Je msanii Susumila alimwacha mkewe sababu yake Kush Tracey?



Baada ya kukiri kuachana na mkewe, msanii tajika Susumila almaarufu "Mr President" , anadaiwa kuwa na ukuruba wa kimapenzi na msanii wa kike kutoka Nairobi, Kush Tracey msanii anayetamba na ngoma ya Huezi Nidandia. Akihojiwa na kituo kimoja cha radio mjini Mombasa, Susumila aliweka bayana kuachana na mkewe ambaye amezaa naye watoto wawili. "Yeah ni kweli tuliachana na mke wangu" alikiri msanii huyo. Alipoulizwa kuhusiana na Kush Tracey ambaye tayari ashafanya naye colabo kama ana uhusiano wa kimapenzi naye alijibu kwa ufupi "No comment".

Naye Kush Tracey alipoulizwa kama yeye ndiye aliyemfanya Susu kuachana na mkewe ili ampate Susumila pia yeye alijibu,"No comment".
Wawili hao tayari washafanya collabo inayotamba kwa jina Umenitosha, ngoma iliyosukwa na AMZ na Amoh
Lakini maswali yanayo wagonga vichwa mashabiki na washikadau wa mziki ni je wasanii hawa wawili wanauhusiano wakimapenzi au ni mziki tu? Mambo ya collabo hayo.
By Nina Kagia

Comments

Popular posts from this blog

SUDI MANJEWAYNE :THE PWANI KING OF DISS DISSES AGAIN IN HIS NEW SINGLE 'WATAJISHUKU"

WAZEE WETU WA KILIFI SIO WACHAWI-MSANII P-DAY AONGEA