana na meneja wa lebo ya Watanashati classic entertainment kuhusiana na swala zima la msanii wake kuitwa nduguye Alikiba.Alikuwa na haya ya kunena........ "Wengi wamekuwa wakimfananisha na Alikiba na walidhani ni kakake ila msanii wetu Nassizu anapinga na kusema hana uhusiano wowote na Kiba ila urafiki wa karibu tu. Kwa sasa kazi zake zinafanywa chini ya Watanashati classic." PATA KUITAZAMA VIDEO YAKE YA "MAW

HII MTAIWEZA? STYLE MPYA YA DIAMOND PLATNUMZ, TAZAMA PICHA HAPA

Image
Mkali wa Bongofleva Diamond Platnumz ni msanii ambaye kwa sasa anayesemekana kuwa na uwezo mkubwa kifedha na pia  kiumaaraufu kutoka Africa Mashariki. Licha ya kushikilia style yake ya kimziki, CEO huyo wa WCB pia amekuwa akitoa mitindo kadhaa ya fashion na kama kawaida, hajakosa wakumfuata, hasa hapa Pwani. Baada ya kushinda tuzo 35 kwenye career yake ya kimziki, Diamond ametoka na style mpya. Je, atapata wa kunfuata? Tazama picha hapa PHOTOS (COURTESY)

MEET STEVE ES TAKING VIDEO PRODUCTION TO THE NEXT LEVEL.

Image
Story narrated by Steve Es himself... Lights!Camera!Action! "I started film way back in 2014. My inspiration came from watching the last airbender i was so drawn to learn the visual effects used so i started reasearching on some editing softwares. I started with windows movie maker went to hitfilm before finally landing on after effects I learned the basics and advanced stuff through youtube tutorials. I did a couple of projects in coast with artists like; Team ocean money Shelly kings Airbase family Around two months ago i got signed in bigdreams and i now work with Ricky Bekko. I, m set to realease my first project under big dreams some time this year."

PRODUZA GOGOLOW ARUDI KIMUZIKI BAADA YA KUPOTEA KWA UTEJA

Image
SIMULIZI ZAKE PRODUCER GOGOLOW.......... "Mwaka wa 2013 nilikuwa drug dealer nikiwa Rage records by 2014 nikaanza kutumia madawa while selling them.Kwa kweli biashara ikaja kubuma,nikaendelea kwenda mbio kwa ajili ya kupona kwangu sasa while I was having a family depending on me. Mwaka 2015 mwezi wa May nikaenda rehab kampuni moja inaitwa reachout rehabilitation centre kwa 4 months then baaa ya kutoka nikakaa kiasi then nikarelapse tena mpaka this year.Kwa kweli ilinirudisha nyuma kimziki,ila sijakata tamaa nimerudi tena ndani ya Malindi nafanya mambo kama kawa.Baada ya kufungwa jela kwa mwaka mmoja but bahati nzuri nikaachiliwa by power of mercy yaani msamaha wa Rais.Ujumbe wangu kwa ndugu ni waquit drugs waenjoy their lives with their families."

MEET THE HIGH SCHOOL PRINCE FROM LAMU,MUSICALLY BLESSED!

Image
As interviewed by Pwani Usanii. PWANI USANII:WHATS YOUR REAL NAME AND WHAT NAME DP YOU USE ON STAGE? MAN DULLA:My government name is Abdul Aziz Abdallah and my stage name is Man Dulla A.K.A Dula del Reshy. I also use Drazzey as my stage name too...quite a lot of names there! PWANI USANII: YOU LOOK YOUNG,HOW OLD ARE YOU? MAN DULLA:I'm 17 years old and i'm Still a student at Wiyoni Secondary school. PWANI USANII:WHEN DID YOU START MUSIC? MAN DULLA:I used to write music for quite a long time but I started recording early this year around April. PWANI USANII: HOW DO YOU HANDLE MUSIC AND SCHOOL? MAN DULLA:I never visit the studio when the school calendar is on. Mostly,I attend my recording sessions during the holiday. PWANI USANII:WHAT TYPE OF MUSIC DO YOU DO? MAN DULLA:When i started music i used to rap and do all hiphop stuff but i later found out that my potential was in swahili RnB and Afro-pop. PWANI USANII:HOW MANY SONGS HAVE YOU RECORDED SO FAR? MQN DULL

HUBA MAHABA! MSANII DULLY MELODY KUMBE MPENZI WA RAPPER CML??

