Alikimya baada kufunga ndoa, wengi tulipodhani kwamba atauwacha muziki na kufukuzana na mambo ya familia,rapper mkali tokea Pwani Kaa La Moto Kiumbe alibadili kibamba na kutobadili mkondo. Kaa la Moto aliachia video yake 'MAJINI' iliyoandaliwa na Johnson Kyalo. Video hiyo, yasemekana kwamba iliandaliwa Mara mbili baada ya mkoba wa director Johnson Kyalo kupotea na vifaa pamoja na data zote za video hiyo. Video ya MAJINI iliyoandaliwa Lamu, ilipata pigo zaidi pale model alipokataa kurudia shooting ilhali alikua amelipwa. Hata hivyo, La Moto hakufa moyo... Video ilifanywa kwa Mara ya pili na matokeo yalikua haya -- TAZAMA HAPA - - - - > https://youtu.be/TlGEeY-ZPQ0