Image
Chambilecho wahenga,mapenzi ni kama kikohozi hayafichiki,hivyo basi msanii Dully melody ameamua kumwaga mtama waziwazi penye kuku wengi.Dully alizimwaga hisia zake kwa mwanadada CML mwanamziki wa Hiphop kutoka mkoani pwani.Msanii huyu wa kibao cha YAGAYAGA ameeleza kwamba anavutiwa na vitu vingi vilivyopelekea yeye kumpenda... "CML ni mrembo sana,wengi wanatamani kuwa naye ,hana dharau,wala kiburi.Ana uwezo mkubwa kwenye gemu,napenda kazi zake na zaidi ana roho safi sana.Sijasikia amegombana na mtu au ana bifu,"alitudokezea Dully. Ukaribu wao ndio uliochangia uhusiano wao kukuwa na kuamua kuwa wazi katika mitandao ya pasipo kuogopa.Hii ni baada ya wawili hao kuonekana Ukunda wikendi iliyopita na baadhi ya watu kuzungumzia. Kutoka upande wa CML ,ambaye ni MSANII wa kike anayefoka ajabu na anayesifika kwa kibao chake cha 'Bao nishafunga',haikua rahisi kupata jibu lake kuhusu uhusiano huo kwani hivi ndivyo alivyosema, "Love is a beautiful thing and every

MC MIKE KAMA MC BORA NCHINI.SOMA HAPA!!

Image
MC MIKE KAMA MC BORA NCHINI.SOMA HAPA!! Ni kijana mtanashati na mwenye bidii sana,MC Mike. Baada ya kuwaburudisha kwa nyimbo za gospel kabambe,jamaa huyu alijibwaga mzima mzima kwenye ulingo wa kuburudisha hadhira kutumia usemi. Alikuwa kwenye Masaku Sevens kama Mc na Youth TV akizuru shule mbalimbali. MC MIKE ameteuliwa kwenye Xtreem Teeniz Awards na kumpigia kura SMS AH3 kwa nambari 21921. Name: Mike Nderitu Karemi Stage Name: Mc Mike County :Mombasa FB: MC MIKE IG: Mc_Mike_Kenya Twitter: MC Mike Kenya PWANI USANII:WHO IS MC MIKE? MC MIKE:Mc Mike is an Emcee, a tv host and event organiser. Pwani Usanii:How did you start emceeing? MC MIKE:I started as an artist and recorded some powerful gospel songs which upto-date are played in the local radio stations in Mombasa and Nairobi then later i bacame a deejay for three years.Then 2013 I went to a friends album launch and the mc failed to turn up so i decided "kuokolea" after the event everybody was aski

Sauti Sol and Nyashinski better than gospel artistes, asema Procuer Amz

Image
Huku wasanii wa muziki wa injili wakijipata kwenye corner, Producer Amz wa Tempoz Records ametoa kauli yake kuhusiana na utata wa nyimbo za injili. Kulingana na Amz, Wasaniii wa nyimbo za Gospel wanaoibuka wameshindwa na kazi, huku akidai wasanii wa secular Sauti Sol na Rapper tajika Nyashinski wanafanya kazi hiyo zaidi yao.
Image
Baada ya kuachilia too Much, rapper kutoka bongo Darassa ameingia studio mara ya pili na Ben Pol na kuachilia ngoma kwa jina Muziki. Kazi iliyofanywa na ma producer watatu tajika kutoka TZ, Mr. Vs, Abbah and Mr T Touch. Video yenyewe ilitayarishwa na Hanscana. Icheki hapa

NEW VIDEO ALERT: NISEME NAWE - OTILE BROWN FT BARAKA THE PRINCE

Image
Otile Brown amevuka border na ameachilia wimbo kwa jina Niseme Nawe aliomshirikisha msanii tajika kutoka TZ, Baraka The Prince. Wimbo wenyewe umetayarishwa na producer Teddy B huku Video yenyewe ikifanyiwa kazi na Dr Eddie. Icheki hapa ===>> 

CELEBRATED KENYAN RAPPER NYASHINSKI SHINES IN COLLABO WITH YEMI ALADE & TZ SINGER RUBY

Image
    Multi-talented Kenyan artiste Nyashinski of the famed music group Kleptomaniax has made Kenyans proud by his stellar performance on Coke Studio Africa season 4. Last weekend he premiered on the show for the first time, collaborating with Nigerian MTV Award-winning Best Female Artist Yemi Alade performing the song Forever by Tanzanian power vocalist Ruby.  Watch it here:  https://www.youtube.com/watch?v=LOcvmgoVq_M Speaking about his entrant into the show and working with the divas, Nyashinski said, “I had a great time recording at Coke Studio and I am so happy with our performance – the feedback was mind blowing! I am just honoured to have been paired with the two ladies, as they are both so talented and have beautiful voices.” The Ruby, Yemi Alade and Nyashinski collabo produced by Chopstixx was a triple threat combination as the version of Ruby’s Forever took into a Zouk-ish live performance played by the Coke Studio Africa House Band.   In F